ukitaka kuona ukomavu na busara, angalia urafiki kati ya Halima Mdee na Esther Bulaya. Hawa wako vyama pinzani lakini kila mmoja anaweka mbele maslahi ya watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao. Bila shaka hii inawapa upeo katika kutoa michango katika kuisaidia serikari yetu.
Hivyo hata hapa jamii forum, tunahitaji kutoa michango yenye ukweli kwa maslahi ya nchi.
Mkuu njia panda ikiwa huna jambo lako la kuchangia ni bora ukabaki kimya badala ya kutoa mchango hasi ili mradi uonekane itikadi yako ni ipi.
Wafikirie watanzania wengine wanaokosa huduma ilhali maisha yao yanazidi kuwa magumu, lakini wewe huoni hilo mkuu.
Hata hivyo pongezi kwa uaminifu unaoonyesha kwa wale wanaokutuma.
Una adabu kama ya mbwa aliyezoezwa.