Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Ni sawa wabunge hao kutaka iwe hivyo, na wana haki ya kuogopa, sana tu.

Wamekuwa wanafanya mambo ya ajabu na ya OVYO sana. Uwakilishi wa wananchi wa majimbo yao ambao ndio msingi wa kuwepo kwao bungeni hawaufanyi badala yake wamekuwa sehemu ya genge la mafisadi ambao pia ndio wamiliki wa serikali ya JK. Kwa hiyo dhamira zao zimewasuta na wamejiona wako uchi, cha kusikitisha badala watubu na kubadilika wanataka kujificha kwa kubaki gizani.

Huo uthubutu wa kutoa hoja mbovu kama hiyo unaonesha kiwango cha ulevi wa madaraka na umaututi wa uongozi wa ccm.
 
Mkuu wewe ndio uwa mtu wa kwanza kuripoti kwa mods nashangaa unavyokuwa mnafiki kwa kauli zako za kejeli...
Ritz kwa sasa umebakia peke yako kutetea upumbavu!...vp wenzio mbona walikimbia juu ya malipo, wewe umeridhika?
Au wewe Nape anakulipa malipo ya ziada kwa mlango wa nyuma?
 
Last edited by a moderator:
Limekuwa Jando hadi bunge lifanywe SIRI? daah..
Wenzetu kenya wanapiga hatua mbele,hata shughuli za mhimili mwingine (mahakama) ,kesi zinaanza kurusha live, sisi ndo tunakimbilia kuficha mambo zetu nyuma ya pazia,
 
Wafanyakazi na Wakulima washinde siku nzima wanakodoa macho kwenye runinga, Taifa letu litajengwa na nani? chapeni kazi wazalendo wenzangu msishabikie siasa zisizo na tija?
 
Apo najua Makind.a alifurahi mapengo yale yote nje. Wanataka wabane upinzani ili wafanye madudu yao vizuri. Wanazuia hili hawajui la mbele.
 
Ni kitu gani kinachokufanya utuhumu kuwa ni wabunge wa ccm? Bunge lote hilo si wa CCM wala Chadema ni wababishaji tu huo ndio ukweli wenyewe na ndio sababu zaidi ubishani hakuna kinachofanyika; kimsingi hao si wabunge ni makada wa vyama wabunge karibu 90% ni vituko tu hata kuchambua bajeti hawajui hata hao wa upinzani kusoma bajeti yao wenyewe iliwashinda sasa tutasema tuna wabunge?

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,

Tatizo la Pro-Chadema JF wengi wao ni unafiki hivi wabunge wa Chadema wana mchango gani kwa taifa zaidi ya maslahi ya binafsi wanachofanya CCM bungeni na Chadema wanafanya hivyo hivyo.

Kama posho wote wanachukuwa aliyepinga na ambaye achukui posho ni Zitto Kabwe peke yake, mikopo ya milioni 90 wabunge wote wamechukuwa hakuna Chadema wala CCM...sasa hivi angalia vikao vya bunge sasa hivi uone wabunge wa Chadema wapo watano tu.

Juzi wabunge wameongezewa mishahara pamoja na posho wabunge wote wamekubali bahati mbaya hata wananchi hawajaambiwa.
 
Last edited by a moderator:
Cha muhimu hapa ni kusubiri, watakao peleka hoja hiyo bungeni inabidi wananchi wawape adhabu ya kuto kuwachaguwa tena,kwani wanawanyima haki yao ya msingi ya kikatiba yAa kupata habari.

Kuna nini cha maana hadi bunge lisirushwe live? Wanatambika kule? Mambonge yote duniani yanaonyeshwa live, kila siku tunashuhudia mabunge ya rusia, uchina, usa, uk, kenya na uganda, iweje tanzania ndi iwe siri?
 
Kuna mikoa watu wana lipia ili kuangalia bunge maana ni zaidi ya ze komedi...
 
Mkuu chama,

Tatizo la Pro-Chadema JF wengi wao ni unafiki hivi wabunge wa Chadema wana mchango gani kwa taifa zaidi ya maslahi ya binafsi wanachofanya CCM bungeni na Chadema wanafanya hivyo hivyo.

Kama posho wote wanachukuwa aliyepinga na ambaye achukui posho ni Zitto Kabwe peke yake, mikopo ya milioni 90 wabunge wote wamechukuwa hakuna Chadema wala CCM...sasa hivi angalia vikao vya bunge sasa hivi uone wabunge wa Chadema wapo watano tu.

Juzi wabunge wameongezewa mishahara pamoja na posho wabunge wote wamekubali bahati mbaya hata wananchi hawajaambiwa.

Mkuu Ritz
Tatizo ya pro Chadema ni wapigania uhuru wamesahau uhuru tulishaupata, wanafurahisha kila baya ni wabunge wa CCM tu lakini wengi wa hawa pro Chadema sidhani kama hata wameshafika Dodoma jamaa hawa wabunge baada ya bunge wote lao moja tu ukipata nafasi ya kuongea nao unaweza kuwashangaa yaani wanachoongea mjengoni sivyo kabisa wanavyofanya lao moja tu sijawahi kusikia wabunge wa Chadema (-Zitto) wakisema posho zao zipelekwe kwenye zahanati za maeneo yao; wao wale kwanza wakishiba ndio wanaingia mjengoni kumwaga komedi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Upumbumvu nadhani unao wewe mie JF nimekuja peke yangu na na jenga hoja peke yangu, nyie Chadema-Kata hata mkija 10000 napambana na wote wewe kwani unalipwa kiasi gani Slaa? Halafu JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru ulivyokuwa kauzu eti kwa sasa nimebaki peke yangu unadhani JF wote ni mateka wa Chadema.
Hapa hoja ni watetea hoja za kipumbavu na siyo U-chadema na U-ccm... wewe unaonekana umebaki peke yako kati ya watetea upumbavu.....
 
Sasa waheshimiwa wabunge hoja imekubaliwa na sasa nitawahoji. Wanao sema NDIYO..NDIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO na wanaosema SIYO ...siyoo. Ndugu waheshimiwa wabunge waliosema NDIYO wameshinda. thithiem thiem thithiem thithiem eaaa rllllllll ..wanafiki hao! Hili ndo Bunge la Tanzania.
 
Haya bana, hata mkitaka kuingia humo bungeni mkiwa uchi ruksa. Nyie wasilisheni tu hoja binafsi ambayo nina uhakika itaungwa mkono kwa asilimia 100 kama kawaida.
 
Hapa hoja ni watetea hoja za kipumbavu na siyo U-chadema na U-ccm... wewe unaonekana umebaki peke yako kati ya watetea upumbavu.....

Haya nenda kwa Lema kachukuwe posho yako umeishatetea hoja Chadema-Kata kama wewe huna hoja gani zaidi ya upambe kwa Lema.
 
Ikipitishwa hiyo hoja watakuja na hoja la kufuta masafa ya TV'Z...wabunge wa ccm wamelewa madaraka.
 
Back
Top Bottom