Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (paye) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa mitandaoni.


IMG_20210803_162352.jpg

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
 
Kutoka maktaba

15 Jun 2016

Kama mnatukata kodi mkateni hadi Rais '-Mbunge Hussein Bashe



Wakati mjadala wa kuijadili bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2917 mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe amesimama bungeni kusisitiza kama serikali imeamua kuwakata kodi wabunge basi ihakikishe inatekeleza hilo kwa viongozi wote bila kubagua.

source : Millard Ayo
 
Suala la kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha Wabunge

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Hon. Mussa Azzan Zungu

0.67804200%201485860446.png

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika: nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuunga mkono hoja naiomba Serikali i-revisit upya suala la kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha Wabunge. Nia njema ya Serikali ambayo ipo, lakini Serikali naiomba i-revisit. Kwa wastani Wabunge tunalipa kodi kwa miaka mitano tuko Bungeni hapa takribani milioni 50, inafika, I stand to be corrected kama utaweza kunirekebisha, lakini kwenye hesabu zangu tunalipa almost milioni 50 kwa miaka mitano ambayo tunakaa hapa Bungeni. Kwa hiyo, naomba Serikali wajaribu kuitazama hiyo upya.

Source : Bunge Polis
 
Wanadai wanalipa kodi stahiki halafu wanatutajia PAYE

Wabunge wanapata ‘benefits in kind’ kibao.

Mkopo ambao ni interest free (serikali inatakiwa idai walau asilimia tano ya huo mkopo kama kodi, sisi raia mikopo ya kununulia magari tunatozwa mpaka 15% interest).

Wanapata posho za vikao kila siku hazina kodi.

Afya yao bure kwa mwaka medical insurance yake ni sawa na mtu anaelipia kiwango cha juu wao wanapata bure, wanatakiwa walipe kodi walau asilimia 30 ya insurance costs kutoka mfukoni kwao.

Wengine wana biashara hizo ni income nje ya ajira wanatakiwa kulipa income tax.

Wengine wamewekeza wanapokea dividends za biashara and interests za bank savings ambazo awalipi kodi.

Sina uhakika ila nadhani wabunge wana pata hela za kuendeshea ofisi zao, wengine ofisi zenyewe zipo majumbani mwao na hazina ata wasaidizi so hela yote inawekwa mfukoni.

Sheria ya nchi inasema income ya zaidi millioni 100 kwa mwaka unatakiwa ulipe income tax.

Wabunge wanapata zaidi ya hiyo kwa mwaka ukijumlisha mishahara, marupupu yao ya vikao, mapato yao ya shughuli binafsi, medical insurance cover and other benefits in kind.

Sio kukamua wafanyabiashara wadogo na wakulima tu, wakati mabwanyenye yananyonya maskini huko bungeni.
 
2 Aug 2021
EXCLUSIVE NDANI YA CLOUDSMEDIA
LIVE: 360 na (CAG) Ludovick Utouh Mstaafu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali | Wapi Tunaelekea. Ilipofika dakika ya 38 ya mahojiano amezungumzia kipato chote cha wabunge lazima kikatwe kodi
Source : CLOUDSMEDIA


Kubwa CPA Ludovick Utouh anasema - Msingi wa Kodi ni Usawa, kwamba wote walipe kodi kutokana na kipato ( hii inajumuisha mishahara, posho marupurupu n.k n.k

CAG Mstaafu, Ludovic Uttoh amesema hakuna sababu za kwanini Wabunge wa #Tanzania hawalipi Kodi licha ya kwamba wana Mishahara kama walivyo Watumishi wengine wanaokatwa Kodi.

Uttoh amesema "Siku zote msingi wa Kodi ni Usawa na wala kodi haitakiwi kuwa na Matabaka. Ikiwa tunasema tunalipa Kodi kwa maendeleo ya Nchi ni kwanini Wabunge hawakatwi?"

Akieleza zaidi, amesema hafahamu kama kuna Nchi nyingine Duniani ambayo Wabunge wake hawalipi kodi. Kwanza logic ya kufanya hivyo haipo".
Source : Ludovic Uttoh: Kama Kodi ni kwa maendeleo ya Nchi kwanini Wabunge hawakatwi wakati nao wanalipwa Mshahara kama wengine?
 
Kutoka maktaba

15 Jun 2016

Kama mnatukata kodi mkateni hadi Rais '-Mbunge Hussein Bashe



Wakati mjadala wa kuijadili bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2917 mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe amesimama bungeni kusisitiza kama serikali imeamua kuwakata kodi wabunge basi ihakikishe inatekeleza hilo kwa viongozi wote bila kubagua.

source : Millard Ayo

Huyu Bashe povu lote hili analitoa kwasabb sh milioni 3 (wameipa jina la mshahara ) kati ya milioni 12 ndiyo itakatwa Kodi. Wabunge wajanja Sana.
 
CAG Mstaafu, Ludovic Uttoh amesema hakuna sababu za kwanini Wabunge wa #Tanzania hawalipi Kodi licha ya kwamba wana Mishahara kama walivyo Watumishi wengine wanaokatwa Kodi.

Uttoh amesema "Siku zote msingi wa Kodi ni Usawa na wala kodi haitakiwi kuwa na Matabaka. Ikiwa tunasema tunalipa Kodi kwa maendeleo ya Nchi ni kwanini Wabunge hawakatwi?"

Akieleza zaidi, amesema hafahamu kama kuna Nchi nyingine Duniani ambayo Wabunge wake hawalipi kodi. Kwanza logic ya kufanya hivyo haipo".
Source : Ludovic Uttoh: Kama Kodi ni kwa maendeleo ya Nchi kwanini Wabunge hawakatwi wakati nao wanalipwa Mshahara kama wengine?
Ngoma inogile
 
3 Aug 2021

Lusinde: Awajibu wanaosema wabunge hawalipi kodi/ ataja mshahara wake hadharani


Mbunge wa Mvumi, Mh. Livingstone Lusinde amevunja ukimya na kutaja mshahara wake hadharani lakini akasema wanaotaka ubunge wasubiri 2021.

Lusinde ametoa Kauli alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amemtaja aliyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Ottouh kuwa anafanya mambo ya kukurupuka hivyo anadanganya Watanzania.

Mheshimiwa Livingstone Lusinde awasomea mapato ya kuwa mbunge mbele ya waandishi wa habari na kubainisha kilichoandikwa ktk salary slip yake:
  • Mshashara shs. 4,600,000
  • Kodi kwa mwezi shs. 1,210,500
  • Posho......?
  • Jimbo....?
  • Msaidizi ofisi .....?
  • Mafuta ya gari...?
  • Dereva...?
  • Mkopo wa gari ....?
  • Kodi ya nyumba Dodoma ....?
  • Bima ya afya ....?
Source : Mwananchi Digital

N. B
https://www.tra.go.tz › swahili › paye
Mamlaka ya Mapato Tanzania - Kodi ya Mapato yatokanayo na Ajira
Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.

Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?​


Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira
Mapato ya ajira yanahusisha;
a) malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
b) Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
c) malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
d) michango na malipo ya kustaafu
e) malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
f) malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
g) Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa

h) malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi


Mapato yasiyohusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira

Mapato yafuatayo hayatahusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira:
(a) Kiasi kilichosamehewa na malipo ya mwisho ya zuio;
(b) Huduma za kafeteria zinazotolewa bila ubaguzi;
(c) Huduma za afya, malipo ya huduma za afya na malipo ya bima kwa huduma za afya ikizingatiwa kwamba huduma au malipo hayo:
(i) Yanapatikana ili kukidhi matibabu ya mhusika, mwenza wake na hadi watoto wao wanne; na
(ii) yanawezeshwa kupatikana na mwajiri (na mtu yeyote anayehusiana na mwajiri anayeendesha biashara kama hiyo au inayohusiana na hiyo) katika misingi isiyo ya kiubaguzi;
(d) Posho yoyote ya kujikimu, safari, burudani au posho nyingine zinazohusisha urudishaji wa gharama kwa mnufaika kwa kiwango chochote alichotumia na kisichohusiana na uzalishaji wa kipato chake katika ajira au huduma inayotolewa;
(e) Faida inayotokana na matumizi ya chombo cha moto ambapo mwajiri hadai kufanya makato yoyote au nafuu kuhusiana na umiliki, matengenezo au uendeshaji wa chombo cha moto;
(f) Faida inayotokana na matumizi ya maeneo ya makazi kwa mwajiriwa wa serikali au taasisi nyingine ambayo bajeti yake haitokani na ruzuku inayotolewa na serikali;
(g) malipo ya safari kwa mwajiriwa, mwenza wake, na hadi watoto wanne kwenda na kurudi eneo la kazi, yanayoendana na gharama halisi za usafiri ikiwa mwajiriwa anaishi zaidi ya maili 20 kutoka katika kituo chake cha kazi na ameajiriwa kutoa huduma kwa mwajiri katika eneo la kazi;
(h) Mchango na malipo ya kustaafu yanayosamehewa chini ya sheria ya Huduma za jamii za Mafao ya Kustaafu
(i) Malipo yasiyokuwa na sababu za msingi au yasiyotekelezeka kiutawala kwa mwajiri kuyajengea hoja au kuelekeza kwa wanufaika wao;
(j) Posho inayolipwa kwa mwajiriwa anayetoa huduma binafsi ndani ya taasisi kwa wagonjwa katika hospitali za umma; na
(k) Posho ya nyumba, usafiri, uwajibikaji, kazi za ziada, kazi za muda wa ziada (ajari), mazingira magumu, na honoraria inayolipwa kwa waajiriwa wa serikali au taasisi, bajeti ambayo inalipwa yote au sehemu yake na ruzuku ya bajeti ya serikali
Source : Mamlaka ya Mapato Tanzania - Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?
 
Bunge acheni uongo onesheni hizo kodi wanazokata na siyo maneno mingi mingi .......
 
Wabunge wanakatwa kodi kwenye mishahara kama kawaida, hilo ni kweli.

Shida iko kwenye posho, wabunge wameweka mshahara mdogo wa 3m halafu wameweka posho nyingi karibu 9m ambazo hazikatwi kodi.

Lengo hasa la kuweka posho ama marupurupu mengine mengi ni kukwepa kodi. Posho halikatwi kodi.

Tunachotaka ni hizo posho zote ziingie kwenye mshahara ili ukatwe kodi.
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.



Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Hivi Hussein Bashe na Jerry Slaa siyo wabunge?? Walipata wapi hoja ya kuzungumza kwamba "na sisi wabunge tukatwe kodi"??
 
Mh. UTOH alikuwa CAG....

Kwa hiyo halijui hilo?

Yeye ni mjinga?

Tunakitetea chama kwa nguvu nyingi mno...

Waache mambo ya ajabu...

#KaziInaendelea
#SiempreCCM
#SiempreSSH
 
Wananchi wanazungumzia "milioni 9" za POSHO......

Ndani ya hizo posho ,kuna posho kwa ajili ya WASAIDIZI WAO 3....je wengi wao wanao hao wasaidizi 3?!!

Is it optional to recruit them?!!!

Kama hawana ,inakuwaje jasho la wananchi linavuja kuwapa fedha ISIYOTUMIKA?!!!

WABUNGE WAELEWE KUWA SISI VIJANA WA CHAMA TUNATUMIA NGUVU KUBWA KUKITETEA CHAMA.....wasituvunje mioyo.....

#KaziIendelee
#SiempreCCM
#SiempreSSH
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.



Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Hili limeshuhudiwa (testified) na wabunge wenyewe kuwa wao hawalipi kodi yoyote ktk mishahara yao. The latest reference ni mbunge wa Ukonga, Jerry Silas...

Huyu hawezi kuwa mwongo kwa kiwango hiki maana anaujua mshahara wake na huwa anaupata hivyo hivyo bila makato yoyote. Na tukumbuke huyu ni mbunge mzoefu wa muda mrefu...

Kama alisema uongo kwa wananchi huku akiwa kama mbunge, basi bunge limuwashibishe kwa mujibu wa kanuni zake...
 
Back
Top Bottom