Bunuasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunuasi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mkwaruzo, May 12, 2011.

 1. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unajua bana, siku izi watoto hawafaidi mambo yale ya kukaa na bibi/babu na kutoleana hadithi pamoja na vitendawili. Si unajuwa tena mambo ya teknolojia yalivyo na nguvu, watoto wanaishia kwenye Tv na gemu. Hata enzi zangu mm za **90 Tv zilikuwepo ila zilikuwa hazijapamba moto kama sasa, hivyo nami nilifaidi.
  Kwa kipindi chote hicho tulikuwa tunatolewa hadithi zilizosheheni wahusika kama vile Mzee Sungura, ****, Bunuasi (Abunuasi), Simba, Fisi, Kobe na wengine kibao.
  Hivyo pamoja na kuwa hadithi nyingi zilijumuisha wanyama, niliweza kujua kuwa **** ni mtu lakini akili yake haipo sawa vizuri. Ila kwa upande wa Bunuasi nilifikiri ni mnyama kumbe tofauti kabisa.
  Sasa kwa vile nimeipata historia ya Bunuasi, acha mimi niende ila nitarudi kuja kuwatolea....
  (Lakini mnaweza kuweka vituko vyake huyu bwana na mimi nitakuja na kimoja)
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  wewe lete tu... Mana hata access ya hivo vitabu haipo anymo'
   
 3. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asili ya Bunuasi ni nchi za kiarabu. Na jina la Bunuasi lilitokea baada ya kifo cha baba yake. Na jina la Bunuasi lilikujaje?
  Baba yake Bunuasi alikuwa ni mfalme. Na alimuusia mwanae kuwa kabla ya kuzikwa, nusa pua zangu, zikitoa harufu nzuri rithi ufalme wangu, ila zikitoa harufu mbaya usirithi ufalme huu.
  Siku ya siku ikafika na Bunuasi akafanya kama alivyoambiwa na baba yake. Na alipotakiwa kurithi ufalme alikataa. Aliulizwa ni kwasababu unakataa, akajibu "abuu alwasiya" (Baba kaniusia). Kwa kuwa kila akiulizwa alikuwa anajibu ivyo ivyo, ikaenda enda hadi ikafikia jina la BUNUASI hasa kwasababu alikuwa ni mtu wa vituko.
   
 4. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vitabu vyake vilikua na mafunzo kemkem
   
 5. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siku moja Bunuasi alitangaza kuwa Mungu anamtembelea nyumbani kwake kila Jumamosi, habari zilisambaa hadi zikafika kwa mfalme. Bunuasi akaitwa na mfalme ma kuambiwa aache kuwadanganya watu. Bunuasi akamuambia mfalme hata wewe kama utataka kumuona njoo.
  Mfalme akamuekea masharti Bunuasi kuwa endapo Mungu hatoonekana atamuadhibu. Bunuasi akakubali. Hivyo habari zikaendelea hadi katika uongozi wote wa mfalme. Na kiongozi mkubwa aliyehitaji kuhudhuria katika tukio hilo ni waziri mkuu.
  Jumamosi ikafika, watu wengi walikusanyika nje ya nyumba ya Bunuasi wakisubiria kumuona Mungu.
  Bunuasi hakuonesha wasiwasi wowote ule. Aliingia ndani na kuweka kiti cha kifahari juu ya zulia zuri. Penbeni yake akaweka fimbo na chini mbele ya kiti akaweka viatu. Pia aliweka joho na kilemba. Vyote hivyo aliviweka kwa staili ya kama mtu kakaa katika kiti.
  Baada ya hapo, akatoka nje huku akitabasamu na kusema kuwa Mungu tayari ameshawasili. Pia akasema kwa heshima, ni vyema wakaanza viongozi kwenda kumuona. Na akaongezea kusema kuwa kila mtu atamuona isipokuwa mtoto wa haramu (mtoto wa nje ya ndoa). Hivyo hakuja haja kwa watu hao kupanga foleni kutaka kumuona Mungu, hawatamuona.
  Mchakato ukaanza, waziri mkuu akawa wa mwanzo kuingia...
  Je atatoka na jibu gani? Na ni ipi hatma ya Bunuasi mbele ya mfalme?
   
 6. K

  KILOTI Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupe mambo ilikuwaje hapo kwa BUNUASI
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  baada ya hapo nini kiliendelea?
   
 8. mseseve

  mseseve JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  si umalzie stori tuu ila imejitahdi kuwa tamu
   
 9. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ila mi nina kumbu kumbu tofauti,kitabu nilikisoma mdogo sana primary school,nakumbuka hakuwa mungu alikuwa malaika.Kilichotokea ni kwamba watu wote kuanzia mfalme mwenyewe kila walipotoka nje ya kile chumba,walidai kuonana na malaika na kuongea naye vizuri sana.Wote walikuwa wanafiki,hamna hata mmoja aliyemwona malaika!
   
 10. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pia bunuasi aliweka sharti ya kila anayeingia ndani atoe kiasi fulani cha pesa.Ki ukweli hakukuwa na malaika yeyote pale,ilikuwa ni janja yake kupata mshiko.Bunuasi alitishia zaidi kwamba,usipomwona malaika wewe ni mwovu na akasema akipatikana mtu mwovu,malaika ameagiza kwamba mfalme ampe adhabu ya kifo.Hii ndo sababu wengi waliishia kudanganya kwamba wamemuona malaika!
   
 11. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ....Waziri mkuu akaingia ndani na kukuta kila kitu kama kilivyowekwa na Bunuasi. Mwanzo alimuona bunuasi ni muongo. Lakini hakuwa na uhakika juu ya hilo, hivyo akaanza kufikiria na kujiuliza je yeye ni mtoto wa haramu. Hakupata jibu. Alihofia kusema hajamuona na watakaofuatia baada yake wakija wakisema wamemuona atakuwa amejiingiza katika aibu.
  Ilimbidi atoke na sawa na la Bunuasi. Akatoka na tabasamu huku akifurahia kumuona Mungu.
  Na kila aliyefuatia alikuwa na mawazo kama ya waziri mkuu. Na hofu zao ziliwafanya wadanganye.
  Hivyo Bunuasi akawa ni mwenye kushinda dhidi ya mfalme kwa lile alilolifanya.
   
 12. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayo yalikuwa ya Bunuasi yasiyotofautiana na ya babu wa Liliondo.
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,169
  Trophy Points: 280
  Ukoo ambao unaongoza kwa kupokea mifano ya hundi ambayo inamakosa kibao, bila shaka nao wangesema wamemuona Mungu wa Bunuasi.
  Hahahhahahahahah bunuasi ni big soo
   
 14. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hadithi hii naifahamu japo inatofauti kidogo ila tangu mwanzo wa hadithi hii nilihisi hitimisho lako litakuwa hili.
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama mimi Jaluo White
   
 16. m

  magneto Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jaguarpaw,
  mi pia naijua hi story,lakini muhusika ni ABDUL na si BUNUAS!kawaida kwenye kila tukio bunuasi hushinda mwisho lakini abdul hushindwa kukamilisha;
  hi ilikuja baada ya abdul mpango wake wa kuuza ashes huku akiwaaminisha kuwa ni sugar kushtukiwa,akarudi mjini pembeni ya mji akajeng nyumba ambayo alisema malaika alimwagiza ajenge na atakaa hapo kwa siku kadhaa mtu mwema atamwona na kuongea nae mtu mbaya hatamwona!ndipo watu wakaja wakawa wakiona kiti na viatu lakini wakitoka wanasema wamemwona,habari zikamfikia mfalme naye akaenda akasema amemwona malaika!
  Baada ya siku abdul akaenda kwenye jumba la mfalme,kama vile ameshika kitu kwa uangalifu alikuwepo mfalme na mawaziri wake,akamwambia mtukufu mfalme leo wakati malaika anaondoka amenipa hili koti lake nikupe nawe utanipa mabegi mawili ya dhahabu!akavesha mfalme afu akawauliza mawaziri kama kapendeza wakajibu kapendeza,mfalme akalivua akawa kalibeba kwa uangalifu kulipeleka chumban
  mkewe akamshangaa ndo nini ivyo mfalme naye akamshangaa ina maana hulioni koti?akamwambia hamna koti apo tuweke jiwe likibaki juu koti lipo likianguka koti halipo wakaweka jiwe likaanguka puu!
  Mfalme akarudi ukumbin kama vile kabeba vitu viwili vizito,akamwambia abdul wakati malaika anaondoka alipitia kuniaga na akanipa mabegi haya mawili ya dhahabu ukiniletea koti!
   
 17. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ngoma droo
   
 18. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  dah!kweli mkuu hiki kitabu umekisoma vizuri sana,nadhani nili confuse jina la abdul na abunuasi!
   
 19. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hii hadithi ni very interesting,Big up mkuu Mikwaruzo, jaguarpaw na magneto, realy mmenogesha story, kaka shusha vitu zaidi!
   
 20. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hapo MKUU umechemsha. ABUNUAS hakuwa na akili hizo. Ninavyojua mie ABUNUAS ni jitu JINGA.
   
Loading...