BUNGENI: Wenje amlipua Membe; yeye atoa onyo kwa mabalozi!

Salimia, kwanza nakusalimia, pili crap ni ipi, aliyosema Wenje, au niliandika Membe analipuliwa, kama ni mimi, alichokuwa anafanya Wenje ni kumpaka mafuta Membe, kumuimbia nyimbo za mapambio au kumuwasha?. Wewe subiria jibu la tuhuma kwa wanabalozi ambao nchi yetu ndio kwanza lazima iwalambe lambe miguu kuomba misaada!.

Hivi kweli Tanzania ni masikini kihivi kukesha tukitembeza bakuli?. Hata kuendesha serikali yetu lazima tusaidiwe na nchi za nje?!. Kunatofauti gani kwa wewe umeoa mke huwezi kumtunza, hivyo unaomba msaada kwa rafikizo wakutunzie mkeo ikiwamo kununulia mpaka nguo za ..., unadhani huyo mkeo atamuheshimu nani zaidi, wewe muoaji au mtunzaji?.
 
Hiyo personal life unayoongelea ni ipi? mbona mwingine alisema Membe hawezi kuongoza nyumba yake,, wewe hukuona kama hiyo nayo ni personal?? you are not fair bali umeweka mbele ushabiki tu
 
Hoja za upinzani kwenye wizara hii zote za msingi na wameangalia vipau mbele vyote vya maana
 
Kumbe hawaoni hawasikiii wanategemea nini?
Watashirikianaje na Watu wanaolalamikiwa kila siku ya Mungu na Watu wanao waongoza.Yeye ni Mwanadiplomasia anajua Diplomasia inasimama wapi haswa unapokuwa ndani ya Nchi husika.Asiwafanye balozi husika hawajui kinachoendelea Serikalini dhidi ya Viongozi na Umma wa Watanzania kwa ujumla.

Anajua kuwa Balozi zote duniani huwa zinaendeshwa kiintelejensia zaidi.Kuwafanya wao hawajui nini kinachoendelea Nchini ni kuwatukana matusi makubwa sana.Tena kuna balozi zinatumia Intelejensia kubwa sana wakati mwingine kushinda intelejensia ya Nchi husika.Iweje Leo watawala wetu wawanyanyapae balozi ambao wako hapa kuwawakilisha Wananchi wa Mataifa yao.

Balozi haziko hapa kutetea mateso wanayopata hawa Watanzania,Wapo hapa kushirikiana na Watanzania katika kuakikisha kile ambacho Nchi zao kimewatuma kufanya ndani ya Taifa letu kupitia ushirikiano kama Mataifa huru kinafanyika na kila mmoja anaridhia mahusiano hayo kuwa yanafaida kwa pande zote mbili za Nchi husika.

Kuria kwao hakuta wasaidia kwa kuwa HAWANA MTETEZI.Hata kama ni kweli balozi hizo zinasupport Watanzania waliowapinzaini kiasiasa dhidi ya chama cha Mapinduzi,basi kumbe ni sawa wanatimiza wajibu wao kama Taifa rafiki,haswa wanapoona rafiki yao Mtanzania wa kawaida anaumizwa basi wako tayari kumsaidia hima.[A friend in need is a Friend Indeed]

ITAKULA KWAO HUO NI MWANZO TUU,ITS A TIME FOR CHANGE VINGINEVYO ITAKUWA SIVYO WANAVYOTALAJIA.

YOU CANT EAT YOUR CAKE AND STIL HAVE IT.
 

Mbopo,

Mkuu kenya ambayo inatuzidi kwa FDI,sidhani kama kipindi Godana,Kalonzo musyoka,Rafael Tuju,Moses wetang'ula wakiwa mawaziri wa mamabo ya nje walisafiri sana. Sidhani kama bi nkoana Mashabane wa South Africa anafanya kazi hii anayoifanya Membe au mwanamke wa shoka wa nigeria bi Okonjo Iweala anafanya kazi kama Membe

Hapo kwenye suala la rada ofcourse msimamo wangu ni kwamba ni lazima tuangalie dignity and Intergrity as a nation.Siungi mkono serikali ya uingereza kutuamulia cha kufanya ingawa sisi ndiyo tuliowapa mwanya wa kutudhalilisha.Na membe inabidi aende mbele zaidi kama anajua ni kwa nini yeye ni waziri wa mambo ya nje,inabidi ashinikize serikali iwawajibishe wahusika wote wa kashfa ya rada to restore our pride as a nation na kuisafisha taswira ya Taifa letu ndani na nje ya Nchi.Asibweteke na kuhesabu kuwa kashinda vita.Bado action inastahili kuchukuliwa,hii ni diplomatic Embarrasement sawa na ule uropokaji wa kutuhumu balozi za nje kusaidia upinzani.Membe kama Top diplomat,is this the best he can do?
 

najua wana magamba makundi yenu ndani ya chama yameajiri watu kwenye mitandao kwa malipo maalum, bilashaka wewe ni mwajiriwa wa membe, wapo waajiriwa wa lowasa, wa mzee 6 na team yake nzima ya CCJ na wengine kibao, nakushauri kama kazi zinasumbua mjini bora urudi kijijini ukalime utaheshimika kuliko unavyojidhalilisha na buku 2 za membe. acha kujiuza ndugu, rudi ukalime.
 

RED: Kama nimemsikiliza vizuri Wenje nasema hakusema hivyo. kasema ni dharau kubwa kwa serikali yetu kutopewa hiyo chenji na badala yake kupewa ngos za waingereza. amepigilia msumari kuwa serikali iwachukulie hatua "wazalendo" waliohusika katika uchafu huo au la wananchi wanaweza shindwa amini usalama wa hiyo chenji itakaporudishwa.

mchango wa waziri kivuli nimeupenda hadi wana magamba wanamuunga mkono e.g. Mh Manyanya
 
Crap! Au umetumwa kumjenga Wenje baada ya wana Mwanza kumtuhumu kuwadanganya na kuhamia Dar? Na kwamba alipokuwa anaomba kura alijidai mlokole na sasa anakunywa pombe ya kufa mtu? Stop manipulating people here!
Kumbe ulokole dili ktk siasa za bongo eeh..!! Mimi mwenyewe wa bugarika Mwanza, mbona sijamtuhumu Wenje kama unavyoropoka hapa...
 
Wewe umeajiriwa na nani??
 
Tangu nimsikie Membe akiongelea kuhusu suala la madagascar wakati wa sakata la Rajoelina na Ravomanana, nilimwona jamaa kama jitu gambafu ambalo linadhani umma hauwezi kuamua nn kifanyike na kiwe. Kwa sasa umma wa wa-tz ushaanza kuinua vichwa, siku inakuja vitaanza kutingisha kushoto kulia na wanaoshabikia u matonya wa serikali hii itabidi waungane na wengi kuleta usawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…