Buriani Mhe. Komba wa 'Joka la kufugwa'

Buriani Mhe. Komba wa 'Joka la kufugwa'

Nyakarungu

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Posts
472
Reaction score
377
BURIANI MH. KOMBA WA JOKA LA KUFUGWA .

Mwaka mmoja kabla ya mimi kuzaliwa 1979, kuna tukio kubwa sana lilitokea katika nchi yetu chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya kwanza ‘Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Wakati huo aliyekuwa Rais wa nchi ya Uganda General Idd Amin Dadaa aliichokoza nchi yetu, pamoja na uchokozi huo aliokuwa ameuanza muda mrefu sana lakini Rais wetu alivumilia sana mpaka ilipolazimu Rais wetu kutangaza vita iliyopelekea mapambano kati ya majeshi ya nchi ya Uganda na Tanzania, hata hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani katika vita ile Idd Amin alipigwa na nchi yetu kuchukua ushindi.

Vijana wetu wa Tanzania walipigana kiume na kwa ari ya kuhakikisha wanatimiza adhima ya kuilinda nchi yetu dhidi ya uvamizi wa Idd Amin,

Nyuma ya ari na moto waliokuwa nao vijana wetu wanajeshi, kulikuwa na uadilifu na uzalendo mkubwa sana uliopikika ndani ya mioyo yao, hali hii ilichagizwa pia na hamasa walizopewa jeshini wakati wa maandalizi ya kwenda vitani (katika nchi zote au katika makundi yote wanapojiandaa na vita, huwepo hali ya kutumia sanaa na namna ya sanaa yoyote ile kuwapa ari na moto wanajeshi kabla ya kwenda vitani)

Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka 11 nikiwa nyumbani kwetu nikilelewa na wazazi wangu, wakati Baba akiwa kiongozi wa kata akitumikia umma kama katibu wa kata, alikuwa akisafiri kwenda umbali wa km 5 katika ofsi yake kwa kutumia baiskeli aina ya phonex, mara zote alichelewa kurudi nyumbani na alifika mida ya saa 2-3 usiku akiwa amechoka na safari hiyo,

Lakini tukiwa familia yenye watoto kadhaa, tulimngoja baba mpaka afike nyumbani usiku ule hivyo mara zote tulikusanyika kwenye nyumba iliyokuwa ikitumika kama jiko tukingojea chakula kipikwe huku tukingojea kusikia sauti ya mbwa wakibweka tukotke nje kumpokea baba kwani tuliamini yeye anapofika mbwa watabweka lakini watatoa sauti za kuashiria furaha ya mtu mtu wanaemfahamu.

Wakati wote huo tukiwa ndani ya jiko mama akipika au akichochea moto jikoni, dada yangu mkubwa Grace na kaka yangu mkubwa Zachayo walikuwa wataalamu wa kunogesha hadithi za shuleni kwao au habari za hapa na pale.

Nakumbuka siku moja nikiwa nimesimama ndani ya jiko nikitazama kwa makini ukali wa moto uliokuwa ukipika mahindi na viazi vitamu huku nikiwa nimeshikiria nguzo iliyokuwa imeshikiria ile nyumba yetu ya nyasi (ambero) kuna wimbo ulisikika ukiimbwa na Marehemu komba radioni wakati huo tulikuwa na radio aina ya mkulima na tulizoea kusikiliza mchezo wa radio ulioitwa chibuku "jangara" ule wimbo uliposikika dada akamuuliza mama, je huyu anaeimba ndiye alikuwa akiimba kipindi kile mjomba Ramadhani a.k.a anko mandevu a.k.a Osama alikuwa anaenda vitani? Mama alijibu ndio, huyu ni mwimbaji wa hizo nyimbo za vita anaitwa komba mtu wa jeshini ni mwanajeshi kabisa na alienda vitani,

Mjomba wetu alipigana ile vita akiwa mstari wa mbele, wakati wa maandalizi ya vita familia ilitega sikio kila mara radioni kwa sababu ya kutaka kujua kinachoendelea ikizingatiwa ndugu yetu alikuwa miongoni mwa wanavita wale,

Hivyo nyimbo zilizotumika kuhamasisha watanzania wajiamini na kulipa jeshi mori na ari zilikuwa zikipigwa kila wakati hivyo baadhi ya watu waliweza kuzikariri,

Siku hiyo Kaka, Dada na Mama waliozisikia nyimbo zilizotungwa na kuimbwa na marehemu komba walianza kuimba kipande huku wakieleza walivyokuwa na wasiwasi juu ya mjomba wetu ambae hata hivyo alirejea akiwa mzima.

Chorus ile ilinivutia ukizingatia nilikuwa na kipaji cha kuimba na kukariri kwa haraka na ndio siku nilipojua jina la mwanajeshi aliyeimba wimbo uliotumika kuwatia moyo wananchi na kuwapa ujasiri na mori wanajeshi.

WALIIMBA….
Tanzania kumezuka…..
Na joka kubwa la kufugwa ni lazima tuliponde life…
Idd Amin Dadaa ni joka kubwa la kufugwa ni lazima tuliponde life….

KOMBA WA JOKA LA KUFUGWA AMETANGULIA, MWIMBAJI NA MTUNZI MAHIRI

Kwa bahati moja au nyingine Baba alirejea na tukatoka kumpokea na hiyo ikiwa mwisho wa stori ile mpaka nilipokuwa mkubwa kiitikio hiki kimekuwa kikiimba kichwani.

Lakini jana baada ya kupata habari za kifo chake nilimpigia mama simu na kumpa taarifa hiyo iliyomsikitisha na kwa bahati nzuri wimbo huo ameniambia anaukmbuka wote, naahidi kuupata.
Je tuna nini cha kujivunia kwa shujaa komba kama sio kukumbuka kazi kubwa aloifanya kwa taifa wakati muhimu kama ule wa vita?

Nawaombea wanafamilia wote Mungu awape nguvu tunawaombea.
 
Japo majoka bado yapo mengine yana makengeza hapa kwetu tanzania,tunahitaji viongozi watakawaowasema live na kuwaondoa hayo majoka..Buriana Capt. Komba
 
Katika vitu muhimu tunavyotakiwa kujifunza ni kutotumia matukio yanayoumiza familia kutafuta lift ya kusikika kisiaisa
 
Ni kweli capt Komba alistahili kupewa sifa kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati huo. Lakini lazima tukumbuke kuwa mazuri mengi sana zaidi ya million utakayofanya, yanaweza kuondolewa na jambo moja baya utakalolifanya. Hata maandiko yanasema hivyo, fanyeni mema siku zote, ukikosea jambo, isifike machweo ya jua kabla hujatubu, kwa maana hilo moja ulilokosa litakuhariabia yote mema uliyofanya maishani mwako. Capt. Komba baada ya kupata sifa zote hizo aligeuka kuwa mtu asiyestahili kitu, alikuwa ni mtu ambaye hafai kwa jinsi alivoyotumia mdomo wake vibaya na sijui kama alikumbuka kutubu kabla hajafa. Aliwachulia vifo wazee wenye hekima na watumishi wenye utumishi uliotukuka kwenye taifa hili. Lakini mwenyezi Mungu mwenye rehema amemuliza Komba, je nani alikuambia kuwa wewe utaishi milele, leo nachukua roho yako. Hakuna gharama yeyote utakayotoa ukiwaheshimu na kuwasemea mema wanadamu wenzio. Komba amekwenda na iwe fundisho kwetu.
 
Kati ya vijana ninaowaheshimu sana linapokuja suala la taifa huwa anakuwa mtaifa na kuacha uvyama ni huyu nyakarungu, sina la kusema, R.I.P KOMBA
 
Kifo cha Komba kimeshangiliwa kila kona ya nchi hii..

Ushabiki wa kisiasa usikupeleke kwenye kukufuru.Kila nafsi iliyozaliwa itaonja umauti hakuna atakaepaa.Capt John Komba alikuwa mwanasiasa wa kawaida ndani ya CCM akiwatumikia vyema wananchi wa jimbo la Mbinga Magharibi katika siasa za kawaida za kidemokrasia sasa kinachofanya wewe na majuha wenzako mushangilie nini?
 
Kati ya vijana ninaowaheshimu sana linapokuja suala la taifa huwa anakuwa mtaifa na kuacha uvyama ni huyu nyakarungu, sina la kusema, R.I.P KOMBA

Nyakarungu yule aliyetajwa kwenye Ripoti ya siri ya Zitto au Mwingine maana hiyo User sio Verified.
 
Ni kweli capt Komba alistahili kupewa sifa kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati huo. Lakini lazima tukumbuke kuwa mazuri mengi sana zaidi ya million utakayofanya, yanaweza kuondolewa na jambo moja baya utakalolifanya. Hata maandiko yanasema hivyo, fanyeni mema siku zote, ukikosea jambo, isifike machweo ya jua kabla hujatubu, kwa maana hilo moja ulilokosa litakuhariabia yote mema uliyofanya maishani mwako. Capt. Komba baada ya kupata sifa zote hizo aligeuka kuwa mtu asiyestahili kitu, alikuwa ni mtu ambaye hafai kwa jinsi alivoyotumia mdomo wake vibaya na sijui kama alikumbuka kutubu kabla hajafa. Aliwachulia vifo wazee wenye hekima na watumishi wenye utumishi uliotukuka kwenye taifa hili. Lakini mwenyezi Mungu mwenye rehema amemuliza Komba, je nani alikuambia kuwa wewe utaishi milele, leo nachukua roho yako. Hakuna gharama yeyote utakayotoa ukiwaheshimu na kuwasemea mema wanadamu wenzio. Komba amekwenda na iwe fundisho kwetu.

Kwa kuongezea tu yule Komba wa enzi za Mwl Nyerere sio Komba ambaye alikuwa hivi sasa kabla ya mauti kumpata,aligeuka na kuwa kibaraka wa mafisadi,hata utu wake aliuweka rehani,akaishiwa hata hekima na kubaki kama mwendawazimu,kinywa chake kilijaa uchafu na dharau kwa wananchi wa nchii hii,nadhani fedha zilimpofua macho,unaweza kufanya mazuri lukuki lakini jambo moja tu baya likakuondolea sifa zote,Komba atakumbukwa na mafisadi wa CCM na sio wananchi wote,alitutakia mabaya tulipodai serikali tatu,akadai ataingia msituni kabla ya kupata hizo serikali tatu,na kujiapiza maneno mambo mengi ungedhani yeye ndie Mungu.Kifo cha Komba na kiwe fundisho kwetu sisi wanaadamu,yatupasa tuwe wanyenyekevu wakati wote hata tukipata madaraka,pia yatupasa kuchunga vinywa na ndimi zetu,neno likitoka halirudi,na neno baya au lenye shari kamwe halisahauliki,maneno ya marehemu aliyokuwa anayatoa mle bungeni yalikuwa chukizo kwa watu wengi huku yakifurahiwa na wachache walioshiba.Tusijisahau sana kama hao wengine waliobaki wanaodai eti milioni 10 ni hela ya mboga,wengine eti nyoka wa makengeza,wengine wanaodai sisi ni wauza juisi tu.Dharau na jeuri ya pesa haileti heshima bali ni sifa za kijinga,na mwisho wake huwa mbaya na kuwa chukizo.
 
BURIANI MH. KOMBA WA JOKA LA KUFUGWA .

Mwaka mmoja kabla ya mimi kuzaliwa 1979, kuna tukio kubwa sana lilitokea katika nchi yetu chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya kwanza ‘Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Wakati huo aliyekuwa Rais wa nchi ya Uganda General Idd Amin Dadaa aliichokoza nchi yetu, pamoja na uchokozi huo aliokuwa ameuanza muda mrefu sana lakini Rais wetu alivumilia sana mpaka ilipolazimu Rais wetu kutangaza vita iliyopelekea mapambano kati ya majeshi ya nchi ya Uganda na Tanzania, hata hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani katika vita ile Idd Amin alipigwa na nchi yetu kuchukua ushindi.

Vijana wetu wa Tanzania walipigana kiume na kwa ari ya kuhakikisha wanatimiza adhima ya kuilinda nchi yetu dhidi ya uvamizi wa Idd Amin,

Nyuma ya ari na moto waliokuwa nao vijana wetu wanajeshi, kulikuwa na uadilifu na uzalendo mkubwa sana uliopikika ndani ya mioyo yao, hali hii ilichagizwa pia na hamasa walizopewa jeshini wakati wa maandalizi ya kwenda vitani (katika nchi zote au katika makundi yote wanapojiandaa na vita, huwepo hali ya kutumia sanaa na namna ya sanaa yoyote ile kuwapa ari na moto wanajeshi kabla ya kwenda vitani)

Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka 11 nikiwa nyumbani kwetu nikilelewa na wazazi wangu, wakati Baba akiwa kiongozi wa kata akitumikia umma kama katibu wa kata, alikuwa akisafiri kwenda umbali wa km 5 katika ofsi yake kwa kutumia baiskeli aina ya phonex, mara zote alichelewa kurudi nyumbani na alifika mida ya saa 2-3 usiku akiwa amechoka na safari hiyo,

Lakini tukiwa familia yenye watoto kadhaa, tulimngoja baba mpaka afike nyumbani usiku ule hivyo mara zote tulikusanyika kwenye nyumba iliyokuwa ikitumika kama jiko tukingojea chakula kipikwe huku tukingojea kusikia sauti ya mbwa wakibweka tukotke nje kumpokea baba kwani tuliamini yeye anapofika mbwa watabweka lakini watatoa sauti za kuashiria furaha ya mtu mtu wanaemfahamu.

Wakati wote huo tukiwa ndani ya jiko mama akipika au akichochea moto jikoni, dada yangu mkubwa Grace na kaka yangu mkubwa Zachayo walikuwa wataalamu wa kunogesha hadithi za shuleni kwao au habari za hapa na pale.

Nakumbuka siku moja nikiwa nimesimama ndani ya jiko nikitazama kwa makini ukali wa moto uliokuwa ukipika mahindi na viazi vitamu huku nikiwa nimeshikiria nguzo iliyokuwa imeshikiria ile nyumba yetu ya nyasi (ambero) kuna wimbo ulisikika ukiimbwa na Marehemu komba radioni wakati huo tulikuwa na radio aina ya mkulima na tulizoea kusikiliza mchezo wa radio ulioitwa chibuku “jangara” ule wimbo uliposikika dada akamuuliza mama, je huyu anaeimba ndiye alikuwa akiimba kipindi kile mjomba Ramadhani a.k.a anko mandevu a.k.a Osama alikuwa anaenda vitani? Mama alijibu ndio, huyu ni mwimbaji wa hizo nyimbo za vita anaitwa komba mtu wa jeshini ni mwanajeshi kabisa na alienda vitani,

Mjomba wetu alipigana ile vita akiwa mstari wa mbele, wakati wa maandalizi ya vita familia ilitega sikio kila mara radioni kwa sababu ya kutaka kujua kinachoendelea ikizingatiwa ndugu yetu alikuwa miongoni mwa wanavita wale,

Hivyo nyimbo zilizotumika kuhamasisha watanzania wajiamini na kulipa jeshi mori na ari zilikuwa zikipigwa kila wakati hivyo baadhi ya watu waliweza kuzikariri,

Siku hiyo Kaka, Dada na Mama waliozisikia nyimbo zilizotungwa na kuimbwa na marehemu komba walianza kuimba kipande huku wakieleza walivyokuwa na wasiwasi juu ya mjomba wetu ambae hata hivyo alirejea akiwa mzima.

Chorus ile ilinivutia ukizingatia nilikuwa na kipaji cha kuimba na kukariri kwa haraka na ndio siku nilipojua jina la mwanajeshi aliyeimba wimbo uliotumika kuwatia moyo wananchi na kuwapa ujasiri na mori wanajeshi.

WALIIMBA….
Tanzania kumezuka…..
Na joka kubwa la kufugwa ni lazima tuliponde life…
Idd Amin Dadaa ni joka kubwa la kufugwa ni lazima tuliponde life….

KOMBA WA JOKA LA KUFUGWA AMETANGULIA, MWIMBAJI NA MTUNZI MAHIRI

Kwa bahati moja au nyingine Baba alirejea na tukatoka kumpokea na hiyo ikiwa mwisho wa stori ile mpaka nilipokuwa mkubwa kiitikio hiki kimekuwa kikiimba kichwani.

Lakini jana baada ya kupata habari za kifo chake nilimpigia mama simu na kumpa taarifa hiyo iliyomsikitisha na kwa bahati nzuri wimbo huo ameniambia anaukmbuka wote, naahidi kuupata.
Je tuna nini cha kujivunia kwa shujaa komba kama sio kukumbuka kazi kubwa aloifanya kwa taifa wakati muhimu kama ule wa vita?

Nawaombea wanafamilia wote Mungu awape nguvu tunawaombea.
Napenda kutoa pole zangu za dhati kabisa kwa familia ya baba yetu kaptain komba,kwakweli kila mwanadamu anamwisho wake.Nimejaribu kusoma habri ya mleta mada alichokiandika unamwona toka moyoni kwake kuwa tukio hilo limemgusa.Naungane naye tupo pamoja na pole sana
 
Nyakarungu,

Umenirudisha mbali sana Mkuu. Marehemu Mama yangu alikuwa pia mpenzi mkubwa sana wa Komba. Nyimbo za kipindi cha vita zilimpaisha sana Komba kiasi kwamba kwa Watanzania wengi kipindi hicho alionekana ni Shujaa.

Ila kuimba na kufanya ni vitu viwili tofauti. Kwamba alikuwa na kipaji cha kuimba na kuhamasisha haina maana alikuwa mtu mzuri kihivyo. Labda kwa sababu tulikuwa hatumfahamu kwa ukaribu.
Ila pia inawezekana kweli kabisa wakati akiimba alikuwa mtu mzuri ila baadaye akabadilika na kuwa mtu ambaye tulikuja kumshuhudia akitishia kwenda msituni na unene wake huo. Mbaya zaidi alipovalia njuga na yeye kuanza kumtukana Jaji Warioba utafikiri kawa Lusinde (Kibajaji). Unajua angelikuwa Lusinde basi watu wangelisema ahh, ni kawaida.

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom