Ni wazi Kwamba Bunge Letu sasa Limechoka, wabunge wameshajikatia tamaa masikini hawa, kuwasukumiza wabunge wetu hawa hasa wa Chama Tawala mpaka hiyo 2015, ni kuwaonea tu Na kuwalazimishia Zigo zito lililowashinda. Hata Kwenye mchezo wa Soka, wachezaji wakichoka hawaweza kupiga makelele TUMECHOKAAAA!! Bali ninyi mnaotazama soka mtawatambua tu Na kumshauri kocha awaengue.
Bunge hili limechoka mbaya, 72% ya wabunge Ni watoro wa vikao hivi Na wachache waliobaki wanabwatuka matusi ya nguoni kila siju, imagine mbunge mweshimiwa anadiriki kutamka mbele ya Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano Wa TANZANIA tusi "CAMMON F U C K YOU!!" (Mods tafadhali msiedit tusi hili ni HANSARD KAMILI YA BINGE LETU", ).. Bunge limeshajichokea tulinusuru Kwa kulivunja.
KATIBA ya JMT, ibara ya 90, haituzungumzii kabisa sisi wananchi tuliolisimika Bunge kuwa Na mandate ya kuliwajibisha. Michezo ya Bunge Na RAIS, RAIS Na Bunge ndiyo pekee inayoweza kulivunja Bunge lakini sisi raia tuliolisimika Bunge hatumo kabisa, sasa nauliza wadau, Bunge ndio hiloo limeshajichokea , RAIS wetu Kama mnavyomjua keshasinzia zake, Hana meno at all Kwa hali hii, tumebaki wenyewe, matusi kila kukicha, ubabe bungeni Live unazidi, Wabunge wamemeza mashine Za kuzalisha uongo.. TUTALIVUNJAJE BUNGE HILI!!??!?