Bunge lisaidie taifa na minyororo ya mafisadi

Hakuna wabunge wa kufanikisha Hilo.
Kwa MASLAHI ya Taifa, ni lazima bunge liwe na mchanganyiko wa wabunge kutoka vyama vyote. Wabunge wa chama kimoja pekee hawawezi kupinga wizi wa fedha za umma.
Hii ni kusema kwamba wanaoharibu uchaguzi kwa kuiba kura au kubadili matokeo, wanalihujumu taifa letu.
 
Salaam nyote Wana Jamii forums

Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge unatarajiwa kuanza tarehe 4 April 2023, ni Bunge la bajeti mambo mengi yatajadiliwa zikiwemo ripoti 16 za kamati za Bunge, Aidha ripoti ya CAG itawasilishwa Bungeni na Kujadiliwa.

Ombi langu kwenu wabunge tafadhari kwenye ripori ya CAG, pitieni ukurasa Kwa ukurasa, nukta Kwa nukta kubaini madudu yote yaliyoibuliwa na ofisi ya CAG, toeni mapendekezo na hatua Kali dhidi ya wezi hawa na mafisadi waliowafunga Watanzania na minyororo ya kutafuna nchi na kudumaza maendeleo ya nchi, Bunge msaidie Rais Samia dhidi ya wanyanganyi hawa, Sheria zipo wazi, wezi hawa wawajibishwe bila kuangaliwa usoni, haiwezekani kundi la Watanzania Wachache waishi kama wafalme Kwa mgongo wa Watanzania maskini.

Bunge ni jumba lenye heshima yake, tumieni mamlaka mliyopewa Kwa mujibu wa Sheria kuwa wajibisha mafisadi wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG, Watanzania wanamaumivu wasaidieni tafadhari.
Nawasilisha.
Bunge hili hili kibogoyo la majizi ya kura?
 
Back
Top Bottom