Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Boral livunjwe tu sababu vilaza wengi badala ya kujadili hoja za msingi wanakaa kurushiana vijembe utafikiri wameenda kuimba taarabu
 
We matope sema bunge livunjwe sio kuja na umanamba wako eti lisionyeshwe live,hata kama ngumi zinapigwa lionyeshwe wananchi wawaone wawakilishi wao.
 
Ukosefu wa Elimu sio chanzo cha matusi, wazazi wetu wengi hawajui hata kusoma ila wametulea tukiwa na nidhamu na heshima kwa kila kiumbe. Nenda vijijini kama utakuta watu wenye Lugha kama za hawa wabunge. Watu kule wana nidhamu bila shuruti wana Mwogopa Mungu na ni wema sana. hakuna udini wala ubaguzi. Matatizo yetu yako dodoma na ni mkakati wa MaCCM kutukana ili kuvivisha mijadala yenye tija kwa Taifa

Aibu yao Makinda na Ndugai.
 
Ni kweli! Inaniuma sana ninapokumbuka kwamba sehemu ya kodi inayokatwa katika mshahara wangu huishia mikononi mwa wabunge wa JMT!
 
Chadema washaliharibu Bunge.

Hamad Rashid aliuongoza upinzani Bungeni vizuri zaidi. Mbowe uongozi wa upinzani Bungeni hauwezi...
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Chadema washaliharibu Bunge.

Hamad Rashid aliuongoza upinzani Bungeni vizuri zaidi. Mbowe uongozi wa upinzani Bungeni hauwezi...

kama alifanikiwa sasa yuko wapi?

kutoendelea kwake kuwa kiongozi wa upinzani ni kufeli na hilo halina ubishi maana hata chama chake kimedhoofu sana.
 
CCM na serikali yake kushindwa kuukubali ukweli, kuisimamia haki na kutimiza majukumu yake kwa Taifa ndiyo chanzo cha

migogoro na kudidimia kwa taifa letu.

Endapo Spika na wasaidizi wake watafuata sheria na kanuni za bunge na kuisimamia serikali, bunge litakuwa na weledi,

lakini kushindwa kufuata utaratibu, sheria na kanuni katika kutekeleza majukum yake ni kuwazalilisha watanzania kwa

kushindwa kuwa na wawakilishi makini hususan kambi ya ccm kuwapuuza na kuwazalilisha wale wa upinzani ni kuamsha

mihemuko isiyo na tija kwa taifa na kulifanya bunge lionekane kituko na ovyo kabisa.
 
Chadema washaliharibu Bunge.

Hamad Rashid aliuongoza upinzani Bungeni vizuri zaidi. Mbowe uongozi wa upinzani Bungeni hauwezi...

Mkuu unafikiri sasa hivi watanzania wanaweza kudanganyika kirahisi hivi???Tena huku mnakosema vijijini watu wanauelewa wa kutosha sana,ni suala la mda tu.
 
Lisu alikua anavuruga kibabe tu Na bila ustaarabu wowote , Ni Kama mjadala kwenye bar ya pombe Za kienyeji . Ile heshima ya uwakili Na ubunge haipo kabisa Kwa Mh. Lisu.
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Mama Makinda was right, bunge limekua kama soko la Kariakoo, inakera kwa kweli.

Huu ni upuuzi kama baba anasema nyumba yangu kama genge la wahuni. Nani katengeneza hilo genge kama sio yeye
 
Huu ni upuuzi kama baba anasema nyumba yangu kama genge la wahuni. Nani katengeneza hilo genge kama sio yeye

Kwa hiyo we ulitaka aingie mdomoni mwa Serukamba na Nkamia awazuie wasitukane? bado siamini kama udhaifu wa huyu mama ni sababu ya kuhalalisha matusi bungeni. ni watu wazima tu wameshindwa kujiheshimu.
 
Wote mko sawa,tunaheshimu mawazo yenu,ila kosa ni hukumu ya moja kwa moja kwa CCM kwamba ndio inaleta udini.TAtizo Sasa linazidi kuwa kubwa.Wanasiasa fanyeni siasa,Huko mna wanachama wa dini mbali mbali. Huko Kwenye nyumba za Ibada nako yafanyike mahubiri kulingana na vitabu vinavyowaongoza,pia Huko kuna waumini ambao ni wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa. Wa siasa wafanye siasa na wa dini wafanye dini. Dini moja isiingilie taratibu za dini nyingine,kufanya hiyo kutasababisha msuguano katika jamii .Huko bungeni wabunge wajadili kutatua matatizo ya wananchi wakiwa wawakilishi wao na sio kujadili mambo ya dini,hayawahusu.Sheria za nchi zipo,wanaotaka kusababisha maafa kwa sababu ya u dini ni wale wasioenenda na utaratibu nilioeleza .Serikali ichukue hatua Kali bila kujali mkosaji ni nani katika jamii,ashughulikiwe ki Sheria ili iwe fundisho kwa wengine watakaojaribu kuleta machafuko.
 
Nawapongeza sn wapinzan hasa Chadema kwa jins walvyo wavumilivu na kua na subira kwa kutokujbu matusi. CCM wakt wao umekwisha wa kutawala nchi hi. Kilichobakia ni kujihami tu, ushaur wangu to all honest MPs wawe makin sana na hawa maccm. Imeniskitisha sn jns ccm wanavyowashambulia CHADEMA hasa pale wanapowapa ukwel.
 
Kila mtu alieangalia bunge siku ya leo bila shaka atakuwa akijiuliza maswali kuhusu mwenendo wa wabunge wetu hawa na kama kweli wanafahamu nini wajibu wao kwa wapiga kura wao.

Mimi najiuliza hawa wabunge wanatofauti gani na mateja au wapiga debe wa stand kwa kauli zao hizi za matusi ndani ya bunge?Hivi si bora hata kichaa kwasababu ni mgaonjwa wa akili ila hawa wabunge nao ni wagonjwa wa akii?Hivi wanamdhalilisha nani kama sio wao wenyewe,ndugu,jamaa,marafiki na familia zao?Hivi hawa wabunge wanastahili kuitwa waheshimiwa na wao kujiita waheshimiwa?Hawa wabunge kweli wanastahili kulipwa mamilioni ya shilingi kila mwisho wa mwezi kama mshahara na marupurupu kwa upuuzi huu?Hivi bunge limegeuka band ya kuimba taarabu(mipasho)!

Mimi nisema kama hali hii itaendelea mpaka 2015 basi tusishangea kuona idadi ya wapiga kura ikishuka kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi mkuu ujao kwani ni nani atakuwa tayari kuendelea kupanga foleni kuchagua "mateja" na kuwapa ticket ya kwenda bungeni!

Leo hii nimeamini ile kauli ya naibu spika alieitoa katika mahojiana na mtangazaji mmoja kwenye TV station moja hapa nchini kuwa kuna wabunge wanavuta bangi!

Bunge hili ni janga la kitaifa pengine kuliko hata ukimwi!

Mwisho namshauri mh.Spika kesho, mara tu baada ya salaa ya kuliombea bunge, atoe kauli ya kuwaomba radhi watanzania wote kwa mwenendo mbovu wa bunge analoliongoza.

We vipi? Una MALYENGE nini?? Tatizo ni SPEAKER & COY, wao ccm wanadhani bunge ni mali yao binafsi!! Sometimes inabidi wapinzani wawe TOUGH ili kukabiliana na bado ngumi. Hujaona mabunge mengine kama Italy, Ukraine zinapigwa?? Hakuna kulemba CCM wakileta ubabe unajibiwa kwa ubabe hakuna MCHUMBA pale!!!!!!!!!!!!
 
Salamu jf,
nini kifanyike kuinusuru hali inayoendelea bungeni? Tupeni ushauri hapa ili ndugai na wenzake wakipita hapa wapate kitu.
 
Mama Makinda aolewe! Job ****** aserukambiwe na serukamba
 
Back
Top Bottom