Bungeni Live: June 28, 2012

Unafikiria kama pinda....je nikikuambia TULIVYO MUELEWA SISI??? Kwa kuwa alishajua kwa MUDA ule tayari Ulimboka keshakufa....then mkija kujua watz lolote na liwe
 
Tamkoa la serikali la Waswahili walisema "litakalo kuwa na liwe", limeyayuka leo bungeni nadhani wanapima upepo wazee wa ni upepo tuu utapita.
 
Chadema kama chama cha upinza kitoe mwongozo nini tufanye watanzania maana dungu zetu wanaendelea kufua kwa mgomo wa madaktari ambao kimsingi wana madai yao ya msingi kabisa...
 
Ha ha ha haaaa...leo imekuwa 'misquote'? Jana mlikuwa mnatamba hapa sijui 'wanatimuliwa wote liwalo na liwe, oooh watafutiwa leseni liwalo na liwe'...leo imekuwa misquote!?

Mkuu wameshikika hawana ujanja !
 

Hapo pekundu, kama ni kweli,
Ina maana raisi anaishi wapi hadi 'arudi nchini mwake'?
 
Tena wamwangalie kweli kweli maana anaweza kuja na zile sumu zao walizo mpaka mwakyembe na Mwandosya.....
 
Can they come up with a new "line" please??!! ...si waliyasema haya haya kipindi cha mgomo uliopita?!
 
Mtoto wa mkulima pinda hakuna kitu usaniiii mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umenena vyema...hali itakuwa tete zaidi kama juhudi za haraka hazitachukuliwa ...na juhudi hizo ziwe za kumaliza matatizo yanayoikumba sekta ya afya..
 
Leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mh Lissu amemtaka Waziri mkuu ajipime na aone kama kweli anastahili kuendelea na nafasi yake ya uwaziri mkuu ama lah.
Hii imekuja baada ya Lissu kumwuliza mbona ahadi zake alizotoa juu ya sakata la madaktari kushindwa kuzitimiza?
Waziri mkuu akajibu kwamba ameshafanya the best kupambana na na swala hilo.
Mhe Lissu akamwambia kama ndiyo umeshafanya the best na bado Madaktari wameanza mgomo huoni ni wakati muafaka wa wewe kujiudhuru.
Mwishowe Waziri mkuu akatetewa na Madam Speaker.
 


Nakubalina na mpango huu wa kuwasaidia wagonjwa kwa wakati huu wa dharura. Shida yangu kubwa ni ufanisi wa hao madaktari wanaoazimwa.

Nijuavyo mimi hao madaktari wanaoazimwa yaani waliostafu, walioko wizarani na pengine na akina mbunge Kigangwara na wengineo kama Dr. Husein Mwinyi kama hawa-practice kwa muda fulani labda zaidi ya miaka 3 na kuendelea mambo haya ya ujuzi yanaanza kupotea/kusahaulika kichwani. Yes unakuwa bado unazo ideas za skills na knowledge but to be effective unahitaji kujikumbusha tena (refreshed).

Sasa swali langu ni Je hao wanaoletwa wastaafu na wa kutoka wizarani (hasa hawa - maana waliachaga siku nyingi ku-practice; kazi wanayo fanya ni ya kisera zaidi - paper works kuliko profession yao - dawa, muscles, diagnosis, nerves, ligaments, tendons and their specific names, surgery, n.k) watapewa muda wa kuwa refresh? Najua ni wataalam kabisa but to my opinion wanahitaji kujikumbusha tena!!!
 
Jenresta Mhagama anabwabwaja utumbo saa hizi. Kila kitu cha magambaz anaunga mkono
 
Hiyo keli mkuu panahitaji watu watakao jali utu na usawa katika jamii ya Ki-Tz. Yanayotokea sasa ni matokeo ya serikali yetu kufanya kazi kwa mazoea ya miaka za sabini. Tubadilike na tuone mahitaji mapya ya kutawala kizazi hizi kinachoona mbali.
 
bensonlifua92 nakubaliana na hoja yako kabisa.
Mgomo uliopita hao walioko wizarani pamoja na taasisi nyengine waliazimwa lakini bado haikusaidia kurejesha huduma katika hali yake ya kawaida.
Hata kama wataongeza na wastaafu bado hawatatosheleza mahitaji ya huduma katika hospitali zilizokumbwa na mgomo.
Pia tunakumbuka katika mgomo uliopita tulielezwa kwamba wanajeshi waliokuwa wakisaidia kuokoa jahazi muhimbili walikuwa wanalipwa posho kubwa sana lakini bado hawakuweza kukidhi viwango vya waliokuwa wamegoma.

Jambo la msingi hapa kama kweli serikali yetu inakubali kushaurika, ni kukaa kwenye meza ya mazungumzo na madaktari kwa moyo mmoja na nia moja ya kutaka kuumaliza mgogoro huu kwa maslahi ya wananchi wanyonge. Inaweza isitimize mahitaji yote kwa mara moja wakati huu lakini inaweza kutekeleza baadhi ya madai ambayo ni lazima kutekelezwa wakati huu hasa la call allowance, risky allowance, mishahara ikaongezwa kidogo (hata nusu ya wanachoomba). Naamini wakifanya hivyo madaktari hawatakuwa na sababu yoyote ya kutorejea kazini.
Tatizo kubwa lililopo sasa ni kwamba serikali imekuwa ikiahidi tu bila kutekeleza, na hapo ndipo madaktari wanakosa imani nayo hadi wakaamua kugoma. Serikali ikiendelea kupiga siasa hizi za majitaka katika suala muhimu kama hili linalogusa uhai wa watu moja kwa moja, isije kutafuta kisingizio chochote itakapotokea wananchi wamechukua hatua kali ambazo hakuna aliyewahi kufikia kama inaweza kutokea hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…