Bus zuri Dar to Arusha

TAHMEED ya Nairobi ina mpk siti mtu mmoja...just alone...WiFi....Siti zina video na Audio player..unaweza kuweka flash yako ukasikiliza muziki wako Murua na Earphone....USB cable...
 
TAHMEED ya Nairobi ina mpk siti mtu mmoja...just alone...WiFi....Siti zina video na Audio player..unaweza kuweka flash yako ukasikiliza muziki wako Murua na Earphone....USB cable...
Tahmeed dar-nrb ni 2x2....lakin full uswahili makonda wanagombeza abiria kama wanapanda bure vile
 
Kwa mbali Kilimanjaro Express.. hayo mengine tupa kule

Kama uko na pesa pita juu chap na Fast Jet

Du! Hao Fast Jet unanichefua. Ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kutaka kukwea ndege nikakata ticket ya Fast Jet week mbili kabla. Ile najiandaa na usiku mrefu bila usingizi kwa wahaka wa kukwea mwewe, Mara PAAA!!! saa tisa usiku nikakutana na "Dear passenger,it is with regret that we advise your flight ........ has been cancelled...........". Mbaya zaidi kuna mshikaji alinitahadharisha na hilo ila nilikaidi. Mzee fasta nikakurupuka mapema nikafika Shekirango jikarukia Kilimanjaro. YAANI tunafika FFU moshi kitu hakiingii gea. Wakaanza kutufaurisha kwa mabasi mengine. Likapita TAHAMEED....mshangao site kama za ndege (ndege kwenye picha). Bahati mbaya walifanikiwa kufaulisha wawili tu,mie na wnzangu tukafaulishwa manasi mengine. Ile kurudi nikapania kupanda TAHAMEED. Nikakata ticket ya TAHAMEED kurudi, ile linakuja sio TAHMEED ile nilioiona kule FFU.
Ila Fast Jet walinifurahisha kitu kimoja. Ile nilivyoenda ku report kurudishiwa fedha walirudisha fast. Yaani ndani ya nusu saa tiGo Pesa ikajibu.
 
Back
Top Bottom