Busara janga la Corona: Wakati CCM wakiahirisha mikutano, CHADEMA wang'ang'ania kufanya mikutano

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
14,975
2,000
Ndugu zangu,

Ili kupambana na janga la ugonjwa wa Corona CCM wametangaza kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi leo Ndg. Humphrey Polepole kuahirisha mikutano na mikusanyo yote inayoratibiwa na CCM.

''Ajizi nyumba ya njaa''; Mwenyekiti wa CHADEMA Ndg. Freeman Mbowe bado kakomaa kuhamasisha mikusanyiko ya kisiasa. Hii ndio busara mpya ya KUB?
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,101
2,000
Wakudadavuwa,
Angalia muda aliozungumza Mbowe na muda Ummy alipotoa tangazo kuhusu mgonjwa wa kwanza.

Kwa jambo kama hili naamini kwa asilimia 100% kuwa mamlaka ya uteuzi wa Ummy yalikuwa na taarifa lakini angalia kilichotokea barabarani Dar -Dom.

Kwa hapa nawatetea Chadema na nampa pole Mzee Polepole.
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,296
2,000
Wakudadavuwa,
busara ya Corona wenzetu Chadema waliianza tangu bungeni kabla Corona haijaingia nchini (proactive) but sisi CCM tumesubiri hadi Corona itusibu ndiyo tupate busara (passive).

wananchi wanaona na wanajua ni yupi mwenye busara kumzidi mwenziwe!
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,382
2,000
Kila kitu chadema kila kitu chadema ivi chadema imewatia nini nyie watu?

Ccm mna tatizo sana mmefanya mikutano miaka 5 bila wenzenu kufanya lakini bado hamjaweza kuwashawishi wapiga kura matokeo yake mmechezea uchaguzi serikali za mitaa.
 

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,531
2,000
Kupitia Corona ,watanzania tutaoata muda wa kuitafakari CHADEMA na nia yake mbaya kwa watu. Swali la msingi litakuwa , je CHADEMA ni chama Cha siasa kinachojali au kikundi kinachohitaji kuvuna ukwasi ?
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
9,929
2,000
Wewe umemshairi Polepole atoe press ya kuwashauri wananchi waipende ccm kwa vile imesitisha mikutano eti inawapenda? Na waichukie CHADEMA kwa vile imeitisha mikutano eti inataka wafe?

Kifupi huu utoto wenu wapelekeeni wapuuzi wenzenu mnaokesha nao kupiga ramli. Wananchi wanajua wakati Mbowe anatangaza mikutano hakukuwa na Tangazo rasmi la Waziri kuhusu kuwepo kwa Corona zaidi ya taarifa za Kigogo 2014,

baada ya Mbowe kutangaza mikutano ndo Ummy anakuja na taarifa za kuwepo mgonjwa huko Arusha. Hatudanganyiki na utoto wenu tafuteni Kiki nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom