Business ideas (Bure)

Maana yangu ya kukushauri usahau kwanza mawazo ya mil 2 kwa mwezi faida nilitaka nikushauri hivi , kwa sasa ni wakati wa mavuno maeneo mbali mbali nchini unaweza kuwekeza fedha kwenye mpunga ni mfano tu ukanunua ukatunza ukauza baada ya miez kama mitano. Hii inaweza kujibu ndoto yako kama ifuatavyo. Ikiwa gunia LA mpunga linauzwa 105,000 limeshakaa stoo kwa Bei ya sasa. Maana yake kwa pes yako utatunza gunia kama 140 za mpunga na zitaweza kukupa mchele kama kg 9000 hivi. Kwa lugha rahis hapa
inawezekana umestock mchele ukiwa tsh kama 1500 hivi kwa kilo. Ikitokea baada ya DEC . kumekuwa na Bei ya badiliko wakati wa scarcity unaweza uza mchele wote kwa tsh 2000 /kg jambo ambalo huwa linatokeaga, ingawa sio lazima , so utaweza pata mil 18. Out of your 15mil hivo profit yako ni kama 3ml. Na kwa miez 6 utakuwa umepata mshahara wa kawaida wa ofisa wa serkali 600, 000/month lakini hauna paye wala TRA . hii in kwa mpunga ,mahindi yana hesabu zake maharage mtama nk , kama utakumbuka nilitangulia kusema high risk high returns hakuna Biashara duniani yenye 100%. Ndo maana eenginr tunaingia na miguu yote na ni lazima uweke na roho ngumu. Kinyume chake utaanza kuzidonoa na hazitaitwa tena 15ml. changamoto ya hilo ni kwamba hatumwi MTU kuanzia kununua hadi kukabidhi stoo n lazima uwepo mwenyewe au mkeo. ubishololo pembeni kama unao, lazma uende shambani ulale huko had ujaze mzigo ukimwamini MTU yeyote wafaa . nafukiri yapo mengi ila huo kwa Leo ndo ushauri wangu kwako mjasiria Mali mtarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Kiukweli biashara ya kukupa faida hiyo labda ufanye sports betting tu usawa huu. Toa M1 anza kubeti kiakili pengine utafanikiwa zaidi. Maana ukijiroga kufungua biashara ya fremu tu haijalishi ni ya mtaji gani jiandae kisaikolojia kugawana faida na mamlaka ya mapato.

Utachezea mitama ya kutosha EFD,Kodi heavy na penalties za hapa na pale hadi akili ikae sawa. Hapo bado huja stabilize sokoni ni hatari sana.
uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo? backward reasoning.
 
Tafakari na hii.

Kama wewe sio muislam, Fanya Biashara ya kununua Mazao ya chakula kwa msimu Huu wa Mavuno na utakuja kuuza wakati wa njaa, yaani January- March.

Nitatolea mfano Biashara ya Mahindi. Kwa sasa hivi, Mahindi gunia la debe 7 kwa maeneo kama Gairo, Kibaigwa ba Mpwapwa na vijiji vyake ni wastani wa elfu 50.

Chukua Million 7 na ununue gunia za Mahindi, roughly utapata kama gunia 130.

Utahitaji viroba vya kuhifadhia mahindi yako, viroba 130 ni sawa na roughly Tshs 90,000 kwa maana ya kiroba kimoja ni Tshs 700 (Kariakoo)

Dawa ya kutunzia Mahindi dhidi ya wadudu, bei kwa kopo ni kama Tshs 4000 (Kariakoo) na kopo 1 linahudumu magunia ma4. Roughly utahitaji km makopo 30 ya dawa kwa gharama ya Tshs 120,000.

Sina uhakika kama una ghala lkn assumption ni kwamba magunia 130 utayahifadhi kwa muda wa miezi 6 kwa gharama chini ya Tshs 1m.

Kama kutakuwa na haja ya usafiri kutoka uliponunulia kupeleka ghalani, haitazidi Tshs laki 5. (Sifikirii ununue Mahindi Gairo afu ghala lipo Tabora)

Kuanzia January, bei ya mahindi hupanda kwa speed kubwa sana. Mf mpk kufikia March mwaka jana, gunia la debe 7 Mpwapwa lilifika Tshs 140,000.

Na hali huwa haipishani sana kwa mikoa mingi. Assumption ni kwamba bei zikibaki kama mwaka Jana, hutauza Mahindi yako chini ya Tshs 18m.

Naomba endelea na ukokotozi. Lakini ili ufanikiwe, nidhamu muhimu. Jiepusha na ushabiki wa kinachoitwa Timu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajamvi, nimebahatika kupata milioni 15, naombeni wazo la biashara itakayonipa atleast 2M per Month. Maoni yote yanakaribishwa.
Asanteni
Mimi Mkuu nikushauri tu kama una eneo japo la heka Moja hebu tafuta japo ngombe zako za maziwa japo 3 ambazo zitakupa an average y lita 60 kwa siku.. hapo hapo kazini kwako unapeleka hayo maziwa na kuyauza 2000 tshs per litre.. hio ni karibia 120,000 kwa siku.. kwa mwezi piga hesabu mwenywe.. than u continue evolving kidg kigd.. mwisho wa mwaka ngombe zina zaa.. unakua nazo 6...na hapo hapo unaendelea kujenga ujuzi.. Muhimu Usimamizi and Put ur Heart into it..

Ni hayo machache
iL Buono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama utaweza kanunue mazao katavi sehemu moja inaitwa bonde la mpimbwe katika vijiji vya kibaoni kwao na mh.pinda,usevya,tupindo,mbede,mwamapuli,chamalendi,ukingwa na vijiji vyote vya bonde hilo,nenda kanunue mahindi kwa gunia tsh 40 mpaka 50 hiyo ni bei ya kununulia,ukifika tafuta dalali wa kukununulia mzigo kutoka vijijini utamlipa kila gunia sh.1000,usafiri wa gunia kutoka kijijini hadi maeneo ambayo gari inaweza kupita haizidi sh 2000_3000,kipindi unakusanya mzigo wako unapanga chumba cha kuishi hapo hapo kijijini ikibidi unapanga na chumba cha kuhifadhia mazao yako ukiwa na dalali watatu ndani ya wiki mbili umekusanya mzigo wa kutosha na magari ni mengi sana yanayobeba mazao kutoka huko katavi kuleta mikoa mingine,gharama ya gunia moja kulisafirisha kulitoa mfano majimoto au mwamapuli kijijini kulileta shy,mwanza au bariadi ni tsh 10000 ikijumuisha nauli,kupakiza na kushusha gunia kwahyo ukiwa na gunia 100 utazisafirisha kwa gharama ya milioni 1,000,000 ukiyafikisha mazao mkoani unayaweka stoo kwanza kusibili bei iwe nzuri kuanzia miezi ya kumi na mbili,wa kwanza na wa pili ndipo unasukuma mzigo wako ukiwa makini faida utatengeneza si chini ya sh 40 elfu kwa gunia hapo tumetoa gharama zote za usafiri,dalali,mfuko,stoo ya muda,watu wa kuyasafisha na kuyawekea dawa mahindi ili yasipeche kwa urahisi mf una gunia 100 utatengeneza faida ya 4milioni ndani ya miezi kuanzia huu wa nane hadi wa pili mwakani ambpo mzigo wako utauza tena ukiwa umetulia kwako, if upo seriazi andaa ml.5 ya kuanzia biashara hiyo,pia kuna mazao kama karanga yanabei mbaya sana kule gunia debe sita sh.elfu 30 ni wewe kuchagua maindi au karanga.ukiwa tayari nitafute nikuunganishe pale pale kijijini kwa mawakala wanao nunua mazao na sehemu ya kuhifadhia natumia simu nimechoka kuandika ukihitaji nitakufafanulia vizuri zaidi,mkuu kazi kwako

Huu ushauri wako nimeupenda, actually ndio biashara nataka niifanye nikipata mtaji freshi. Kulima ni risky zaidi kuliko biashara ya ulanguzi.
 
Kifupi kwa siku wataka kuingiza sio chini ya 80,000/=, au 560,000/= kwa wiki, hapo ndio ufikirie ni biashara gani hasa ufanye na utaiweza.
 
kaongeze elimu, kama una degree kachukue MBA.

kitendo cha ww kutojua biashara ya kufanya, ni kiashiria kuwa elimu yako inahitaji kuongezwa kidogo.
Mawazo finyu kabisa haya,,mpe uahauri sio kupiga vijembe kama mwanamke, kwani kuomba ushauri ni vibaya,au hujui hata rais anawashauri wake ,daaah mijitu bhana roho mbaya kwelkwel ,usikute hata kwako mchoyo wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli biashara ya kukupa faida hiyo labda ufanye sports betting tu usawa huu. Toa M1 anza kubeti kiakili pengine utafanikiwa zaidi. Maana ukijiroga kufungua biashara ya fremu tu haijalishi ni ya mtaji gani jiandae kisaikolojia kugawana faida na mamlaka ya mapato.

Utachezea mitama ya kutosha EFD,Kodi heavy na penalties za hapa na pale hadi akili ikae sawa. Hapo bado huja stabilize sokoni ni hatari sana.
Kubet kiakili ni kwa namna gani mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom