Business ideas (Bure)

Kupata faida sio tatizo tatizo ni mabadiliko yanayotokana na biashara na mazingira tuliyo nayo kwanza kama uko tayari kufanya biashara wekeza hata milioni mbili kwanza kwenye biashara utayo chagua kuifanya utakapo kuwa tayar umeona changamoto zake na ukaweza kuzitatua hapo ongeza mtaji ili uweze kupata faida zaidi
 
Habari wanajamvi, nimebahatika kupata milioni 15, naombeni wazo la biashara itakayonipa atleast 2M per Month. Maoni yote yanakaribishwa.
Asanteni
Mkuu, ukitaka kufanikiwa ki biashara, usiwaze faida kwanza. Tengeneza ndoto kwanza halafu fijiria namna gani utafanikisha ndoto yako. Faida itakuja baada ya juhudi zako na namna unavyoendeleza ndoto yako. Hivyo kama unataka kufanikiwa, acha kufikiria faida kwanza. Acha faida ije kama matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama utaweza kanunue mazao katavi sehemu moja inaitwa bonde la mpimbwe katika vijiji vya kibaoni kwao na mh.pinda,usevya,tupindo,mbede,mwamapuli,chamalendi,ukingwa na vijiji vyote vya bonde hilo,nenda kanunue mahindi kwa gunia tsh 40 mpaka 50 hiyo ni bei ya kununulia,ukifika tafuta dalali wa kukununulia mzigo kutoka vijijini utamlipa kila gunia sh.1000,usafiri wa gunia kutoka kijijini hadi maeneo ambayo gari inaweza kupita haizidi sh 2000_3000,kipindi unakusanya mzigo wako unapanga chumba cha kuishi hapo hapo kijijini ikibidi unapanga na chumba cha kuhifadhia mazao yako ukiwa na dalali watatu ndani ya wiki mbili umekusanya mzigo wa kutosha na magari ni mengi sana yanayobeba mazao kutoka huko katavi kuleta mikoa mingine,gharama ya gunia moja kulisafirisha kulitoa mfano majimoto au mwamapuli kijijini kulileta shy,mwanza au bariadi ni tsh 10000 ikijumuisha nauli,kupakiza na kushusha gunia kwahyo ukiwa na gunia 100 utazisafirisha kwa gharama ya milioni 1,000,000 ukiyafikisha mazao mkoani unayaweka stoo kwanza kusibili bei iwe nzuri kuanzia miezi ya kumi na mbili,wa kwanza na wa pili ndipo unasukuma mzigo wako ukiwa makini faida utatengeneza si chini ya sh 40 elfu kwa gunia hapo tumetoa gharama zote za usafiri,dalali,mfuko,stoo ya muda,watu wa kuyasafisha na kuyawekea dawa mahindi ili yasipeche kwa urahisi mf una gunia 100 utatengeneza faida ya 4milioni ndani ya miezi kuanzia huu wa nane hadi wa pili mwakani ambpo mzigo wako utauza tena ukiwa umetulia kwako, if upo seriazi andaa ml.5 ya kuanzia biashara hiyo,pia kuna mazao kama karanga yanabei mbaya sana kule gunia debe sita sh.elfu 30 ni wewe kuchagua maindi au karanga.ukiwa tayari nitafute nikuunganishe pale pale kijijini kwa mawakala wanao nunua mazao na sehemu ya kuhifadhia natumia simu nimechoka kuandika ukihitaji nitakufafanulia vizuri zaidi,mkuu kazi kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka ukibeba magunia kwenye fuso linalozidi tani 1, ushuru unakuhusu.
 
Kwa sasa biashara nyingi zimekuwa ngumu kutokana na upatikaji wa fedha pia kodi ambayo pia ni muhimu kuilipa.
Ni vyema ukaangalia biashara itakayokuweka huru na kazi yako,yaan uendelee na ajira yako huku biashara inaendelea.

Mim nakushauri uanzishe biashara ya duka la madawa muhimu ya binadamu.

Mahitaj yake ni lazima uwe na kibali cha umiliki pia tafuta muuzaj ambaye awe na taaluma husika
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu uanzishaj wa duka la dawa mtafute mfamasia anayefanya kazi ktk hospitali ya serikali atakufafanulia zaidi kuhusu kibali,muuzaji,location,common drugs na tathmini ya mtaji.
Au unaweza kuonana na waliokwisha anza hii biashara kitambo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: _ID

Similar Discussions

127 Reactions
Reply
Back
Top Bottom