Jerry Silaa weka hadharani salary slip yako kabla ya kuitikia wito wa kwenda kwenye kamati

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kama kusema kuwa wabunge hawalipi kodi ndio sababu ya wewe kuitwa kwenye Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, nakushauri uweke hadharani salary slip yako kabla ya kufika mbele ya kamati ili umma ujue ukweli halisi ni upi.

Unaweza kuficha taarifa ambazo sio sahihi kwenda kwenye public (mfano kiwango cha makato), ila ukaacha orodha ya makato unayokatwa ionekane ili tuone kama PAYE imo katika orodha hiyo.

Unaweza fanya hivyo kupitia mitandao mfano twitter na watu wakathibitisha maneno yako ili hata wakikusulubu,, basi umma utajua ni nani wa kumuhukumu.

Hata mliowahahi kuwa wabunge wa upinzani, mnaweza kuingilia swala hili na kueleza ukweli ni upi hata kama kweli mlikuwa hamkatwi kodi na hamkuwahi kuongea hadharani kama alivyofanya Jerry Silaa lengo tujue ukweli ni upi ila kwa ushahidi wa salary slip.

Vile vile, pamoja na taarifa ya Bunge kukanusha madai ya Jerry Silaa, nilitegemea Spika wa Bunge atoke hadharani na salary slip yake kuthibitisha uongo wa Mhe. Jerry Silaa ila hilo halikutokea na bila shaka halitatokea.
 
Msimdanganye Mwenzenu
Ana Familia Watu wenyewe nyie wabongo??? Hata Itokee nini mtaishia kuandika kwenye Clip basi
 
Lakini sheria ya income tax imetamka kuwa gratuity za wabunge ndio hazitakatwa kodi.

Mshahara wa rais ndio haukatwi kofi na marupurupu yake yote(which is upuuzi na ufisadi wa level ya juu sana).

Kama kuna mtu ana kifungu cha sheria ya kodi ambacho kinaexempt mshahara wa mbunge kutokatwa kodi aweke hapa kwa ufahamu..
Mbaya zaidi kwenye revised edition ya income tax ya 2019 kifungu cha exemption ya kodi ya gratuity ya mbunge kama kimetolewa.Hapa ndipo Jerry Slaa anaweza kubanwa
 
1629580312801.jpeg
 
Kama kusema kuwa wabunge hawalipi kodi ndio sababu ya wewe kuitwa kwenye Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, nakushauri uweke hadharani salary slip yako kabla ya kufika mbele ya kamati ili umma ujue ukweli halisi ni upi...
 
Back
Top Bottom