Bungeni Live: June 19, 2012

Silivester Mabumba naona ameamua kujibu hoja- sijui amejiona yeye ndiyo serikali?
 
Limesemwa na mbunge wa CCM Sylvester Mabumba kwa maana hiyo ni wazi mipango ya aerikali ni ya kiopen university
 
Naibu spika amwomba afute kauli ya kumwita Lusinde Chizi
 
Naibu spika: Onyo kwa msigwa, naomba wananchi wa iringa mjini kupitia mchungaji msigwa awe na nidhamu, nakuonya msigwa USIROPOKE.
 
Lusinde katoa point mbili muhimu:

1) Unafiki wa mbowe kuchukua posho, na kutumia gari la upinzani wakati alilikataa
2) Bajeti ya upinzani haiakisi ilani ya chama chao, mbona hawaoni elimu bure kwenye bajeti ya chadema?

Itaakisi vp wakati hawajashika dola?wapeni dola halafu ndo u challenge, JK zile zake keshatekeleza ngapi hadi sasa hivi?
 
Mnyika hana point, anabwabwaja tu bungeni. anajitetea eti mtwara kuna shida ya maji kuliko ubungo, anajitetea kupata msamaha wa wananchi wa jimbo lake
 
Mnyika ni noooooma!....Lusinde kapewa za uso.
Sasa anachangia.....
 
Nashauri serikali iweke kiwango cha elimu, cha mtu kugombea ubunge, Mnyika anaaibisha bunge
 
Mnyika anatoka nje ya mada jamani, mbona hachangii bajeti? Inatia aibu sana.
 

Red: Mkuu kwa vile serikali haijafanya improvement katika maeneo iliyoyaahidi kufanya vizuri ni sahihi kwa Mh Zitto kurudia kuikumbusha tena serikali maeneo hayo. Zitto ni mtu makini sana ieleweke.

Namsifu Lusinde kwa kuikumbusha serikali iangalie maeneo ambayo yalipata bahati mbaya ya kutokuwa na viongozi mara baada ya uhuru na hivyo kuwa nyuma kimaendeleo hadi leo. This is a good point ingawaje kwa masikitiko yangu Mh Ritha Mlaki hakumuelewa Mh Lusinde. Mlaki ameendelea kujigamba kuwa anaishukuru serikali kwa kujenga barabara za rami vichochoroni kule kwao!!
 
Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu: Namkumbusha mnyika na wabunge wa aina hiyo, hapa ni bungeni sio magengeni, Kanuni ya 64, mbunge wa aina yoyote hatatumia jina la rais kwa dhihaka katika mjadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…