Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Nampa big up mbunge aliyemuumbua mbunge aliyejamba Acheni kabisa harufu mbaya inatesa

Leo Mbowe kesho mwingine ataibuka na kusema waziri mkuu na keshokutwa mwingine ataibuka na kudai ni spika au naibu spika sasa sijui na hao nao utawapa big up?!

Usifikirie ya leo tu, kuna kesho na keshokutwa!
 
Wakati mwingine mambo wanayosema viongozi wetu nayo yanakwaza sana,fikiria mtihani wa kitaifa unafanyika,65% ya wanafunzi
wanapata Zero,halafu mtu mzima
kama Chiligati anasimama na kuisifia
serikali kwa kigezo eti tangu Kikwete aingie madarakani idadi ya madarasa imeongezeka!
 
Mama Makinda was right, bunge limekua kama soko la Kariakoo, inakera kwa kweli.

Ndugu kumbuka

1. ukiona familia inayumba ujue tatizo ni kiongozi wa familia
2. Ukiona nchi inayumba ujue tatizo ni kiongozi wa nchi
3. Ukiona Wizara inayumba ujue tatizo ni waziri husika wa wizara hiyo
4. Ukiona BUNGE linayumba ujue tatizo ni SPIKA wa Bunge
**Kumbuka wakati wa Samwel Sitta hakukuwa na upuuzi huu tunaouona sasa haya yote ni matunda ya CCM kwa kumweka Spika asye na uwezo ili mambo yao yaende**
 
Halafu kuna Wabunge wametamka kwenye Mic kwamba watamshughulikia Wenje, nadhani ni wale Wanzibar, kwa hiyo lolote litakalo mpata Wenje inabidi wahusike,kwa kuwa tayari iko kwenye Hansard.
 
Halafu kuna Wabunge wametamka kwenye Mic kwamba watamshughulikia Wenje, nadhani ni wale Wanzibar, kwa hiyo lolote litakalo mpata Wenje inabidi wahusike,kwa kuwa tayari iko kwenye Hansard.

Mkuu hata mimi nilimsikia na bili shaka hiyo kauli hitapita bila kujadiliwa,
 
bunge dhaifu la wabunge dhaifu linaloongozwa na viongozi dhaifu nimatokeo ya wananchi dhaifu wanaoshindwa kuwawajibisha wabunge wao
 
sidhani kama Serikali inaweza kulitii bunge ha ovyo kama hili.!
 
Hata Mkamia na Lusinde wanapokea posho yenye kodi yangu?.Hapana hii nitaipinga.
 
Mkamia, ''SIONGEI NA MBWA NAONGEA NA MWENYE MBW''. Mkamia hata wewe? Kweli nchi inaangamia kwa kukosa viongozi wenye maarifa
 
Tukiwa tunachangia ni bora pia tukajiuliza chanzo cha hayo yote ni nini.Kusema tu kwamba tumepeleka vichaa bungeni mi naona sio sahihi...lazima kuna tatizo ambalo tunatakiwa ku address badala ya kulaumu na kuleta siasa kwenye mambo ya msingi.Bungeni kuna kanuni ambazo zinaliongoza bunge katika mijadala ya kila siku.Inapofika wakati kanuni zinatumika kuwwabana baadhi na kuwabeba baadhi,upande mmoja utaumia.Na inafika wakati wanakata tamaa.Ikifikia hali hiyo lazima yatokee haya tunayoona.Mmoja anapotukana hachukuliwi hatua kuna mwingine atajibu mapigo na matokeo yake ndiyo hayo
 
Tatizo kubwa ni viongozi wa Bunge wa sasa kuuvunja mhimili wa bunge na kuunganisha na Serikali, sasa anaepaswa kuisimamia serikali hawezi hata kujisimamia mwenyewe.
Hii imetokana na viongozi wa Bunge kuitetea serikali badala ya kuiacha ijitetee yenyewe hasa Makinda na Ndugai,
Pili, viongozi wa bunge kuruhusu vita ya maneno, wakati wapinzani wanajadili hoja, CCM wanajadili propaganda na maisha binafsi ya wenzao plus shukrani tele.

Kwa kawaida bunge la mijadala yenye maslah kitaifa huwa na pande mbili, SERIKALI na WABUNGE, Lakin kwasasa kuna pande nne SERIKALI, WABUNGE CCM, WABUNGE UPINZANI, na VIONGOZ WA BUNGE.
Hii imejidhihirisha hiv karibun kwan Hoja hata iwe nzur na yenye manufaa kwa taifa, itatizamwa imetoka upande gani na yeyote kati ya hizo pande (isipokuwa upinzani) anaweza kukwamisha.

Kwa kifupi tukubali tu, kuwa hatuna bunge, na pesa yetu ya kodi inapotea bure pale, sababu kubwa kuliko ni Presha ya uchaguzi 2015.
 
Heshima huja kwa mtu anayejiheshimu pia. Ukitaka kujua kama mti umezeeka angalia matawi ya mwisho juu kabisa ya mti utaona yanaanza kukauka, hapo ujue huo mti unafikia ukomo. Pia kwa walaji wa samaki ukitaka kujua kama samaki ameoza angalia kichwani. Wengi hupendelea kunusa kwenye mapezi. Mifano ya mti na samaki inaashiria kuwa ukitaka kuangalia uimara au uozo wa uongozi angalia viongozi wa juu kabisa wa taasisi husika. Mwazo wa kuwa na bunge la wahuni limeaasisiwa na viongozi wa bunge WAHUNI. Viongozi wa bunge WAHUNI wameletwa na chama cha WAHUNI. Labda ipo haja ya kujua Mhuni ni mtu wa namna gani. Mhuni katika jami ni mtu asiyeaminika, asiyesema ukweli, mwenyekupindisha mambo. Asiyeona haya kuibadilisha ndiyo ikawa ni hapana, mtu anayekubali hili leo kesho pasipo aibu akaukana ukweli aliusema kwa kinywa chake.Hivi ndivyo ilivyo kwa viongozi wa bunge. Viongozi wanabadilisha kanuni za bunge kwa maslahi ya chama. Chama pia kinaukataa ukweli, pale wananchi wanapokataa kukipa kura wanaiba kura wakisaidiwa na vyombo vya dola. Watu wanajua hivyo. Ni ndoto kufikiri kuwa chombo au chama cha namnahiyo kitaheshimiwa. Waslam wana usemi unaosema 'ukicheza na mbwa, utaingia naye hadi msikitini' Msikitini ni mahali patakatifu na mbwa ni najisi kwao. Ukizoea kucheza na najisi hajui mahali patakatifu. Kosa sio la mbwa ni la yule anayecheza na najisi.
Na sasa ndio naona sababu za kufanya bunge lisionekane live, inabidi liwe linahaririwa kwanza...Imefika mahali ukiona inafika zamu ya wabunge fulani ni kama unaangalia muvi ya X ukiwa na familia sebuleni....mapigo ya moyo yanaongezeka. kama hawa tunaowaita viongozi wanaenda kufanya UHUNI bungeni tutegemee nini kutoka kwenye jamii ya kawaida mitaani kwetu ? Mtu anayemsema mwenzake kajamba kwenye hadhara ndio huyo huyo kesho akwambie usiibe...usizini...usiseme uongo. Nalazimika kuamini hata kati ya wachangiaji wanaotumia lugha za matusi humu baadhi yao ni hao tunaowaita waheshimiwa..Kama mtu mzima anadiriki kutamka matusi hadharani..mbele ya TV seuse humu alipoficha utambulisho ? Ushauri wangu kwa SPIKA na naibu wake, waje na sheria (iwapo hakuna) kwamba mbunge anayetamka tusi basi mchango wake uishie pale pale akae chini..Tupo wengi tunaoumia na mwenendo huu usio wa kiungwana, mtu unaona aibu kwa niaba ya anayeongea. TUNAHITAJI VIONGOZI WANAOJIHESHIMU. Wapo baadhi ya wabunge wanaposimama unapata amani ya kumsikiliza anavyojenga hoja na kujibu shutuma(kama zipo) bila lugha za kihuni wala jazba zisizo na msingi, Pongezi kwao...
 
Mkamia, ''SIONGEI NA MBWA NAONGEA NA MWENYE MBW''. Mkamia hata wewe? Kweli nchi inaangamia kwa kukosa viongozi wenye maarifa
Kwa mtu kama m 23, hataliona hili... yeye anachoweza kuona ni CCM hawatukani na CDM ndo wanaotukana ....bhaaaaaaasi. Anasahau kuwa tusi litabaki kuwa tusi hata kama limetukanwa na unayemuamini kupita kiasi... ANY WAY ...........The best way to convince a fool that he is wrong is to let him have his way
 
Mkamia, ''SIONGEI NA MBWA NAONGEA NA MWENYE MBW''. Mkamia hata wewe? Kweli nchi inaangamia kwa kukosa viongozi wenye maarifa

Maneno ya Wabunge wa CCM huku Ndugai akifurahia:
  1. Msigwa ni Mchungaji wa Nguruwe
  2. Bara Kina mama hutembea uchi
  3. Tusiruhusu Wapinzani washike shike "Ikulu"
  4. Sindano ni lazima iingizwe uzi kwenye tundu nyuma ili ishone
  5. Wenje tutakufanya nk
  6. Impotent ni -------
  7. Mbowe "Kajamba hapa" akakimbilia Kibaha
 
Tuliwaweka wenyewe hao waimba hip hop na wengineo, kwa hivyo tutarajie zaidi ya hivyo.
 
Ndugu zangu mnatakiwa muelewa kwamba wabunge wanatuwakilisha sisi wananchi. Jinsi hali ilivyotete Bungeni vivyo hivyo huku mtaani. Na nawaona wamejitahidi nakumbuka Sugu aliongea kwamba wangeamua kufuata mizuka ya wananchi wangetwangana bungeni, tuangalie hoja na tuwe wachujaji takataka tupa kule.
 
bunge la spika ana makinda limekosa nidhamu, hii inatokana na tatizo la spika mwenyewe kama baba au mama kushindwa kusimamia vizuri. familia ya bunge ni mbovu na haina maadili. mama mipasho wabunge mipasho tunapata bunge la mipashano. waweke na bia kabsa pale mezani pao na si pipi.
 
Nikifuatilia mijadala bungeni, nimeona mara nyingi kauli zikitolewa toka vyama vyote, chama tawala na vyama vya upinzani, kwamba tuna wabunge wapumbavu. Baadhi ya viongozi wamekuwa wakichachamaa na kusema kuwaita wabunge au viongozi wa serikali wapumbavu ni kwenda mbali mno.

Najua kwamba Biblia inatumia neno mpumbavu, na ninaamini Biblia ni kitabu kitakatifu, si kitabu cha matusi. Kwa hiyo basi, kama tuna wabunge wapumbavu yawapasa wabunge walikubali hilo na kurekebisha upumbavu wao badala ya kulalamika kwamba wanatukanwa.

Labda kwanza wana Jamii Forum, kama kioo cha jamii, tunapaswa kuwaeleza hawa Wabunge wetu (nachelea kuwaita waheshimiwa, maana huwezi kuwa mheshimiwa na mpumbavu kwa wakati mmoja) mambo mawili ya msingi

1. Mpumbavu ni mtu wa aina gani.
2. Ni kauli au matendo gani ya mbunge au kiongozi yatamfanya astahili kuitwa mpumbavu?


***********

Hadi sasa nimepata yafuatayo ya msingi, kwamba mtu atastahili kuitwa mpumbavu ikiwa;

1. Yeye hajui kitu, ni mbulula, mjinga, na hana hekima wala busara, hafikiri, hajitambui
2. Hatumii muda wake kufanya yale anayotarajiwa kufanya kwa wakati huo, kutofanya mambo ambayo ametumwa na yasiyo na kutetea mambo yasiyo na maslahi ya wananchi waliomtuma (ndani na nje ya jimbo lake), na kwamba yeye hafanyi mambo yanayowaondoa Watanzania kutoka hapa pabaya tulipo.
3. Anayetaka kuthibitisha uwongo kuwa ukweli
4. Anayetengua kanuni za Bunge kwa manufaa yake binafsi au kikundi chake
5. Anaeweka mbele maslahi yake binafsi badala ya watu waliomchagua au taifa kwa ujumla
6. Hapendezwi na maneno mazuri yanayotolewa na wengine

Najua kuna mengi zaidi yatakuja
 
Mpumbavu= asiuejua kitu, mbulula, mjinga , asiye na hekima wala busara , asiyefikiri, asiyejitambua, mpuuzi, mshenzi mshenzi = mchanganyiko wa yote hayo.
 
Tusome Mistari ifuatayo katika Mithali 17:

7 Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu; Siuze midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
10 Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu, Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.
12 Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.
16 Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
21 Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe; Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
24 Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
25 Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye, Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
 
Back
Top Bottom