Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,264
Huo mfumo tunaotumia sasa wa bunge zima na wabunge wote kujadili kila masuala hautupi tija na pia unaligharimu taifa bila umuhimu wote. Kama huu ndio mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola basi hauna tija kwetu inabidi tuachane nao tu.
Ilipaswa kuwe na kamati za kisekta za bunge kujadili na kusimamia masuala ya nchi na wabunge wagawanye huko kulingana na utaalamu na uzoefu wao. Sasa hivi unaweza kukuta mbunge anachangia ripoti ya CAG wakati hajui hata balance sheet ikoje au sheria ya manunuzi ya nchi inasemaje. Mtu anachangia sekta ya gesi akitokwa na povu na hajui chochote kuhusu biashara ya gesi, mwingine unakuta anotoka Kinondoni au Ilala na anachangia kwenye kilimo.
Bunge lingegawa kazi zake kwenye kamati, midahalo na usimamizi wote wa serikali ufanyike huko. Hata hiyo ripoti ya CAG ingejadiliwa na uamuzi kumalizika kwenye kamati ya wabunge wachache husika, sio kuita wabunge wote kuijadili wakati wengine wanataka waonekane live tu. Sasa hivi unaweza kukuta mambo CAG na ushoga yanajadiliwa katika kikao kimoja! Hii inakuwa shaghalabaghala tu.
Bunge zima likutane tu wakati wa kupitisha miswaada iliyotoka kwenye kamati na bajeti kuu, hii italeta tija ya mijadala na itasaidia sana na kubana matumizi.