msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 862
- 1,249
Ndugu Godbless Lema kwa muda sasa amekuwa ni "specialist"wa kuwatabiria vifo viongozi wa Serikali na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi. Kibaya zaidi Vifo vikitokea Machema wanajifungia sehemu na "kuchoma" nyama.
Wakati wa Kifo cha Hayati John Pombe Magufuli walifanya hivyo, wakati wa kifo cha Mzee Job Ndugai, Spika Mstaafu wa Bunge walifanya hivyo, huu ni kama ndio utamaduni wao wa kila siku.
Wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa kila siku wakimtangazia kifo mpaka Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan utadhani wenyewe wataishi milele.
Huwezi kusikia Chadema kama Chama angalau wametuma salamu za pole kwenye misiba ya viongozi wa Serikali, hawana kabisa ustaarabu huo.
Mh Rais Dkt. Samia tayari kashatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania wa Kwanza, Mzee Edwin Mtei ambaye pia ndiye Kiongozi mwanzilishi wa Chadema.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wa JMT nyakati zile, alilazimika kusafiri mpaka Jijini Nairobi kwenda kumsalimia Mh Tundu Lissu alipokuwa hospitali.
Mh Rais huyu huyu(Mama Samia) alikwenda kumtembelea Mama yake Mh. Halima Mdee akiwa hospitalini. Sio Mwenyekiti Tundu Lissu, sio KM John Mnyika, sio Makamu Mwenyekiti John Heche waliwahi kufika kwa Mama Halima Mdee kumjulia khali mpaka umauti unamfika.
Tuna Chama cha Siasa cha ajabu sana Nchi hii.Tuna viongozi wa AJABU SANA ndani ya Chadema hii ya Tundu Lissu. Angalau Mzee Freeman Mbowe ungeweza kumuona kwenye misiba ya Viongozi wa Kitaifa lakini sio Chadema hii ya Tundu Lissu na John Heche.
Nadhani kuna kitu washauri wa Chadema wakina Padre Kitima, Askofu Bagonza, Askofu Mwamakula wanapaswa kuwafundisha utamaduni huu Viongozi wa Chadema Taifa na wafuasi wao.
Biblia inasema(Mwanzo 3:19)
"Tulitoka kwa udongo tutarudi kwa udongo"
Kifo uhai always havinaga mwenyewe.
Kwakheri Mzee Edwin Mtei, Umevipigana vita vyema na imani ukailinda.