Bungeni: Kamati ya kuchunguza tuhuma za rushwa yaundwa

ELFU-ONEIR

Senior Member
Jun 27, 2012
181
64
Kamati ya bunge ya kuchunguza tuhuma za rushwa zilizowapata wabunge imeundwa na mh spika leo mjini dodoma

hii ni kwa hisani ya twitter account ya mh. zitto

zitto zuberi kabwe speaker has just announced a probe team to investigate the corruption allegations against members of parliament. Credible team members....

zitto zuberi kabwe
probe team to be headed by brig. Gen ngwilizi, chiligati, arfi, blandes and bi. Riziki. 3 ccm, 1 cdm and 1 cuf.
Wana JF nimekuwa nasikiliza taarifa ya habari ya CLOUDS FM saa 12 jioni nikasikia kwamba Spika Anna Makinda ameteua kamati ya wabunge watakaofanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge. Moja ya jina nililolisikia kwenye kamati hiyo ni Gozibert Blandes Mbunge wa Karagwe, Nilijiuliza kama bunge limekosa watu wasio na doa kuwapo kwenye kamati ya uchunguzi.

Huyu bwana kwanza si mbunge harali, alitangazwa mshindi mbele ya mtutu wa bunduki, askari walitumwa toka Bukoba mjini kwenda karagwe kuwatisha wananchi waliokuwa wanasubiri matokeo ya uchaguzi. Alisindikizwa na askari mpaka airport Bukoba na sasa hivi hawezi kukanyaga huko wananchi wana hasira naye. Sasa mtu kama huyu anatoa wapi moral authority ya kwenda kuwahoji watuhumiwa wakati yeye ni mtuhumiwa wa vote rigging?

Nawakilisha.

 
Hakuna jipya kamati ngapi zimeundwa na hakuna lolote linalotusaidia sisi wananchi?
 
nchi hii tume kibao zimeundwa hakuna majibu wala cha maana zaidi ya kuongeza mzigo kwa taifa
 
hizi kamati toka zianze kuundwa zina faida gani? zaidi ya kula posho tu? upuuzi mtupu...........




 
Hata kama wakileta majibu watakuambia tukiisoma yote itayumbisha serikali ie Richmond
 
Allowance ni 4Mil per day msichekelee tu ni kiziba mdomo na hakuna kitakachofanyika. Watakumbushana tu "Unakumbuka ule mzigo niliokutumia mwezi wa 4? Nusu ilikua mgao wa hili jambo unaloniulizia".......

Taarifa: Hakuna ufa wa RUSHWA! Tanzania kama kahaba, haina msimamo hata kidogo.
 
Hii ni kwa hisani ya twitter account ya Mh. Zitto

Zitto Zuberi Kabwe 1h Speaker has just announced a probe team to investigate the corruption allegations against members of Parliament. Credible Team Members....

Zitto Zuberi Kabwe 1h
Probe team to be headed by Brig. Gen Ngwilizi, Chiligati, Arfi, Blandes and Bi. Riziki. 3 CCM, 1 CDM and 1 CUF.
 
Ofcoz lissu ni mmoja kati ya watakao hojiwa na kamati hio kwahio anahusika sana hasa ukizingatia aliwataja baadhi ya wabunge na madam amesema nayeye ahojiwe

mkuu,
sasa mbona huleti taarifa kwa undani badala yake umeweka picha ya lissu.yale yale ya watu kudaiwa hati za muungano wanakataa na badala yake wanaleta picha za nyerere na karume.tusiwe dhaifu kama serikali ya ccm tena.
 
Huu ni ufinyu wa mawazo sana. Tunaunda tume kuchunguza tukio badala ya tume kuchunguza weakness ya mfumo (chanzo) unaosabibisha mazingira ya matukio kama haya. Ndo maana kila mara zinaundwa tume ili wa-tz tuone kuwa hatua zimechukuliwa, tukishasahau hata ripoti hatutaijua wa kuihoji, then linatokea tukio jingine inaundwa tume tena. Ovyo kabisa. Isije ikatokea wajumbe wa hii tume nao wakapokea rushwa ili kupotosha ukweli?
 
Back
Top Bottom