Serikali yasema itaweka wazi mikataba ya Madini na Nishati kama itahitajika

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,352
8,033
Serikali ya Tanzania imeshindwa kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu mikataba ya madini kuingizwa bungeni ili ijadiliwe kabla ya kuingia makubaliano na wawekezaji.

Ni hoja ya muda mrefu ya wabunge wakitaka mikataba hiyo iwe inaruhusiwa kupelekwa kwa wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kwa lengo la kuweka uwazi.

Leo Jumatatu, Septemba 19, 2022, Mbunge wa Bahi (CCM), Kenneth Nollo ameibana Serikali akihoji ni lini Serikali itaanza kupeleka mikataba ya madini na nishati ijadiliwe bungeni ndipo waingie makubaliano na Wawekezaji.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda ameliambia Bunge leo kuwa mara nyingi mikataba hiyo hupelekwa kwenye kamati za Bunge kama itahitajika na huko hutolewa ushauri.

“Lakini Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia Sura ya 450 (5) inatoa wajibu wa Bunge ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Bunge katika utekelezaji wa jukumu lake linaweza kuitisha mikataba inayohusu masuala ya Utajiri na Rasilimali za Nchi,” amesema Pinda.

Naibu Waziri amesema takwa hili la sheria linazingatia misingi iliyowekwa na sheria kwamba mikataba au makubaliano yaliyoingiwa kati ya Serikali na wawekezaji yanazingatia haki, usawa na nia njema kwa pande zote na kuzingatia maslahi ya wananchi wa Tanzania.
 
Hiyo mikataba imekuwa ikihitajika muda wote wala asiseme ikihitajika. Ila kwa sasa kwakuwa ni bunge la chama kimoja hakuna maana yoyote wakiipeleka.
 
Back
Top Bottom