Bus la Maning nice linanyanyasa abiria

Leo nimeshuhudia mtafaruku kati ya watumishi wa BUS LA MANING NICE na abiria wa kike ambaye ni mwanafunzi aliyesafiri kutokea Lindi kuja Kibaha. Ameshuka na makondakta wakamshushia begi na godoro la futi 3, wakamdai alipie godoro elfu30. Mwanafunzi akapigwa butwaa kwani anadai godoro huwa analipia elfu3. Basi akaambiwa alipie elfu10, yeye akawa na elfu5. Kilichofuatia ni purukushani ya kumnyang'anya godoro huyo msichana na kuondoka nalo kuelekea morogoro ambako ndio kituo cha mwisho cha bus hilo la maning nice. Kilichotushangaza wengi ni bus hilo kuwa na wanaume 4 ambao wote wanajiita ni makondakta kunyang'nyana godoro na mwanafunzi wa shule. Nawasifu bodaboda waliingilia huo mgogoro kwa kuona wazi kuwa hiyo gharama haikuwa fair ila godoro lilishatupwa kwenye booth na booth kufungwa kwa hiyo haikuwezekana kupata godoro na bus likaondoka japo abiria waliokuwa ndani walipaza kelele kulaani kitendo hicho cha makondakta. Mwanafunzi alipohojiwa alibainisha kuwa alikata tiketi mapema sana tangu tarehe 8 Desemba na aliwapa taarifa kuwa ana begi moja na godoro, mkata tiketi akamshauri alete begi na godoro jana jioni tarehe 10 Desemba na hakuambiwa kuwa godoro atalipia kiasi gani hadi leo aliposhuka kwenye bus kibaha ndio akapewa hiyo "Suprize" ya kufunga mwaka. Mwanafunzi akaishia kulia na kufajiriwa na madereva wa bodaboda hadi ndugu yake alipofika kumpokea kama dk15 baadae.

Picha ya wanaume 4 wanamnyang'anya godoro mtoto wa shule imenisikitisha sana ila bahati mbaya mfukoni nilikuwa na elfu2 tu na hao makondakta kwa lugha waliyokuwa wanatumia nilishindwa kuwaomba wapokee elfu2 ili wampe huyo mtoto kagodoro kake. Na lugha waliyokuwa wanatumia ilikuwa sio ya kistaarabu na matusi ya nguoni. Kiukweli imeniuma sana kushuhudia unyama huu ulivyofanyika na napata wasiwasi kuwa mwenye kampuni anaweza kujua haya mambo ambayo yanaweza kuharibu sifa za kampuni ya wakati huu ambao ushindani ni muhimu na customer care ndio dira. Kama anayoelezea huyu mtoto ni sahihi basi nilitegemea mteja alipie mizigo inayotakiwa kulipia anapopakia mizigo na kupewa risiti halali ya malipo ya mizigo labda na luggage tag ambayo kopi yake inaambatanishwa kwenye tiketi ya abiria kwa ajili ya utambulisho. Kwa namna wanavyoendesha mambo walikuwa na uwezo wa kumdai mwanafunzi huyu hata laki1 kwa godoro la elfu50!! Hii ni kama blackmail kwa kweli. Labda hainihusu, ila bus moja linakuwaje na makondakta 4, wanalipwaje mishahara? Nadhani hii inasababisha "wajiongeze" jinsi ya kupata mshahara!!

Nini maoni yako kuhusu kitendo kilichofanywa na watumishi wa bus la kampuni hii kwa mtoto huyu? Huyu mwanafunzi angeweza kusaidiwa "customer watchdog" ipi kama ipo??
Nilichoweza kumsaidia mwanafunzi huyu ni kupiga picha ya ticket hii na kumpa elfu2 niliyokuwa nayo imsaidie kwenye ngwe ya safari iliyobakia kufika nyumbani kwao.
Lakini pia nadhani taarifa hii itawasaidia abiria wengine kujihadhari na kutumia usafiri wa kampuni hii ya MANING NICE kwani uthubutu wa matendo ya hao makondakta ni ushahidi kuwa management ya kampuni ni mbovu sana, haya ni mawazo yangu. Kama taarifa hii itawaokoa wahanga "watarajiwa" nitajisikia nimeutendea haki umma. Ila pia naomba mamlaka husika wafuatilie huduma za kampuni hii ili kupunguza adha wanazopata abiria. Lakini pia iwe taratibu kumtaarifu abiria gharama ya mizigo kabla ya safari ili abiria awe na uhuru wa maamuzi. Hapa hapa pia naomba mamlaka husika iweke rasmi muda wa buses kusimama kwa ajili ya kula. Hivi karibuni nilishuhudia abiria wa bus la Arusha wakipewa dk 10 kwa huduma ya chakula. Hadi mtu wa mwisho anashuka kutoka kwenye bus zilishaisha dk4, niliona kama haikuwa fair kwa huyu abiria wa mwisho aliyekuwa na watoto mapacha, daaah!! God bless Tanzania.View attachment 2040736
reporting time saa saba ya usiku.
 
Biashara huria ndio madhara yake shetani amewatangulia.Sehemu Ambazo zinagusa jamii ya Hali ya chini Serikali iweke mikono yake mfano: Shule zinafungwa watoto kurudi makwao wasafirishwe na Serikali kama ilivyokuwa zamani Hata kama wazazi wanachangia usafiri lakini nauli ilipwe shuleni,shule itafute bus,mabinti wanateseka stendi
 
Miaka yote wakati wa likizo nauli hupanda mara dufu, couz wanajua wanafunzi wengi wanasafiri, aaaaah.

Makondakta wote sio wa bus au daladala n hovyo, sitasahau nilivyotukanwa matusi kisa naul 400, hapo nlkua nimeibiwa km 70k bila kujua, wakat huo nipo advance, namshukuru yule kaka alinisaidia kunilipia, nataman sana nikutane nae nimrudishie fadhira zake.
 
Mimi kama mpita njia nilijaribu kupiga picha tiketi ya huyo mwanafunzi na kuituma kwa trafiki kibaha na pia kutoa taarifa kwa afisa wa LATRA Morogoro 0738 000 054

Sent from my SM-N920S using JamiiForums mobile app
Kama unazo namba za huyo mwanafunzi naomba nipatie niwasiliane nae, nataka niangalie namna yakumnunulia godoro lingine.

Kama abiria mliokuwepo kwenye hilo basi sijaelewa mlishindwaje kumsaidia huyo mwanafunzi mpaka bus likaondoka na gorodoro ni aibu kwenu, ila nikupogeze kufanya hicho ulichoweza kufanya.
 
Nimejikuta nimepata hasira sana.
Navyojijua ningekua kwenye hilo bus kama abiria lazima huyo mwanafunzi angekabidhwa hilo godoro lake vizuri tu either kwa kumlipia au kwa njia nyingine yoyote ambayo ningeona inafaa kwa wakati huo.
 
Nimejikuta nimepata hasira sana.
Navyojijua ningekua kwenye hilo bus kama abiria lazima huyo mwanafunzi angekabidhwa hilo godoro lake vizuri tu either kwa kumlipia au kwa njia nyingine yoyote ambayo ningeona inafaa kwa wakati huo.
Inaumiza sana mwanafunzi ameachwa apambane mwenyewe wakati bus lina abiria wamekaa
 
Bei ya elfu kumi kwa ilo godoro ni sahihi labda tu uyu mwanafunzi akuambiwa bei mapema.
jamani godoro la mwanafunzi la futi 3 inch 3
hawa Manning ni washamba sana kwenye root za Dar - Arusha au Dar - Dodoma hawawezi toa tiketi ya kishamba namna hiyo
Haina namba ya Bus /namba ya usajiri wa Gari
kwa hiyo itasumbua ufuatiliaji labda huyu Binti awahi madai yake
LATRA iingilie kati kwa wanafunzi kuhusu mizigo km sanduku hata liwe la chuma na godoro visilipiwe (Kisheria ni nusu nauli sema hakuna sehemu km hiyo siku hizi kwa wanafunzi)
betina tupe mrejesho kuna mafaniko kweli?
1639486959630.png
 
Back
Top Bottom