''Wanatafutwa''Wanasakwa''hizo kauli zenu zinaonyesha jinsi mlivyo wanafiki!!nikiwaagizia walipo mtawafuata??au mtaendelea kuwasaka mukiwa mmekaa hapo hapo?haya basi wapo pale magogoni,mkifika muulizeni jamaa mmoja anaitwa jk ndiye amewaficha humo ndani kwake.
Siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.'
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine
HALI bado tete ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea mjini Dodoma kufuatia madai ya kuwepo kwa wabunge waliokula mlungula ili kuitetea ajira ya Bosi Mkuu wa Shirika la Ugavi Tanzania (Tanesco), William Mhando ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.
Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama vya siasa wanapiga ndogondogo ili waheshimiwa wanaotuhumiwa kupokea kitu kidogo wabatilishiwe ubunge wao na serikali iitishe chaguzi ndogo ili kuziba nafasi zao.
Unajua tatizo kubwa ni kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaojiona wasafi na wapo viongozi wa siasa wanataka wabunge wenye kashfa watimuliwe na kwenye majimbo yao kuitishwe chaguzi ndogo.
Hawa viongozi wa siasa (baadhi) ni wale ambao wabunge wao waliotuhumiwa ni tishio kwa maslahi yao ndiyo maana wanataka wangoke, lakini uchunguzi umeanza, sijui kama kuna atakayepona, alisema mbunge mmoja wa kutoka mkoa wa Arusha.
Awali majina ya wabunge hao yalikuwa siri, lakini juzikati, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu (Chadema-Singida Mashariki) aliwafungukia waheshimiwa hao kwa majina.
Lissu aliwataja Christopher ole Sendeka, Sarah Msafiri, Yusuf Nassir, Charles Mwaijage, Mariam Kisangi, Vicky Kamata na Munde Tambwe ambao wote walikuwa kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjiliwa mbali na Spika wa Bunge, Mh. Anna Semamba Makinda.
Hata hivyo, kamati hiyo pia ilikuwa ikiundwa na Selemani Zedi (Mwenyekiti), Diana Chilolo (Makamu Mw/kiti), Haji Khamis, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Dr. Festus Limbu, Athuman Mfutakamba na Lucy Mayenga.
Wengine ni Josephine Changula, Mwanamrisho Taratibu, Suleiman Nchambi, Ally Mbarouk Salim, Kisyeri Chambiri na John Mnyika.
Tayari Kamati ya Maadili, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imeanza kufanya uchunguzi kama madai hayo yana ukweli wowote. Ikithibitika, ina maana hakuna atakayepona
Thubutu, watapona tena wote, wangekuwa wa cdm siku hiyohiyo yangetimia, lakini hawa magamba watalindana hadi mwisho, ukizingatia na vcky kamata yupo kwa hiyo list, kitashuka tu ki memo kutoka hapo magogoni na picha ndo litakuwa limeisha
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.