Bus la Maning nice linanyanyasa abiria

Bettina

Senior Member
May 3, 2009
102
24
Leo nimeshuhudia mtafaruku kati ya watumishi wa BUS LA MANING NICE na abiria wa kike ambaye ni mwanafunzi aliyesafiri kutokea Lindi kuja Kibaha. Ameshuka na makondakta wakamshushia begi na godoro la futi 3, wakamdai alipie godoro elfu30. Mwanafunzi akapigwa butwaa kwani anadai godoro huwa analipia elfu3. Basi akaambiwa alipie elfu10, yeye akawa na elfu5. Kilichofuatia ni purukushani ya kumnyang'anya godoro huyo msichana na kuondoka nalo kuelekea morogoro ambako ndio kituo cha mwisho cha bus hilo la maning nice. Kilichotushangaza wengi ni bus hilo kuwa na wanaume 4 ambao wote wanajiita ni makondakta kunyang'nyana godoro na mwanafunzi wa shule. Nawasifu bodaboda waliingilia huo mgogoro kwa kuona wazi kuwa hiyo gharama haikuwa fair ila godoro lilishatupwa kwenye booth na booth kufungwa kwa hiyo haikuwezekana kupata godoro na bus likaondoka japo abiria waliokuwa ndani walipaza kelele kulaani kitendo hicho cha makondakta. Mwanafunzi alipohojiwa alibainisha kuwa alikata tiketi mapema sana tangu tarehe 8 Desemba na aliwapa taarifa kuwa ana begi moja na godoro, mkata tiketi akamshauri alete begi na godoro jana jioni tarehe 10 Desemba na hakuambiwa kuwa godoro atalipia kiasi gani hadi leo aliposhuka kwenye bus kibaha ndio akapewa hiyo "Suprize" ya kufunga mwaka. Mwanafunzi akaishia kulia na kufajiriwa na madereva wa bodaboda hadi ndugu yake alipofika kumpokea kama dk15 baadae.

Picha ya wanaume 4 wanamnyang'anya godoro mtoto wa shule imenisikitisha sana ila bahati mbaya mfukoni nilikuwa na elfu2 tu na hao makondakta kwa lugha waliyokuwa wanatumia nilishindwa kuwaomba wapokee elfu2 ili wampe huyo mtoto kagodoro kake. Na lugha waliyokuwa wanatumia ilikuwa sio ya kistaarabu na matusi ya nguoni. Kiukweli imeniuma sana kushuhudia unyama huu ulivyofanyika na napata wasiwasi kuwa mwenye kampuni anaweza kujua haya mambo ambayo yanaweza kuharibu sifa za kampuni ya wakati huu ambao ushindani ni muhimu na customer care ndio dira. Kama anayoelezea huyu mtoto ni sahihi basi nilitegemea mteja alipie mizigo inayotakiwa kulipia anapopakia mizigo na kupewa risiti halali ya malipo ya mizigo labda na luggage tag ambayo kopi yake inaambatanishwa kwenye tiketi ya abiria kwa ajili ya utambulisho. Kwa namna wanavyoendesha mambo walikuwa na uwezo wa kumdai mwanafunzi huyu hata laki1 kwa godoro la elfu50!! Hii ni kama blackmail kwa kweli. Labda hainihusu, ila bus moja linakuwaje na makondakta 4, wanalipwaje mishahara? Nadhani hii inasababisha "wajiongeze" jinsi ya kupata mshahara!!

Nini maoni yako kuhusu kitendo kilichofanywa na watumishi wa bus la kampuni hii kwa mtoto huyu? Huyu mwanafunzi angeweza kusaidiwa "customer watchdog" ipi kama ipo??
Nilichoweza kumsaidia mwanafunzi huyu ni kupiga picha ya ticket hii na kumpa elfu2 niliyokuwa nayo imsaidie kwenye ngwe ya safari iliyobakia kufika nyumbani kwao.
Lakini pia nadhani taarifa hii itawasaidia abiria wengine kujihadhari na kutumia usafiri wa kampuni hii ya MANING NICE kwani uthubutu wa matendo ya hao makondakta ni ushahidi kuwa management ya kampuni ni mbovu sana, haya ni mawazo yangu. Kama taarifa hii itawaokoa wahanga "watarajiwa" nitajisikia nimeutendea haki umma. Ila pia naomba mamlaka husika wafuatilie huduma za kampuni hii ili kupunguza adha wanazopata abiria. Lakini pia iwe taratibu kumtaarifu abiria gharama ya mizigo kabla ya safari ili abiria awe na uhuru wa maamuzi. Hapa hapa pia naomba mamlaka husika iweke rasmi muda wa buses kusimama kwa ajili ya kula. Hivi karibuni nilishuhudia abiria wa bus la Arusha wakipewa dk 10 kwa huduma ya chakula. Hadi mtu wa mwisho anashuka kutoka kwenye bus zilishaisha dk4, niliona kama haikuwa fair kwa huyu abiria wa mwisho aliyekuwa na watoto mapacha, daaah!! God bless Tanzania.
Screenshot_20211211-185208.jpg
 
Uko sahihi. Naambiwa hapa tiketi hadi stendi ya Magufuli wanachaji elfu26 ila kama utashuka kituo kinachofuata unalipishwa elfu40 ambayo kwao no nauli ya Morogoro. Muhimu haki za mtejwa zilindwe jamani, khaa!!
Washenzi hao
 
Huu utaratibu wa kulipisha mizigo ya abiria umeanza lini?! Yaani mimi. Ninachojua abiria ana mizigo yake ile ana beba free mfano kapanda na begi la nguo na kifurushi cha nyanya, nazi, mchele, mahindi au dumu la mafuta ya kupikia.

Sasa siku hizi wenye mabasi naona wameamua kutoza bei tena za kubuni na kwasababu hii tozo ni ya kiwizi wizi basi kunakuwa hakuna taarifa rasmi za kueleweka juu hizo gharama.

Inakera sana.
 
Hapohapo Kibaha kuna Ofisi za chama cha Kutetea Abiria CHAKUA
amuone mtu mmoja anaitwa Hassan Mchanjama, hilo Bus la Manning litashughlikiwa na Godoro mwenye Kampuni atalipia Traffic au Mahakamani
Pole yake huyo Mwanangu, kwel tunasomesha kwa shida halafu wale waliotoroka darasani wanakuja kulipiza kisasi tena wanaume wa4?
 
Yaani imebidi nije nicomment kabla sijamaliza kusoma, mimi ni muhanga wa huo upumbavu wao, tena hiyo gari ya moro to mtwara.
Hilo bus lina makondakta washenzi wa tabia, kuna siku niliwapigia simu kuwajulisha nitatoka mtwara to lindi, na nilikuwa na kigodoro kama hiko cha mwanafunzi, asee walikomaa niwalipe 15000 elfu sehemu ya km 100 tu.
Iliniuma sitasahau, ni washenzi hao viumbe wa hiyo kampuni sijapata kuona.
 
Yaani imebidi nije nicomment kabla sijamaliza kusoma, mimi ni muhanga wa huo upumbavu wao, tena hiyo gari ya moro to mtwara.
Hilo bus lina makondakta washenzi wa tabia, kuna siku niliwapigia simu kuwajulisha nitatoka mtwara to lindi, na nilikuwa na kigodoro kama hiko cha mwanafunzi, asee walikomaa niwalipe 15000 elfu sehemu ya km 100 tu.
Iliniuma sitasahau, ni washenzi hao viumbe wa hiyo kampuni sijapata kuona.
Duh kumbe ni tabia yao!!
Taasisi husika itetee wasafiri jamani
 
Duuuh sijui kwanini wamefanya upumbavu huo, ila Mining nice chama la wana bus langu la mchana Mtwara -Dar ilikuwa poa sana
 
Tatzo ni tozo gharama za maisha zimepanda mafuta pia yamepanda, Siri ni kua makondakta wa mabus huwa wanaweka mafuta kwenye gar wao wenyewe na kulipa posho ya dereva na turnboy Sasa ile hela ya mizigo ndo inafanya hyo kazi, na kesho gari inatakiwa igeuke muda mwngne makondakta wanajikuta Wana madeni makubwa huko kwenye filling station

Sasa ukikutana nae akiwa na hzo stress zake ndo hapo na yeye atataka akulipishe hela nyingi kweny mzigo unaochukua nafas kubwa, hii yote ni madhara ya gharama za maisha kupanda hii lazima itamuathiri kila mmoja mwenye kipato Cha kawaida hata mtoto anaezaliwa leo
 
Back
Top Bottom