Wazazi/Walezi mnatumia njia gani kumdhibiti Mtoto asiimbe nyimbo zenye mashairi ya kuhamasisha ngono/matusi hasa za wasanii wa Tanzania?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
NALIA NGWENA na ubishi wangu huu nimepiga sana vibao lakini kila nyimbo mpya bwana mdogo wangu anapita nazo /anazihifadhi akilini. Ni mtoto wa miaka minne nimekuwa nikishangazwa sana namna gani akihifadhi nyimbo kichwani mbaya zaidi huwa napata aibu ninapokua na wageni unakuta anaimba mashairi ya hamasa za ngono/matusi.

Kuna nyimbo moja nafikiri ni ubeti wa Mboso Khan Kuna kakipande anasema "Mjusi kafiri asafishe mtaro" mwanangu huo ubeti alikuwa anaimba wote. Na Kuna nyimbo nyingine nafikiri ni ya Harmonize Kuna ubeti anaimba "inama nipache Rungu". Yote Tisa kumi nyimbo ya umeyatimba ushairi wa Mboso anaweza akaimba asubuhi mpaka jioni hata hajali wala nini tena mbele ya wageni.

Nilipiga vibao lakini niliona vibao siyo suluhisho maana kuna muda huwa ananiambia "baba mbona kwenye TV huwa wanaimba"!? Husema kuwa namuonea. Kiukweli nyimbo za wasanii wetu wanatumia maneno machafu sana/matusi mpaka wewe MTU mzima hata kusikia mbele ya wakubwa wako unaona aibu.

Wakuu nyinyi mnatumia njia gani kumdhibiti mtoto wako asiimbe nyimbo zenye maudhui ya matusi/maneno machafu? Nasoma comments.
 
Pole. Hiyo TV na hizo channel za Bongo music huwa anaweka mwenyewe? Kama sio yeye huwezi kumlaumu.

Kama wazazi ndio nyimbo mnazopenda kusikiliza kwenye TV mkiwa na mtoto pembeni mnafeli pakubwa.

Mtoto wa miaka minne alipaswa kuangalia TV kwa uangalizi wa mzazi. Kuna vipindi vinavyoendana na umri wake.

Malezi ni kazi kama kazi nyingine.
 
NACHUKUA HII MKUU.
 
Kuna familia ya jirani yangu ni waislamu wale swala Tano baba ni Ostadh mama ni Ostadhat madogo wanaenda na kurudishwa na gari wako wa3 miaka 2, mi4, na 7, TV nyumbn ni katuni na mawaidha tu, juzi kati kukawa na birthday ya mtoto wa jirani wakaitwa watoto wote wa mtaani humo ndani zikawa zinapigwa nyimbo za akina mboso, Zuchu, jux kilichomshangaza Ostadh ni jinsi wanaye walivyokuwa wanaitikia mstari baada ya mstari mpaka akaamua kuwachomoa kwenye birthday na kuwafungia ndani😂😂😂
 
Mi nimezaliwa kwenye familia yenye msimamo mkali kwanzia unazaliwa hadi unaondoka nyumbani hutasikia radio au TV inapiga mziki.

Kwahiyo imekua ni kama kosa la jinai kusikiliza mziki hata baada ya kuondoka nyumbani huwa siwezi kukaa sehem inayopigwa mziki labda niwe kwnye Bus nasafiri.

Labda utumie mbinu ya kibandidu kama hiyo laa sivyo lazima wakariri hadi rege
 
Kuna familia ya jirani yangu ni waislamu wale swala Tano baba ni Ostadh mama ni Ostadhat madogo wanaenda na kurudishwa na gari wako wa3 miaka 2, mi4,na 7, TV nyumbn ni katuni na mawaidha tu, juzi kati kukawa na birthday ya mtoto wa jirani wakaitwa watoto wote wa mtaani humo ndani zikawa zinapigwa nyimbo za akina mboso, Zuchu, jux kilichomshangaza Ostadh ni jinsi wanaye walivyokuwa wanaitikia mstari baada ya mstari mpaka akaamua kuwachomoa kwenye birthday na kuwafungia ndani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom