Bus zuri Dar to Arusha

tahmeed lina ac na choo.
kilimanjaro lina ac

hizo ndo basi nzuri unazoweza kupanda kwa njia hyo. huduma zao ni nzuri na hawana maudhi.
kuhusu hotel zipo lodge nzuri za bei hyo na zina usalama hapo hapo town
Asante sana mkuu. Kuna mtu kaniambia kuna Aspen Lodge unaifahamu? Usalama upo?
 
namba zao za simu cna kwa kwel... ila ukifika stand arusha pale ukiuliza utaonyeshwa. . haipo mbali sana na stand... n quality sana kwa kwel... mm mwenyewe nilishangaaa kukuta chumba kizur vile alafu ni affordable..
 
Basi zuri(Full Luxury) kuliko yote njia ya Dar -Arusha ni Tahmeed.baadhi ya hudumu zilizopo ndani ya basi ni 1.Huduma ya choo, 2.Huduma ya wifi bure 3.,Soft drinks bure(Maji na soda),Full AC, Seat zake ni nzuri,speed yai ni nzuri n.k.Ni Tahmeed pekee ambayo ukisoma mlangoni utakuta Sumatra wameandika (Daraja la Juu).nauli yao ni 33,000.Japo kipindi hiki nasikia wameshusha nauli mpaka 28,000(Sina uhakika). Ukiacha Tahmeed mabasi mengine ya dar -arusha yanafanana tu yote ni yale anbayo Sumatra wanayaita ya daraja la kati au daraja la kawaida.
 
Hilo Tahmeed zilikuwa vifuso mpaka juzi tu.?
Nayachukia kupita maelezo hata nauli ingenkuwa dala na ndani unapata pilao sipandi.
Lenyewe likiwa ccm mi ntakuwa ukawa, likiwa ukawa mi ntakuwa ccm tusikutane sehemu moja.
 
Kwa kuongelea uzoefu na sio majina napendekeza dar express
Angalia ile ya shs 33'000; wanayo class tofauti tofauti.

Kwa hiyo bajeti yako ya kulala jaribu AM, Golden rose, hizo zippo mijini kati...dkk tano kwa miguu kutoka stand
 
Basi zuri(Full Luxury) kuliko yote njia ya Dar -Arusha ni Tahmeed.baadhi ya hudumu zilizopo ndani ya basi ni 1.Huduma ya choo, 2.Huduma ya wifi bure 3.,Soft drinks bure(Maji na soda),Full AC, Seat zake ni nzuri,speed yai ni nzuri n.k.Ni Tahmeed pekee ambayo ukisoma mlangoni utakuta Sumatra wameandika (Daraja la Juu).nauli yao ni 33,000.Japo kipindi hiki nasikia wameshusha nauli mpaka 28,000(Sina uhakika). Ukiacha Tahmeed mabasi mengine ya dar -arusha yanafanana tu yote ni yale anbayo Sumatra wanayaita ya daraja la kati au daraja la kawaida.
Umezungumza kwa ufasaha kuliko wote humu,umesahau tv kila kona.njia ya dar to arusha ni tahmeed pekee ndio wamethibishwa na sumatra kuwa ni bus la kifahari(royals)
 
Bus nzuri sio AC bhana!,ni kufika tu salama ndio uzuri wa basi,panda Kilimanjaro au dar express pia yapo mengine mengi tuu!.Swala la hotel wewe nenda na Hela ya kutosha maana!.
 
Wakuu hasa wenyeji wa njia ya Dar - Arusha, naomba kujua Bus zuri (luxury) kuliko yote na la bei kubwa kuliko yote ni lipi na ni bei gani? Kwa wenyeji wa Arusha Hoteli gani nzuri ya kati ya Tsh. 30,000 - 50,000? Natanguliza shukrani zangu.

Kwa upande wa mabasi sina uhakika sana kwani tangu fastjet iingie mjini nimeyaweka pembeni kidogo. Nitakushauri kuhusu hotel nzuri na bei nafuu. Kuna hotel mpya inaitwa PEACE iko karibu sana na Chuo kikuu cha SAUT tawi la Arusha. Ni nzuri sana na wana breakfast nzuri pia. Bei zao ni 55,000/=, lakini wanaweza kupunguza hadi 50,000/=. Nilifikia hapo wiki mbili zilizopita na tulikuwa wengi pamoja na wanasheria walioenda Arusha kwenye mkutano wao wa mwaka. Hutojutia kufikia katika hoteli hiyo. Kama una gari binafsi, kuna parking yenye usalama wa kutosha. Goodluck.
 
Nilisafiri kwenda Arusha juzi kati pale nikapanda libasi fulani hivi tingatinga(jina silitaji nisije onekana nina majungu) wale jamaa wapiga debe wakalipamba lile tingatinga nikawapa nauli 25,000! mbaya zaidi ndio ilikua mara ya kwanza kwenda huko!

Niliichukia ile safari aisee! masiti yenyewe ni 2*3 huku vitoto vinalia!! gari ni kuukuu! nilikaa dirishani siti ya watu 3 kero tupu mara huyu anataka nimuitie wa korosho! mara huyu hivi! Next time siji kurudia ule ujinga. Mabasi ya kupanda nimeshayajua sasa watanikoma.
 
Back
Top Bottom