Bungeni: Jesca Kishoa ahoji kwanini mikataba haiwekwi wazi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge Jesca David Kishoa amehoji kwanini Mikataba haiwekwi wazi akisema kufanya hivyo kuna faida mbalimbali ikiwemo kujenga uaminifu kati ya Wananchi na Serikali.

Amesema hayo Bungeni Dodoma na kuongeza kuwa, Serikali inapaswa kuweka akilini kwamba Rasilimali za Tanzania ni za Wananchi na Serikali ni wasimamizi.

Ameeleza, "Nchi nyingi zimeshafanya hivyo, sisi tunafeli wapi? Kwanini tunashindwa kuweka Mikataba yetu wazi? Waziri atuambie ni lini Nchi yetu itaanza kutekeleza rasmi Sheria ambayo tuliyotunga wenyewe".
 
Wakijua wapinzani nishida, wao sio sehemu ya serikali.

Hawanajema na Tz.
 
Mikataba ni nyenzo ya ushindani katika biashara huwezi tu kuweka wazi kwa kila mtu.Ndio maana wanaosimamia wanaapa kitotoa siri.Ukiweka mambo wazi serikali za nchi nyingine zitatumia taarifa hizo kukukabili kiushindani.
 
Huyu mbunge ni mjinga sana, ninachofahamu ni kwamba Kamati zote za Bunge hupata fursa ya kupitia mikataba husika kwenye sekta ambayo kamati inasimamia pia kuna Kamati ya kudumu ya Sheria na Katiba, hii pia hupelekewa Mikataba yote inayosainiwa na serikali na wawekezaji sasa huyu anapokuwa anaongea hivyo anakuwa anadanganya wananchi ili iweje?
 
Anazungumzia sheria namba 23 ya 2015
Screenshot_2021-05-01-01-06-28.png
 
Mikataba ni nyenzo ya ushindani katika biashara huwezi tu kuweka wazi kwa kila mtu.Ndio maana wanaosimamia wanaapa kitotoa siri.Ukiweka mambo wazi serikali za nchi nyingine zitatumia taarifa hizo kukukabili kiushindani.
Acha uongo mbona kampuni za simu zikiandaa product mpya huwa inapita TCRA kabla haijaruhusiwa ku launch. Kwani TCRA hawatoharibu ushindani maana wanaona business strategy za makampuni?

Kama TCRA ni sawa kwanini bunge iwe ni tatizo? Mlipitisha sheria za transparency 2015 ili iweje
 
Back
Top Bottom