Tatizo chaguzi nyingi hapa Afrika ni zinafanyika kiwiziwizi,Kitendo cha kukiuka makubaliano ya amani na katiba ya nchi kwa kuingia ktk duru ya 3 ni dhahiri amedhamiria kuongoza tena,uchaguzi ni kama kizugio tu kwa Warundi.
Huu utoto sana jamani issue ya nchi nyingine watu mnaakomaa kupeana makundi kupitia matukio yasiyowahusu, haya sasa nani ana ushahidi kua Ukawa wanahusika na hii issue? Utoto tu
Raia wamlaki rais Ngozi

wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza
Mashahidi wameiambia BBC kwamba rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
Nkurunziza arudi nyumbani kwake Ngozi

Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
Majenerali waasi kushtakiwa

Burundi
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..
Majenerali waasi wakamatwa:

Maandamano yaliokuwa yakiendelea nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
[h=1]Tag Archives: Gen Godefroid Niyombare[/h] May 15 2015
[h=1]Burundi coup leaders arrested[/h] Three army generals who were part of a group
that attempted to overthrow Burundi President
Pierre Nkurunziza a few days ago have been
arrested. Coup Ring Leader Gen Godefroid
Niyombare
Former Burundi Defence minister Gen
Cyrille Ndayirukiye was one of the three arrested
today. But the general who led the coup and made
the announcement on radio, Gen Godefroid
Niyombare (pictured left) has not been found.
The General had earlier told AFP News Agency on
phone yesterday that he and others who plotted
the coup will surrender but hoped they will not be
killed.I hope they wont kill us. He said.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.