Burudani kwenye mabasi zitolewe tu

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,339
10,185
Leo nipo safarini basi nililopanda limefanya nifungue huu uzi. Kiukweli inafikia mahali safari inakua mbaya kutokana na hizi burudani zinazotolewa kwenye mabasi.

Yani miziki inayopigwa haina mahadhi ya kuchezwa kwenye public transport kama hizi, nimeshangaa sana nyimbo kama ya Whozu - Sina Shida Ndogondogo kuchezwa kwenye basi wakati ni nyimbo za bata.

Nyingine nyingi ni matusi tu mara "nina bonge la ndonga" "nina kipururu" yani kila nyimbo inahamasisha ngono tu. Kiukweli hii sio burudani tunayoihitaji sisi kama wasafiri tukiwa na mama, baba na wadogo zetu.

Huwa nasikiliza hizi nyimbo zenye matusi sana tu ila nikiwa eneo linalofaa kucheza nyimbo hizo. Hii mada ni pana sana wamiliki na waendesha usafiri wa umma wanapaswa kujua haya mabasi tunapanda watu rika tofauti.

Hata hawa wazee wanazisikiliza hizi zenye matusi sana ila ni maeneo husika na sio nyimbo za chumbani kuzileta kwenye mabasi, wapo wasanii wengi sana wanaimba bongo flava ila wanajali maadili na nyimbo zao unapiga popote; Alikiba, Ben Pol, Bright, Barnaba, Lady JayDee, wapo wengi tu na hata hao waimba matusi kuna nyimbo wanaimba vitu vya maana na zinafaa kucheza popote.

Wengi kila saa utasikia muhogo mara kitumbua mara papa, "huko wasafi mara inama nilenge rungu kwa mredi kipepe" nyingi mahadhi yake ni chumbani na hata kwenye TV zinapaswa kuchezwa usiku.

Naishia hapa ila bongo flava kiukweli ina hali mbaya yani kila msanii ni mapenzi na lazima aihusishe ngono ndani yake.
 
Ungetoa na list ya nyimbo zakupigwa hapa
Ikiwa nyimbo za sikuhizi zote matusi
Unataka waweke gospel na qaswida ili mkereke zaidi?!
Hakuna haja ya kuweka list hapa, vitu viko wazi. Haya ni maoni yangu kama ww una-support pia uko sahihi, nadhani solution ya kero zote za usafiri wa umma ni kuwa na usafiri binafsi. Acha tupambane ipo siku sitapanda tena basi.
 
Hizi nyimbo kwa kweli zimekuwa nyingi..

Yaani hata Tv stations zinapiga mchana kweupe

Zikipigwa ukiwa mbele ya mtu unayeheshimiana naye lazima aibu ikupate

Mifano;

✓Kata ya Ommy dimpoz na Nandy

✓Gusanisha ya Gnako

✓Come again ya Lulu diva

Yaani kiufupi nyimbo zimekuwa ni soft porn sasa

Tcra waweke katazo ya nyimbo zenye haya maupuuzi kupigwa in daytime..

Wasimamizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara nao vilevile waweke miongozo
 
Kosa sio la watu wa mabasi, kosa ni la serikali. Hasa wakati huu wa korona LATRA, Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya Habari walipaswa kuandaa vipindi kuhusu kujikinga na covid-19 na iwe sheria lazima kila bus kuwa na copy ya hiyo video ili kutoa elimu kwa wasafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunanawishwa tu mikono mkuu, kiukweli wazo lako zuri elimu inapaswa kutolewa kila mahali watu wawe aware, watu wananawa mikono lakini bado sio salama. Wengi wanajua akishanawa ndio basi, anashika tena sehemu hatarishi na bila kunawa tena anagusa pua, mdomo au macho. Mungu atusaidie katika hili janga.
 
Hizi nyimbo kwa kweli zimekuwa nyingi..

Yaani hata Tv stations zinapiga mchana kweupe

Zikipigwa ukiwa mbele ya mtu unayeheshimiana naye lazima aibu ikupate

Mifano;

✓Kata ya Ommy dimpoz na Nandy

✓Gusanisha ya Gnako

✓Come again ya Lulu diva

Yaani kiufupi nyimbo zimekuwa ni soft porn sasa

Tcra waweke katazo ya nyimbo zenye haya maupuuzi kupigwa in daytime..

Wasimamizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara nao vilevile waweke miongozo
Acha tu mkuu kwenye mabasi tunaangalia porn kabisa bora hata wapige tu audio maana video nyingine ni hatari.

Kupunguza aibu unafumba tu macho kama umelala vile. 😂
 
Haya mambo huwa yanakera zaidi kipindi cha watoto kurudi shule unakuta mwanaume yuko na binti yake anampeleka shule konda anaweka madudu, sijui chura, movie za mapenzi n.k inabidi katoto kainame kajifanye hakaoni, mzazi anajifanya anaangalia mazingira ya nje kumbe aibu.
 
Hili ni tatizo la kimaadili mkuu. Hapo ndipo tulipofikia jamii yetu, sio kwenye usafiri tu bali kila mahali iwe ni mtaani, migahawani na mahoteli yaani kila mahali ni huo upuuzi. Huu mziki wa kizazi kipya sio mziki tena bali ni uhamasishaji wa ngono. Kweli kizazi hiki ni kizazi kilichopotoka watu wanawaza ngono tu kila mahali. Mungu atunusuru ndio maana hata tunapatwa na majanga ya namna ya ajabu ukifuatilia kwa makini ni hasira za Mungu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naishia hapa ila bongo flava kiukweli ina hali mbaya yani kila msanii ni mapenzi na lazima aihusishe ngono ndani yake.

Hapa nimepaelewa zaidi
 
Unachosema ni cha kweli kabisa. Unaweza kuziona hizo nyimbo ni za kawaida ukiwa unaziskiza kwako lakini ukiwa pamoja na watu wazima mahali alafu ikapigwa, yani unahisi unakosa pumzi kabisa ... unahisi aibu kana kwamba uliuimba wewe.

Kwakweli siku nilipopanda basi na kuketi na wamama watu wazima kabisa kisha ikapigwa nyimbo ya WOWOWO kwenye TV, hapo ndo nilijua ule wimbo una 'effect' gani. Nilikosa pa kuweka sura!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kuna mwaka konda alishaweka X nadhani zililuwa ni bus za Dar to mbeya.
Alafu mbona baadhi ya ma dj wa kenya huwa wanazi fanyia utundu yunaona kule kinako faa kuangalia mfano Dj joe mfalme wa maisha magic na faru hawa wa kwetu wanashindwaga nn au wakishajua piga baby scrach wanaana jiita ma Dj
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom