Busara janga la Corona: Wakati CCM wakiahirisha mikutano, CHADEMA wang'ang'ania kufanya mikutano

Ndugu zangu,

Ili kupambana na janga la ugonjwa wa Corona CCM wametangaza kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi leo Ndg. Humphrey Polepole kuahirisha mikutano na mikusanyo yote inayoratibiwa na CCM.

''Ajizi nyumba ya njaa''; Mwenyekiti wa CHADEMA Ndg. Freeman Mbowe bado kakomaa kuhamasisha mikusanyiko ya kisiasa. Hii ndio busara mpya ya KUB?
Acha ujinga we Mzee!! una wajukuu sasa watajifumza mimi toka kwako?
 
KUB anajua kucheza na akili za wale watu, naona amefanya kitu kinachoendana na invitation to treat;). Akomalie hapohapo alafu ikifika siku ya tarehe husika anawatangazia watu wake kwamba anawaomba wasitishe kidogo atawatangazia tena lini waanze kazi
 
Upotoshaji upi kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba CDM wanataka waendelee na mikutano hata baada ya Waziri mkuu kusitisha mikusanyiko hiyo wakati unajua kabisa tamko la waziri mkuu limekuja baada ya tangazo la Mbowe.

Mada yako inawapotosha watu ambao hawajui yupi alianza kutoa tamko kati ya Waziri mkuu na Mbowe. Yaani unawaaminisha watu kuwa CDM wanapingana na serikali na hawajali afya za watanzania.

Coronavirus haina chama
 
tumia akili hata kidogo basi.
Ndugu zangu,

Ili kupambana na janga la ugonjwa wa Corona CCM wametangaza kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi leo Ndg. Humphrey Polepole kuahirisha mikutano na mikusanyo yote inayoratibiwa na CCM.

''Ajizi nyumba ya njaa''; Mwenyekiti wa CHADEMA Ndg. Freeman Mbowe bado kakomaa kuhamasisha mikusanyiko ya kisiasa. Hii ndio busara mpya ya KUB?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli kuwa CDM wanang'ang'ania mikutano.

Ikumbukwe kuwa tamko la Mbowe ilikuwa kabla ya katazo la mikusanyiko kwani mpaka jana jioni hata mh. Rais alikuwa akihutubia mikusanyiko.

Mh. Lema alishauri jana kuwa CORONA haichagui na Rais aache mikusanyiko.

Sasa imekuwaje mnashupaa na overtaken event?
 
Back
Top Bottom