Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,347
- 10,227
Leo nipo safarini basi nililopanda limefanya nifungue huu uzi. Kiukweli inafikia mahali safari inakua mbaya kutokana na hizi burudani zinazotolewa kwenye mabasi.
Yani miziki inayopigwa haina mahadhi ya kuchezwa kwenye public transport kama hizi, nimeshangaa sana nyimbo kama ya Whozu - Sina Shida Ndogondogo kuchezwa kwenye basi wakati ni nyimbo za bata.
Nyingine nyingi ni matusi tu mara "nina bonge la ndonga" "nina kipururu" yani kila nyimbo inahamasisha ngono tu. Kiukweli hii sio burudani tunayoihitaji sisi kama wasafiri tukiwa na mama, baba na wadogo zetu.
Huwa nasikiliza hizi nyimbo zenye matusi sana tu ila nikiwa eneo linalofaa kucheza nyimbo hizo. Hii mada ni pana sana wamiliki na waendesha usafiri wa umma wanapaswa kujua haya mabasi tunapanda watu rika tofauti.
Hata hawa wazee wanazisikiliza hizi zenye matusi sana ila ni maeneo husika na sio nyimbo za chumbani kuzileta kwenye mabasi, wapo wasanii wengi sana wanaimba bongo flava ila wanajali maadili na nyimbo zao unapiga popote; Alikiba, Ben Pol, Bright, Barnaba, Lady JayDee, wapo wengi tu na hata hao waimba matusi kuna nyimbo wanaimba vitu vya maana na zinafaa kucheza popote.
Wengi kila saa utasikia muhogo mara kitumbua mara papa, "huko wasafi mara inama nilenge rungu kwa mredi kipepe" nyingi mahadhi yake ni chumbani na hata kwenye TV zinapaswa kuchezwa usiku.
Naishia hapa ila bongo flava kiukweli ina hali mbaya yani kila msanii ni mapenzi na lazima aihusishe ngono ndani yake.