Bunge linasaidia Wabunge kukwepa kodi. Jerry Silaa yupo sahihi kabisa!

Majizi yote haya vikao vya Bunge kwa mwaka havifiki hata miezi minne lakini angalia wanavyojilipa miezi mingine karibu 9 ambayo hawafanyi lolote zaidi ya kujibaraguza tu huku na kule.
Ndio maana wanatukata hela nyingi kwenye simu
 
Haya n pamoja na yale yanalalamikiwa kukosekana kwa usawa na ubaguzi katika jamii yetu.
 
Ninaunga mkono hoja ya kufanya marejeo/mapitio ya mshahara na marupurupu ya waheshimiwa Sana.
Hivi kwenye mshahara wao wanakatwa asilimia fulani kwa ajili ya mafao baada ya uwakilishi wao (ninasikia wanalipwa donge nono baada ya miaka 5) na matibabu yao na familia zao(ninasikia Wana package mzuri sana.

Ushauri
1).Wasaidizi wa wabunge ,isiwe suala la hiari,iwe ni lazima kila Mbunge awaajiri wasaidizi hao ña walipwe stahiki zao,(Kuna baadhi ya wasaidizi hususan madereva wanalialia njaa,hawalipwi kwa wakati).
2).Wasaidizi wa wabunge nao waingizwe kwenye mifuko ya pensheni ya uzeeni na bima ya afya.
3).Kama waheshimiwa Sana hawachangii mifuko ya pension na bima ya afya ,ni busara na wao (kwa hiari yao wapeleke mswaada wa dharura bungeni kwenye kikao kinachofuata wafanye marekebisho sheria,kanuni na taratibu za bunge) waanze kuchangia mifuko hiyo. (Waheshimiwa wetu,waone fahari kuchangia mifuko hii).
4).waheshimiwa Sana,ikiwapendeza,wafanye marekebisho ya kanuni ili wasaidizi wao (katibu na dereva wa Mbunge) wawe waajiriwa wa kudumu wa ofisi ya bunge /halmashauri ili waweze kukidhi vigezo vya kulipwa pensheni (pawe na muendelezo wa ajira zao ) na ufanisi wa kazi badala ya kila Mbunge kuajiri katibu na dereva wake,Hii itasaidia kipindi cha kupokezana vijiti waheshimiwa Sana kuwe na muendelezo(continuity ) wa shughuli za ofisi ya Mbunge mafanikio na changamoto za Wananchi wa jimboni kwake.
 
Nionavyo, ni kweli Wabunge wakisaidiwa na ofisi ya Bunge, wanakwepa kodi. Wanatumia mtindo wa kizamani, wa kifisadi kukwepa kodi. Mshahara wa Mbunge milioni 2 plus, marupurupu ni zaidi ya milioni 8! Jumla yote milioni 11!


Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Aisee, Kama hiyo orodha ya posho ni kweli. Basi wabunge wetu ni wabinafsi sana kwa nchi hii.
 
Ndio maana wanaweka hayo matozo na Kodi ili kuendeleza wizi na unyonyaji. Hapa ndio tunapata ile logic kwanini watanzania wanaacha kazi zao za kitaalamu ili waingie bungeni kwa gharama yoyote hata kuua
 
Hili nalo ni gumu kulielewa. Yaani kweli Dereva wa Mbunge anaajiliwa na Mbunge, halafu malipo ya mfuko wa jamii nani analipa? Ni uhuni ndani ya nchi. Inafikia hatua Bunge ni chombo cha uhuni uhuni tu!
 
TRA walistahili kuomba kodi za waajiliwa wa Mbunge. Akiajili dereva lazima waombe kodi zao.
 
Hawa ni wakwepa kodi tu! Ni sawa na makampuni yanayopunguza mishara na kuongeza marupurupu ili walipe kodi kidogo serikalini. Bunge nalo hivyo hivyo tena kwa zaidi sana! Unawezaje kulia posho kubwa kuliko hata huo mshahara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…