Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?

Wala haihitaji uwe mwenye akili za ajabu kujua kwamba ukosefu wa heshima kati ya wabunge na wabunge, na wabunge na uongozi wa bunge umetokana na jinsi Makinda na Ndugai wanavyoliendesha bunge. Mambo yaliyolifikisha Bunge letu katika hadhi iliyopo ni kama yafuatavyo;

1. Utaratibu wa hila na ubinafsi uliotumika kumpata Spika wa sasa na kumwondoa Spika aliyekuwapo kabla yake
2. Kuruhusu wabunge wa chama tawala kukejeli na kuonyesha dharau kwa kila kauli au hoja inayotolewa na wabunge wa vyama vya upinzani
3. Wabunge wa chama tawala kutoelewa wajibu na kazi ya chama cha upinzani bungeni
4. Matumizi ya kanuni na taratibu za bunge katika namna ya kuwanyima uhuru wa uwakilishi wao wa kibunge wabunge wa vyama vya upinzani
5. Kuruhusu kanuni na taratibu za Bunge zivunjwe na wabunge wa chama tawala bila uongozi wa bunge kukemea au kuchukua hatua yeyote
6. Tabia ya wabunge wa chama tawala kuunga mkono au kushabikia kila kauli na hoja inayotolewa na wabunge wenzao wa chama tawala, hata kama kauli au hoja hiyo haina maslahi kwa taifa na wananchi
7. Kutumia nafasi ya uongozi wa Bunge kwa maslahi ya chama tawala na Raisi badala ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Kauli na vitendo visivyo vya kawaida tunavyovishuhudia bungeni ni matokeo tu ya mambo hayo saba yaliyoorodheshwa hapo juu. Ikiwa Makinda na Ndugai wana nia ya kweli ya kurejesha heshima ya Bunge machoni pa wananchi wanapaswa kushughulikia mambo hayo, vipengele 2-7. Hii itasaidia kujenga heshima kati ya wabunge wenyewe, wananchi kuwaheshimu wabunge na Bunge.

Yaani sijaelewa kabisa kisa na mantiki ya Moderators kuiunganisha hii thread ya "Makinda na Ndugai ndio chanzo cha Bunge kukosa heshima. Suluhisho ni hili" na "Bungeni tumepeleka vichaa, wendawazimu au mateja?" Haya ni mambo mawili tofauti na Moderators mnapaswa kuwa na uwezo wa kuliona hilo.
Ikiwa nitawasema wengi wa viongozi wa Tanzania kwa kutokuwa na umakini katika kufanya maamuzi, basi sina budi kuwasema baadhi ya JF Moderators kwa kosa hilo hilo la kutokufanya maamuzi ya makini katika ku-moderate. Moderation inawapa power ya namna fulani, sasa mnaweza mkajikuta mna-abuse hiyo power na kutufanya baadhi yetu wana JF kuanza kuhoji kama tunastahili kushiriki katika social forum inayokuwa moderated kwa namna hii.

Kama mmefanya hivi kwa ajenda nyingine basi tuambiane.
 
Niliwahi kuzungumza siku za huko nyuma kuwa bunge letu halina maana,kama limeweza kusahau kazi zake na kuwa mtetezi wa serikali unategemea nini,lakini pia nilishauri ikibidi wabunge wajiuzuru maana kinacho fanyika ni zaidi ya the comedy.

Kingine Spika aliwahi kukiri kuombwa na watu fulani ili achukue fomu ili kupambana na mh Sitta,Sitta alionekana kama mpinzani wa chama chake ndiyo maana kilichofanyika kwa mh fulani aliyejivua gamba ni kumuomba madame spika apambane na mh Sitta ili kuja kuficha udhaifu wa serikali dhaifu,alkini alisahau kuwa udhaifu kamwe haufichwi kwa udhaifu wa mdhaifu
 
Wanasiasa ni very opportunistic...wanapenda kufanya kile wanachoona wananchi wanakishangilia...kwa sababu ukiacha uongo "they always think of popularity and the next election respectively"...
Sasa kama mtu anaongea utumbo...halafu anakuja kuona walioongea ya maana hawajasifiwa wala kuandikwa magazetini na kwenye media nyingine....halafu yeye wapumba anakuta "amchana fulani" "atikisa bunge" "avunja ukimya" "awapoteza wapinzani" "ampasha flani" n.k...
TUACHE KUSHABIKIA UJINGA HATA KAMA MBUNGE HUYO NI YOUR SPOUSE WATAJIREKEBISHA.....
 
Bunge ze komedi..wastage of taxpayer's money. Akili za tumboni mbaya sana.

Nawalaani wabunge wote wehu na waporomosha mitusi. Watu wazima hovyoo. Mnapotosha jamii hususan watoto wakisikia pumba zenu.

This too shall pass
 
Chuki, kweli ipo kama jina lako. Hili bunge laiti ungeambiwa uwe unaangali wewe tu then una repot kwa wana jf ungedanganya umma. Sasa wale waliotoa lugha za matusi leo walikuwa cdm tu? Be honesty Chuki!! Kwa taarifa yako kama umeambiwa basi mi nimeona.

Mtoa maada ndg Salary Slip, hajaegemea upande wwte na yupo sawa kbs kwani kama ni aibu kwa sisi raia wa kawaida ambao tunasikiliza na wale wabunge sio ndugu zetu, je kwa familia zao, rafiki zao, na waliowasaidia kuingia bungen wengine kiuchumi, kura n.k itakuwa vp? Mch. Msigwa, sugu, mwigulu nchemba, lusinde, juma nkamia ila yy nadhan kaomba msamaha palepale kwan kakiri kuropoka lile neno, wenje, kuna mbunge wa zanzibar CUF sikumshika jina lake alisema msigwa mchungaji wa nguruwe, jah people wa makambako, tundu lisu n.k ni baadhi ya wabunge ambao kwa kweli wanatakiwa kujirekebisha na kama hawatabadilika nitawashangaa wananchi wanaoongozwa na hawa wabunge watawarudisha tena bungeni 2015. Wanatia aibu na hii ni list ambayo wengi wao wamechangia leo 15.4 tu. Very shame....


Asante kwa uchambuzi mzuri lakini nimepata shaka na tuhuma kwa mchungaji Msigwa ambaye nilimsikia akinukuu kifungu toka kitabu Kitakatifu yaani Biblia. Na alinukuu maneno yaliandikwa na mwandishi wa Methali. Labda ingekuwa vyema akama angakuwa amepewa nafasi na kudadavua maandiko hayo katika muktadha chanya wa kitheolojia. Hayakuwa maneno yake na baadae akaongezea ya kwakwe ambayo aliwalaumu watu walioko kwenye vyombo vya maamuzi kwa kutochukua hatua ama kuzuia au kuwajibisha wote waliohusika na utoroshwaji wa twiga, wizi wa EPA, Meremeta na mengine kama elimu mbovu. Na alimlaumu waziri mkuu kwa kushindwa kumjibu kwa ufasaha alipotaka majibu ni kwanini Zanzibar wanawalazimisha wasiokuwa Waislamu kufunga. Labda lililokuwa na utata kidogo ni pale aliposema akili ndogo kuongoza akili kubwa. Huyu namtetea mbali na sentence yenye ukakasi kidogo lakini alikuwa anaagalia maslahi mapana ya nchi ambayo watawala wameyaharibu kwa kushindwa kuwajibika na kuwajibishana na matokeo yake ni mabaya sana kuliko hata na sentensi yake. Naomba kusahihishwa kama nimeongeza na nimechakachua
 
mambo haya hayaepukiki katika bunge la vyama vingi. Nchi za wenzetu tumesikia watu wanachapana mkono kabisa. kuna mambo yanakera kwa kweli. Kinachowashinda wengi ni kushindwa ku handle temper zao. Soon tutaona ngumi live!
 
Tatizo la Bunge letu sichelei kusema lililokuwa TUKUFU kwa sasa halina hadhi ya kuitwa hivyo.Hata wabunge sidhani kama wanahaki ya kuitwa waheshimiwa.

Tulipime Bunge letu kwa kipimo cha kawaida cha familia.Leo baba anashindwa kumwadabisha mtoto wake lakini yupo makini kumwadabisha mtoto wa mwenzake.Tuone viongozi wetu Waziri Mkuu ,Lukuvi na wanaokalia kiti cha spika,(Spika,Naibi Spika na wenyeviti) kama wawakilishi waliochaguliwa kwa upande wa CCM walitakiwa kuwa wakwanza kuwakemea wabunge wa upande wa CCM ili kukiweka chama chao katika sifa njema,lakini badala yake wanaenda na kulaumu vyama vya upinzani kuwa ni wakorofi ndio yale ya baba ameshindwa kumwadabisha mtoto wake anakimbilia kwa wa mwenzake.

Viongozi wetu wanaoliendesha bunge wamekuwa dhaifu sana kiasi kwamba wamelifanya bunge kama kilabu cha pombe tena mbaya zaidi siyo kile cha kistaarabu bali cha wanywa gongo kabisa.Haiingii akilini Mbunge anasimama anatukana kiongozi wa kambi ya upinzani Spika anashangilia na kupigilia misumali kabisa kwamba safi sana "Mkuki kwa nguruwe.........."Huyu ndiyo kiongozi watanzania tunayedhani atatenda haki.

Spika anashindwa kufuata kanuni za bunge,anapitisha miswada inayolifanya bunge kuwa kibogoyo,linakosa MENO na KUCHA za kuichachafya serikali ,amekuwa ni mtu wa NDIYO mzee,sichelei kusema nafuu bunge la wakati wa Nyerere japo lilikuwa la chama kimoja lakini lilikuwa na UHURU wa mawazo na fikra,mbunge alikuwa akitoa shilingi waziri mkuu lazima aanze kutetemeka leo mbunge analalama mwisho wa siku anaunga mkono hoja,je mtu huyu anauhuru wa mawazo yake?Anauhuru wa anachokipigania?Au anaogopa kesho yangu sitapewa nafasi ya kugombea ubunge,mbunge huyu anaangalia maslahi yake kwanza na ya taifa baadaye na mbunge huyu anataka tumuite MUHESHIMIWA,tuambiane ukweli uheshimiwa wake ni upi?Wa kuvaa suti na kupanda VX au V8?

Mbunge anayehoji serikali anaonekana ni msaliti tuone alichosema Deo Filikunjombe je siyo kweli kwamba serikali IMEVAA MIWANI YA MBAO na KUZIBA masikio isisikie?Hivi Spika alikuwa anahaja ya kusema futa kauli yako?Kuna ubaya gani kutumia neno hili la picha kuionyesha ni kiasi gani serikali haioni inachotenda.

Bunge litarudi tu kwenye nafasi yake ya UTAKATIFU mpaka pale kiti cha SPIKA kitakapoona hakitendei haki watanzania na atakapojiuzulu wadhifa huo kwa hiari bila shuruti.

Na kutokana na udhaifu wa spika ili wabunge wa upinzani wauonyeshe umma kuwa wanaonewa ndiyo Matsusi,kashfa na lugha mbovu zinatumika kwa upande wao.

Tumuombe spika na hasa waandishi wahabari ni muda huu mnatakiwa kufanya kazi ya ziada andikeni,andikeni,andikeni udhaifu wa kiti cha spika ili turudishe imani kwa bunge letu.

Pasco na team yako ya waandishi anzeni sasa kulinusuru bunge kwa kuandika na kuandika msichoke watanzania wenye nia njema tupo nyuma yenu.
 
Simple solution Spika asitokane na Chama chochote ile aweze kusimamia kanuni bila kuona haya, maana tatizo ni Spika na Naibu Spika na Wenyeviti. thanks again Tetty sikua nimesoma maelezo yako nimekua kama nimekopi na kupaste.
 
Tatizo ni kujaribu kuzuia hoja za upinzani kwa jazba Nkamia alitumia lugha chafu na huyu kinda (no! sorry Ni kwa wingi) Makinda anajibu hoja kwa maandishi ya kwenye kanga badala ya kutumia kanuni za Bunge eti mkuki kwa nguruwe......? kama yeye hafati utaratibu wapi wengine waige? Kweli Msingwa upo sawa Akili ndogo ikitawala akili kubwa tatizo lazima liwepo! ndo kama ulivyosema Ilboru ccm ni wakubwa mno kiasi kwamba hata usipokua na shabaha hatuwezi kuwakosa 2015.
 
Bunge hili wamejaa walanguzi kama kina john komba,mwigulu nchemba, kigwangala, edward lowassa na hata habib mnyaa! Kazi yao ni kwenda kuwahonga wananchi wakati wa uchaguzi kwa kuwapa vitenge,kanga na hata vipesa ili kuwarubuni wawapigie kura, bunge hili halina la maana zaidi ya mipasho na kusinzia!
 
Analaaniwa akiukae ilyo Haki machoni pa walio haki
 
wananchi anaopiga kura sidhani kama watafanya makosa kurudisha vichaa wa cdm bungeni.
Coz hawana tija, sidhani 2015 idadi yao itazidi watano.

miccm bwana hakili hakuna kabisaaa!
Utaniambia nini kwa maovu ya ccm na mawaziri wake?
Hata kama ukisema ni freemasons afadhali hao,
hata ukiwaita magaidi hao ndo wakombozi wa nchi hii.
Kaa na mijambazi yako!
 
Mkuu post yako inaonyesha jinsi ulivyoguswa na ili suala,ila kuna w.a.p.u.m.b.a.v.u wengine wanataka kuleta siasa kwenye jambo la msingi,kwa ili la leo,hawa jamaha hawastahili kuitwa waheshimiwa hata kidogo,utamheshimu mtu vp kama yeye mwenyewe hajiheshimu?ila kiti cha spika ndio chanzo cha yote hayo,haya ndio madhara ya kua na spika aliyewekwa na watu wachache wakati hana uwezo
Root cause analysis start here............Then clearly show your Problem Tree..........After that Objective tree will come....................>>>>>>>>>>>>plan of Interventions.
 
Acha wanafunz wachore mazombi maana baba zao na mama zao walio bungen nao wanaongea kama mazombi
 
CCM College Ihemi
Mbigili Primary School

[TH="colspan: 5, align: left"] kwa wale wanaohoji haya matusi na utovu wa nidhamu wa wabunge unasababishwa na nini, ambao wanataka majibu tembeleeni tovuti ya bunge wwww.parliament.go.tz au kwa kucheck elimu ya mwenye matusi yasiyochujwa ndg Lusinde wa mtera ni,Parliament of Tanzania ambapo nimekopi kipande cha elimu na uzoefu tu nikaanza kucheka saaana. halafu leo anataka kuwekwa kwenye kamati za bunge duuuh!!!!

EDUCATION
[/TH]

[TH="width: 35%"] School Name/Location [/TH]
[TH="width: 27%"] Course/Degree/Award [/TH]
[TH="width: 15%, align: center"] Start Date [/TH]
[TH="width: 13%, align: center"] End Date [/TH]
[TH="width: 10%, align: center"] Level [/TH]

[TD="align: center"]Certificate[/TD]
[TD="align: center"]2007[/TD]
[TD="align: center"]2008[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]

[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1980[/TD]
[TD="align: center"]1987[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
Company Name
The Parliament of TanzaniaMember - Mtera Constituency

[TH="colspan: 4, align: left"] EMPLOYMENT HISTORY [/TH]

[TH="align: center"] Position [/TH]
[TH="align: center"] From [/TH]
[TH="align: center"] To [/TH]

[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]
Chama Cha Mapinduzi, CCMSecretary - Tarime District
Chama Cha Mapinduzi, CCMAssistant Secretary/Accountant
CHADEMAMember - National Executive Board
Civic United Front, CUFSecretary - Kawe Constituency
Chama Cha Mapinduzi, CCMSecretary

[TH="colspan: 4, align: left"] POLITICAL EXPERIENCE [/TH]

[TH="class: text_menu, width: 47%"]Ministry/Political Party/Location [/TH]
[TH="class: text_menu, width: 31%, align: center"]Position [/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]

[TD="align: center"]2006[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]

[TD="align: center"]2006[/TD]
[TD="align: center"]2007[/TD]

[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"][/TD]

[TD="align: center"]1992[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]

[TD="align: center"][/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[h=3][/h]
 
Back
Top Bottom