Mh. Rais hongera kwa kuvunja rekodi hizi, Bado moja tu!

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Mheshimiwa Raisi, binafsi nakupongeza kwa uongozi wako, tangu uingie madarakani umevunja rekodi nyingi tofauti na awamu zote zilizotangulia lakini bado moja tu. Kabla ya kuitaja, naomba nigusie baadhi ya rekodi ulizovunja.

Umevunja rekodi ya kuwa Rais wa awamu hii. Wewe mwenyewe unakiri kuwa walikusukumizia huko. Na hii ni baada ya kundi A kumwaga mboga na hivyo kundi B kuamua kumwaga ugali.

Umevunja rekodi ya kuungwa mkono na wapinzani hali inayowapelekea kujivua nafasi zao za kisiasa za ubunge na udiwani na kujiunga na chama tawala na kupewa nafasi za kugombea nafasi ileile na kushinda. Kubwa zaidi ni pale mgombea uraisi wa upinzani alipoamua kuunga mkono juhudi. (Je, naye atapewa nafasi ya kugombea nafasi ileile? Ha ha ha, natania!)

Umevunja rekodi ya kuzuia kufanya mikutano ya kisiasa na kufanya maandamano ya kisiasa hadi uchaguzi ujao. Hii ni mpya na haijawahi kutokea. Halii hii imepelekea kutokea mtu maarufu na misemo yake miwili iliyojizolea umaarufu; "watapata tabu sana na watapigwa hadi wachakae"

Umevunja rekodi ya kutosafiri nje ya nchi isipokuwa Afrika mashariki. Pia umevunja rekodi ya kutohudhuria mikutano ya kimataifa ambapo huwatuma Makamu wa rais ama Waziri Mkuu ama Waziri wa Mambo ya Nje ama Mabalozi. Umeokoa pesa nyingi.

Umevunja rekodi ya kufanya ziara nyingi ndani ya nchi kuliko nje ya nchi. Umeonesha uzalendo. Umevunja rekodi ya kugawa pesa taslimu katika ziara mbalimbali hali inayopelekea wenye shida mbalimbali kukusubiria ili utatue kero zao.

Umevunja rekodi ya kutolihutubia taifa kila mwisho wa mwezi kupitia radio na televisheni tofauti na awamu zilizotangulia.

Katika awamu hii, umevunja rekodi ya kutoonesha Bunge Live na kupitisha sheria ya vyama vya siasa. Kwa mara ya kwanza sauti moja ya waliosema "siyooooo-ooo" Bungeni imeshinda sauti za waliosema "ndiyooooooo".

Umevunja rekodi ya kununua ndege za dreamliner, bombardier na airbus kwa pesa taslimu. Pia umevunja rekodi na kuikodisha ndege ya Rais katika shirika la ndege la taifa. Kujenga reli ya kisasa na maflai ova.

Kwa muda wote uliokaa madarakani, umevunja rekodi ya kuwanyoosha watumishi wa umma kwa kutowaongezea mshahara, kutowapandisha madaraja, kutopandisha kima cha chini cha mshahara, kutumbua wenye vyeti feki na wasiowajibika, kuzuia uhamisho kwa muda mrefu na kujenga nidhamu kazini. Sasa hivi hakuna tofauti ya mshahara kwa mtumishi ajira mpya ya 2012 au 2013 na ajira mpya ya 2019, wote ngoma droo.

Umevunja rekodi kupitisha sheria zinazoongoza namna sahihi ya kutumia vyombo vya habari. Umevunja rekodi kupitisha sheria ya takwimu hadi IMF wanaisoma namba. Wanatusingizia eti uchumi wetu utakua kwa 4% wakati waziri wetu wa fedha alitwambia utakua kwa 7.3%.

Umevunja rekodi ya kubana matumizi ya serikali. Umehamisha baadhi ya mafungu kwenda ofisi ya Rais ili kudhibiti ufujaji wa pesa ya umma. Huku mtaani siku hizi hawadondoshi hata mia, hakuna anayeokota hela njiani kama zamani. Jero imerudisha heshima yake, inaitwa mia tano.

Rekodi moja kubwa iliyobaki kuvunjwa ambayo itafanya historia ikuandike vizuri zaidi hata kama kuna mapungufu katika uongozi wako, ni kuongoza awamu moja tu. Uchaguzi ujao waache hao wengine wanyukane wenyewe.

"The Stone (Jiwe) was rolled away from the Door, not to permit Christ to come out, but to enable the Disciples to go in. Happy Easter!"
 
Amevunja rekodi nyingi sana kwa kweli na itachukua miaka mingi kuja kuvunjwa na mwingine.
 
Mkuu katika kipindi kifupi ameweza kutuonyesha dira kua tukiamua kubadilika na kupata maendeleo ya taifa letu bila kuwategemea mabeberu na wanyonyaji inawezekana, miradi mikubwa ya maendeleo imefanyika katika kipindi kifupi cha utawala wake, kuna kasi kubwa ya ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, wafanyakazi na watumishi wa serikali pia wameanza kuwajibika tofauti na awamu zilizopita, muhimu ni wananchi wote tuwe wazalendo kuhakikisha nchi inasonga mbele.
 
Mkuu katika kipindi kifupi ameweza kutuonyesha dira kua tukiamua kubadilika na kupata maendeleo ya taifa letu bila kuwategemea mabeberu na wanyonyaji inawezekana, miradi mikubwa ya maendeleo imefanyika katika kipindi kifupi cha utawala wake, kuna kasi kubwa ya ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, wafanyakazi na watumishi wa serikali pia wameanza kuwajibika tofauti na awamu zilizopita, muhimu ni wananchi wote tuwe wazalendo kuhakikisha nchi inasonga mbele.
Tungekuwa tunavitaja hivyo viwanda kwa majina ingependeza zaidi
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom