Bunge letu si bunge tukufu

Bunge kama hili la Sitta unategemea liwe tukufu hata siku moja? We fikiria sasa hivi wabune wa CCM wanachofikiria ni namna gani watarudi bungeni mwakani et mbunge anauliza mbona waziri hujanitendea haki jimboni kwangu we hutaki nirudi mwakani?
Mwingine kaenda mbali hadi kumtuhumu mbunge waziri ambaye ni mwanamke mwenzakake, wewe Hawa mbona hututendei haki wanawake wenzio au hutaki turudi bungeni? Hapo kuna utukufu wowte kweli au ni kulitafuta maslahi na sasa wako katika hatihati za kutafuta kurudi kurudi 2010?
HAKUNA BUNGE TUKUFU HATA SIKU MOJA HAPO.......
 
Well me i am speechless coz honestly speaking sijapata hassa jina linalostahili kuitwa hili Bunge maana nahisi kuliita tukutu,butu mafisadi yooote mmelipendelea sana maaana mie nahisi kama bunge la mashetani ambalo halipendi wasiokuwa mashetani na wakigundua kuna binadamu , wanafanya ushetani wao ili kumuangamiza huyo binadamu
lakini itafika wakati dua zetu wananchi na vilio vyetu VITAMFIKIA MOLA WETU na hao mashetani wote wataangamizwa wabaki binadamu kwenye bunge letu. MUNGU TUKUBALIE DUA ZETU
 
Well me i am speechless coz honestly speaking sijapata hassa jina linalostahili kuitwa hili Bunge maana nahisi kuliita tukutu,butu mafisadi yooote mmelipendelea sana maaana mie nahisi kama bunge la mashetani ambalo halipendi wasiokuwa mashetani na wakigundua kuna binadamu , wanafanya ushetani wao ili kumuangamiza huyo binadamu
lakini itafika wakati dua zetu wananchi na vilio vyetu VITAMFIKIA MOLA WETU na hao mashetani wote wataangamizwa wabaki binadamu kwenye bunge letu. MUNGU TUKUBALIE DUA ZETU

Mungu husikia sala za waja wake na labda hivi karibuni atasikia dua na sala zetu kuhusu uozo uliokithiri ndani ya serikali yote likiwemo Bunge haramu.
 
Wabunge 'vijogoo' CCM sasa watishiwa kufukuzwa

Godfrey Dilunga Juni 24, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Wakutana kwa faragha, wasema tatizo ni Katiba

Waomba msaada wa wasomi kujiorodhesha waungane

WABUNGE machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioibua hoja kali dhidi ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010, wakionyesha kukerwa na ukwamaji wa baadhi ya mipango ya kuendeleza Taifa, wangekiona cha moto kama wangegoma kuipitisha, Raia Mwema limebaini.

Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizopatikana hapa, baadhi ya wabunge hao walilazimika kukutana kwa faragha, muda mfupi kabla ya kupitishwa kwa bajeti, kujadili mustakabali wao ndani ya wigo wa kitisho cha kuvuliwa uanachama wa CCM.

Uchunguzi umebaini kuwa miongoni mwa mambo yaliyowaweka wabunge hao katika hatari ya kufukuzwa CCM ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 71, kifungu kidogo cha ‘f’ ambacho kinaungana na ibara ya 90, kifungu cha ‘b’.


Vifungu hivyo ndivyo vilivyowatikisa wabunge hao hadi kufikia hatua ya kunywea, na hatimaye kubadili msimamo wao mkali ili bajeti ipitishwe na wao wabaki salama kwa ajili ya kupigania kile kinachoelezwa kuwa ni “kuichangamsha Serikali na mawaziri wa Rais Jakaya Kikwete.”

Wakati ibara ya 90, kifungu cha kwanza (b) katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikitoa maelekezo ya namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoweza kufikia hatua ya kulivunja Bunge, ibara ya 71 ya Katiba hiyo, inatoa maelekezo ya namna ya kumshughulikia mbunge anayetofautiana na chama chake.

Ibara ya 90 (2), ambayo ilitumiwa kuwatisha wabunge kabla ya kupitishwa Bajeti inaeleza: “Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa….(kifungu kidogo b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti iliyopendekezwa na Serikali.


Inaelezwa kuwa ibara hiyo ya 90, ambayo ilisomwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, dakika chache kabla ya Bunge kuingia katika hatua ya kupitisha au kutopitisha Bajeti ya Serikali, iliwatisha wabunge ambao uchunguzi umebaini kuwa wengi wao hawakujiandaa kurejea katika uchaguzi mara baada ya Bunge kuvunjwa wakati huu, kama bajeti isingepitishwa.

Wabunge walitishwa na kifungu hicho kutokana na ukweli huo kwamba hawakujiandaa kuingia katika uchaguzi mwaka huu, wengi wakiwa wamejianda ‘kibajeti’ kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani na wengine hali zao ni mbaya majimboni na wapo katika mpambano wa kujiweka sawa dhidi ya washindani wao watarajiwa.

Lakini wakati ibara hiyo ya 90 ikiwatisha wabunge wote, ibara ya 71 ya Katiba iliwaweka katika wakati mgumu zaidi wabunge ambao hawakuhofia sana ibara ya 90.

Ibara hiyo ya 71 iliyowatisha wabunge hao, wakiwamo Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii; Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe; Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro; Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na wengineo ambao hatimaye walinywea, inaeleza jinsi mbunge anavyoweza kusitishwa kuwa mbunge.

Ibara hiyo ya 70 (1) inaeleza; “Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo jambo lolote kati ya mambo yafuatayo;

Na hapo kifungu ‘f’, kinadakia kwa kueleza; “Iwapo mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.”

Raia Mwema lilizungumza na mmoja wa wabunge hao, Mpendazoe, ambaye katika maelezo yake alitoa dukuduku lake akisema Watanzania hawapaswi kuwashutumu wao; bali jambo la kukazania kwa sasa ni mabadiliko ya Katiba ambayo alisema imeweka wigo wa kulinda mfumo wa sasa ambao unainufaisha Serikali hata katika mambo yenye maslahi kwa Taifa.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, hali ingekuwa tete kwa upande wao endapo wangejitokeza wazi wazi kupinga bajeti kwa kupiga kura ya hapana kwa kuwa kufanya hivyo wangekuwa wanapingana na Rais Jakaya Kikwete.

Lakini mbali na kupingana na Rais Kikwete, pia Rais huyo huyo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, amepewa ‘mabavu’ na Katiba kuwafukuza katika CCM wakati mwingine bila hata uamuzi huo kujadiliwa katika vikao.


“Unajua tulikutana kujadili hili suala, tatizo la msingi ni Katiba. Katiba hairuhusu mtu asiye mwanachama wa chama cha siasa kuendelea kuwa mbunge kama atavuliwa uanachama huo.

“Sasa ni rahisi sana, kwa mfano, wabunge wachache wa CCM tungepinga bajeti na wengi wakaipitisha; maana yake tunampinga Rais …hilo si tatizo kumpinga Rais kwa manufaa ya Taifa, lakini tulikwenda mbali zaidi kutazama Katiba,” alisema.

“Tukabaini kuwa Katiba ina upungufu wa muda mrefu unaokwamisha mambo mengi kwa manufaa ya Taifa. Hebu fikiria, Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kwa kuzingatia kuwa Katiba haitaki mbunge asiye mwanachama, anaruhusiwa kwa utashi wake tu kumwandikia barua Spika wa Bunge kwamba mbunge fulani si tena mwanachama wa chama chake.


“Anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe kama mwenyekiti au kwa kumwagiza Katibu Mkuu wa chama tu. Kwa hiyo barua inapofika kwa Spika kutoka kwa mwenyekiti wa chama, Spika mara moja anatangaza Jimbo la Uchaguzi la mbunge husika kuwa wazi.

“Kwa hiyo, tukaona hayo yote tuyaache lakini utumike utaratibu mpya ndani ya kanuni zetu za Bunge wa kuwashirikisha wananchi na hasa wanasheria na wasomi maarufu vyuoni kuorodhesha majina yao na kisha kumkabidhi mbunge yeyote ili iletwe bungeni hoja ya mabadiliko ya Katiba,’ alisema mbunge huyo.

Kwa mujibu wa maelezo hayo ya kushirikisha wasomi na wanasheria, ruksa ya utaratibu huo inatolewa na kanuni za kudumu za Bunge, toleo la mwaka 2007, zilizotungwa chini ya ibara ya 89 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sura ya pili, toleo la 2002.

Kanuni inayotoa fursa hiyo katika kitabu hicho ni kanuni namba 34, kuanzia kifungu kidogo cha kwanza hadi cha tatu.

Inaeleza Kanuni hiyo: Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo, na ombi hilo halitawasilishwa bungeni mpaka kwanza taarifa ya ombi hilo iwe imetolewa kwa maandishi na na kupokewa na Katibu si chini ya siku mbili za kazi kabla ya mkutano ambamo ombi hilo linakusudiwa kuwasilishwa.

Kifungu cha pili cha kanuni hiyo ya 34 pia kinaeleza: “Ombi lolote linaweza kuwasilishwa bungeni na mbunge likionyesha jina la mbunge anayeliwasilisha.”

Kifungu cha tatu cha kanuni hiyo pia kinaeleza; “Mbunge anayewasilisha ombi atatoa maelezo mafupi ya kutambulisha watu wanaotoa ombi hilo, idadi yao, saini zilizoambatanishwa kwenye ombi hilo, madai ya msingi yaliyomo na madhumuni ya ombi hilo.”

Mbunge Mpendazoe aliendelea kusema: “Mimi nasema wananchi, na hasa wasomi wakiendelea kutegemea hiari ya serikali ili yafanyike mabadiliko ya Katiba, hiyo itakuwa ndoto isiyokamilika kwa sababu serikali inafaidika na udhaifu wa sasa wa Katiba.

“Kwa hiyo, kwa kuwa ni wazi sasa Katiba inalinda system iliyopo hata pale pasipostahili, ni vema wananchi wakasaidiana na wabunge na Bunge kama chombo chenye jukumu la kutunga Katiba ili kurekebisha mambo kwa maslahi ya Taifa.

“Wajiorodheshe wasomi katika vyuo vikuu, wanasheria na watu wengine hoja zipangwe kwa mtiririko maalumu, watie saini zao na kanuni za Bunge zitatumika, maana ya kuwapo kwa kanuni kama hiyo ya Bunge ni kwamba Bunge lipo kwa ajili ya matakwa ya wananchi na halina budi kutekeleza matakwa yao kwa manufaa ya Taifa zima na si kwa manufaa ya Serikali pekee,’ anasema mbunge huyo.

Alhamisi wiki iliyopita, Bajeti ya Serikali ya mwaka mpya wa fedha unaoanza mwezi ujao ilipitishwa kwa kupigiwa kura na wabunge, kama kawaida, kwa mtindo wa kila mmoja kuitwa jina na kutamka “ndiyo” kama anakubaliana nayo, “hapana” kama haikubali na “sina upande wowote” kama ataamua kutokuwa upande wa wanaoipinga au kuikubali.

Kutokana na mwenendo wa baadhi ya hoja za wabunge waliochangia katika mjadala wa bajeti, ilitarajiwa kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wangeipinga. Lakini ilikuwa kinyume chake; kwani wengi waliikubali huku baadhi wakiamua kutokuwamo ukumbini wakati wa upigaji kura, iwe kwa kutoa taarifa kwa Spika au la.

Hali hiyo imekuwa ikiibua malalamiko ya wananchi nchi nzima dhidi ya wabunge hao kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni unafiki wao na kuwa na misimamo inayoyumba, malalamiko ambayo yanaelekezwa kwa wabunge machachari wa CCM.

Wakati upande wa wabunge wa CCM ukiwa katika hali hiyo, wabunge wa Kambi ya Upinzani bungeni walisimama imara. Takriban wote waliipinga bajeti hiyo kutokana na kutoridhishwa na baadhi ya mambo.

Miongoni mwa ushauri wa Kambi ya Upinzani ambao umepuuzwa ni wito wao wa kutaka fungu maalumu la fedha kwa ajili ya kutekeleza mkakati wa kuhami uchumi dhidi ya mtikisiko wa uchumi duniani, Sh. trilioni 1.7 zitungiwe sheria maalumu ya bunge lakini pia taarifa za utumiaji wa fedha hizo ziwe zinawasilishwa katika Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya kulipa bunge fursa ya uhakiki ili kuzuia uwezekano wa kuibuka kwa kile kilichoitwa “EPA namba mbili”; yaani kuibuliwa kampuni hewa na kupewa fedha ambazo mwishowe zinaishia katika mifuko binafsi ya wanasiasa na marafiki wao.
 
Mkuu MN, ni kweli debe tupu lakini angalia:
1. mshahara na marupurupu 12m and it is planned to increase!
2. mikopo ya magari bwerere
3. nafasi ya kupewa ulaji - bodi, RC, Ministers and Deputies etc
4. mengineyo ya kushibisha kabisaaaaa....

sasa Mkuu kwa hayo hata mimi nina uhakika given the chance na kwa kuangalia hali halisi ya hapa nyumbani uongo si kazi ningeamua kutulia tu....... ndio maisha hayo mkuu, kwanza jilinde mwenyewe then wananchi wako..... samahani but this is the fact of life in our Bunge!!!
 
CCM kilukuwa chama cha wakulima na wafanyakazi (alama ya jembe na nyundo) wakati wa Nyerere na mimi nilikuwa mwanachama hai. Leo ni chama cha wafanyabiashara na wanasiasa (alama ya matumizi mabaya ya mali ya umma [ufisadi] na siasa za udanganyifu na mabavu hasa vijijini).
 
Sioni sababu ya kuwa bunge Tanzania. Hili ni kundi la watu linalokutana kupoteza muda na mapesa ya watanzania. Ni kundi linalotutia hasara kubwa kila mwaka. Bunge linatakiwa kuwa wawakilishi wa wananchi kwa serikali. Linatakiwa kupeleka kero, malalamiko na matakwa ya wananchi kwa serikali na wakati huohuo linapaswa kulinda na kutetea masilahi ya wananchi na taifa. Bunge letu hapa Tanzania ni kituko, kwani linatenda kinyume na majukumu yake.

Bunge linatakiwa kuwa na meno/makucha makali kuliko serikali. Linapaswa kuiambia serikali ukweli bila kuogopa wala kutishwa. Lakini kama tuna bunge linaloiogopa serikali na kutishiwa na serikali nalo likatishika, sasa kuna haja gani ya kuwa na bunge?.
Serikali inafanya itakavyo na inawapa wabunge majibu itakavyo na bado wabunge wanakubali upuuzi huo kwa kushangilia bila aibu wala soni.

Tumeona wazi kwamba bajeti ya mwaka 2009/2010 haikuwa nzuri ama haikuwa na faida kwa mtanzania wa kawaida, na baadhi ya wabunge waliliona hilo, wamejaribu kulipigia kelele ile kutishwa kidogo tu wamefyata mkia na kukubali kupitisha bajeti hiyo. Kama wewe ni mbunge ambaye umetumwa bungeni na wananchi wa jimbo lako, kama unaona jambo fulani ni baya ama halina faida kwa wananchi kwanini ukubali lipite?. Ni bora kusimama katika ukweli na kulikataa hilo jambo kwa gharama yoyote ile.

wanaogopwa kufukuzwa toka CCM, kwani walizaliwa na CCM?. Bila CCM hawawezi kuishi?. Ni bora kufukuzwa CCM lakini unasimamia ukweli na bila shaka hata huko jimboni kwako wananchi watakuelewa, watakuthamini na hata ukiamua kugombea ubunge kwa tiketi ya chama kingine ni lazima utapita, wananchi hawachagui chama bali wanachagua mtu mwenye uwezo wa kuwawakilisha kunako husika.

katika suala la TICTS, wananchi tuelewe nani mwenye nguvu?. Wabunge kwa pamoja kabisa mliona TICTS ni mzigo na ni lazima kuiondoa pale Bandarini lakini mpaka sasa ni mwaka hawa jamaa wa TICTS bado wapo na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Wabunge mnafanya nini huko bungeni?. Kwa upande wangu naona ni bora kutokuwa na bunge kwani tutaokoa pesa za wananchi wa Tanzania.
 
Sioni sababu ya kuwa bunge Tanzania. Hili ni kundi la watu linalokutana kupoteza muda na mapesa ya watanzania. Ni kundi linalotutia hasara kubwa kila mwaka. Bunge linatakiwa kuwa wawakilishi wa wananchi kwa serikali. Linatakiwa kupeleka kero, malalamiko na matakwa ya wananchi kwa serikali na wakati huohuo linapaswa kulinda na kutetea masilahi ya wananchi na taifa. Bunge letu hapa Tanzania ni kituko, kwani linatenda kinyume na majukumu yake.

Bunge linatakiwa kuwa na meno/makucha makali kuliko serikali. Linapaswa kuiambia serikali ukweli bila kuogopa wala kutishwa. Lakini kama tuna bunge linaloiogopa serikali na kutishiwa na serikali nalo likatishika, sasa kuna haja gani ya kuwa na bunge?.
Serikali inafanya itakavyo na inawapa wabunge majibu itakavyo na bado wabunge wanakubali upuuzi huo kwa kushangilia bila aibu wala soni.

Tumeona wazi kwamba bajeti ya mwaka 2009/2010 haikuwa nzuri ama haikuwa na faida kwa mtanzania wa kawaida, na baadhi ya wabunge waliliona hilo, wamejaribu kulipigia kelele ile kutishwa kidogo tu wamefyata mkia na kukubali kupitisha bajeti hiyo. Kama wewe ni mbunge ambaye umetumwa bungeni na wananchi wa jimbo lako, kama unaona jambo fulani ni baya ama halina faida kwa wananchi kwanini ukubali lipite?. Ni bora kusimama katika ukweli na kulikataa hilo jambo kwa gharama yoyote ile.

wanaogopwa kufukuzwa toka CCM, kwani walizaliwa na CCM?. Bila CCM hawawezi kuishi?. Ni bora kufukuzwa CCM lakini unasimamia ukweli na bila shaka hata huko jimboni kwako wananchi watakuelewa, watakuthamini na hata ukiamua kugombea ubunge kwa tiketi ya chama kingine ni lazima utapita, wananchi hawachagui chama bali wanachagua mtu mwenye uwezo wa kuwawakilisha kunako husika.

katika suala la TICTS, wananchi tuelewe nani mwenye nguvu?. Wabunge kwa pamoja kabisa mliona TICTS ni mzigo na ni lazima kuiondoa pale Bandarini lakini mpaka sasa ni mwaka hawa jamaa wa TICTS bado wapo na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Wabunge mnafanya nini huko bungeni?. Kwa upande wangu naona ni bora kutokuwa na bunge kwani tutaokoa pesa za wananchi wa Tanzania.

Maneno yako kuhusu hili Bunge la Tanzania yamejaa hekima na busara kubwa na ni mameno yenye ukweli mtupu. Ahsante sana Kidatu.
 
Wasomi: Bunge limepoteza mwelekeo

Fredy Azzah
Mwananchi
12/2/2010


BAADHI ya wasomi na wanasiasa nchini, wameelezea hofu yao kuhusu jinsi Bunge linavyoshughulikia mambo yenye maslahi kwa nchi; wakisema kuwa sasa limeanza kupoteza mwelekeo.

Wasomi na wanasiasa hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana walipozungumza na gazeti hilo kuhusu mjadala wa Richmond ulivyoendeshwa hadi kufungwa kwake.


Mhadhiri Msaidizi katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema Bunge limekubali kuufunga mjadala wa Richmond baada ya kuona haliwezi kuibana serikali itekeleze maazimio yake, hivyo ni dhahiri wananchi wataanza kupoteza imani nalo.

"Tusipende kufanya mambo kwa matukio, badala yake tujiulize kuwa kwanini matukio haya yanatokea, demokrasia tuliyonayo ni ya makundi na sio ya kuwasaidia wanyonge? Alihoji na kuongeza: "Suala hili limeanza tangu mwaka 2007, limekuja kuisha baada ya vikao vikubwa vya CCM kukaa na kamati ya Mzee Mwinyi imechangia.

"Bunge letu haliko huru na haliwezi kuidhibiti serikali kwa sababu liko chini ya CCM; kwa hiyo wabunge wamelinda maslahi yao na chama chao. Hali ya chama ilikuwa mbaya sana, hakuna wakati CCM imepita katika kipindi kigumu kama hiki cha Rais Jakaya Kikwete.

Alibainisha zaidi akisema: "Wabunge wameangalia na kujihoji kwamba je, waendelee na msimamo wao ya awali, au walinde posho zao katika kipindi hiki cha kumaliza miaka mitano ya ubunge wao?"

Kwa mujibu wa Bashiru huu ni wakati ambao Bunge litakuwa dhaifu kuliko wakati mwingine wowote katika uhai wake kwa kuwa wabunge wanajipanga kulinda maslahi yao badala ya maslahi ya taifa. "Mimi mwenyewe sina imani tena na bunge Wale wabunge waliosema mpaka kieleweke wako wapi sasa?" alihoji.

Alisema kwa kuwa wabunge wameacha kutetea haki za wanyonge na kuanza kutetea maslahi yao, kila mwananchi sasa anatakiwa kuingia kwenye mapambano ya kujikomboa dhidi ya umaskini walionao kwa kufanya kazi kwa nguvu zao na kudai haki zao za msingi.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga aliungana na Bashiru akisema sakata la Richmond limemalizwa kwa maslahi ya CCM.

"Bunge limeshindwa kazi, limeshindwa kuisimamia serikali kama ilivyo moja ya kazi zake, badala ya ripoti yake ni mabovu na wamepoteza muda mrefu bure bila mafanikio," alisema na kuongeza: "Pamoja na uzito wa suala la Richmond, wabunge wamelichukulia kwa maslahi yao na CCM".

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema suala hilo limezimwa kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi.

"Mimi sielewi. Wanasema mjadala wa Richmond umefungwa, lakini hatujaambiwa hasara iliyopatikana kutokana na mkataba huu," alisema Profesa Lipumba na kuongeza: "Pia, Watanzania tunataka kujua nani alisababisha hasara hiyo? Kwa ujumla, wameufunga kwa sababu huu ni mwaka wa uchaguzi".


Hata hivyo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bensoni Bana, alisema hana tatizo na jinsi suala la Richmond lilivyomalizwa bungeni; lakini kama kuna mbunge anayeona kuna shida, anaweza kulipeleka suala hilo kwa wananchi.

Alisema Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliifunga hoja hiyo kwa kutumia vifungu vya sheria na karibu wabunge wa pande zote walionekana kuridhika na majibu ya kamati ya bunge na serikali, hivyo haoni kama kuna tatizo.


Alisema jibu la suala la Richmond lilishapatikana tangu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa na mawaziri wengine wawili walipoamua kujiuzuru kwa manufaa ya umma.

"Ingawa hoja hiyo imekwisha, serikali imejifunza kutochezea hoja za wabunge wakati wote na hatujui gharama ambazo serikali ilitumia kumaliza suala hilo,"alisema Bana. Juzi Bunge lilifunga sakata la Richmond na kuiacha serikali iendelee kutekeleza maazimio yake.
 
bunge limejaa puppets mpaka lina kera.halina maana lolote ni bora livunjwe tu na nchi itaweza kufanya mambo mengi bila ya wao.
 
Haya ni matokeo ya kibano cha 6 toka NEC, hapa mshindi ni king maker sasa ndio amepata nguvu na amini msiamini, anakuja kuwashika!
 
Mimi nimekata tamaa kabisa na mwelekeo wa nchi yetu. Baadhi ya Wabunge walinipa matumaini makubwa labda Bunge la CCM litaacha kuwa rubber stamp ya Serikali na hivyo kuanza kuweka maslahi ya nchi mbele badala ya yale ya CCM. Wale Wabunge wote waliojiita wapambanaji miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 wamenyamaza kabisa na kufuata mstari wa Serikali na hivyo yale yote waliyokuwa wanayapigia kelele kuwekwa kapuni ili kuonyesha "mshikamano" ndani chama.

Inaudhi na inauma sana kuona Serikali hii iliyofanya mambo kienyeji enyeji mno na kushindwa kutimiza hata moja ya ahadi zake inarudi tena madarakani kama vile kila kitu kilikuwa ni shwari kabisa katika awamu ya kwanza ya Serikali hii. Pia kwa mara nyingine tena sioni dalili katika uchaguzi ujao vyama vya upinzani kupata hata Wabunge 20 bara katika uchaguzi huo. Hivyo CCM wataendelea kuiburuza na kuifisadi nchi watakavyo bila ya kuwa na woga wowote. Kweli CCM itatawala Tanzania daima! :(
 
.........Binafsi nimekuwa nikipata shida sana naposikia wabunge,mawaziri,maspika,waandishi wa habari,wananchi nk wanapoliita bunge letu kwa lugha ya "Bunge tukufu" ninapata shida kwasababu ya yanayooendelea mule mjengoni kama tulivyozoea kupaita...Unafiki,majungu,mzaha,ufisadi,vijembe,ubinafsi,chuki,masihara,wizi,visasi nk.Haya yote yananifanya kuwa mzito kuikubali hii sifa kuwa ni bunge tukufu...tangu bunge la kumi limeanza tuliona majungu,mipasho ikitawala na wabunge+mawaziri wakisahau wajibu wao tuliowatuma.Binafsi nakumbuka rais wa awamu ya tatu Ben Mkapa baada ya kuingia madarakani halikataa kuitwa mtukufu kwasababu kuwa ni sifa ya juu mno kwake na inamstahili Mungu pekee,yawezekana alijua hatachakachua ndio maana hakutaka kuitwa "Mtukufu Rais" hilo sijui!..langu ni kuwa,Je kwa hali hii ili bunge linafaa kuitwa "Bunge tukufu".......
 
KATIKA HILI ZITTO KABWE YUKO SAHIHI KABISA NA KWAMBA BAADA YA OFISI YA SPIKA KUWAGAWIA WABUNGE NAKALA YA MUSWADA WA MOI SASA KILA MBUNGE ARUDI JIMBONI TUKASHAURIANE KWANZA TENA BILA KUKOSA!!!!

Katika hili mchangon wa Mheshimiwa Zitto IKO SAHIHI KABISA.

Kiukweli nawaasa Wapiganaji, tusiwe wanafiki kwamba kama hatukubaliani na Zitto juu ya mambo kaadha, sawa na mimi nisivyokubaliana naye juu ya mambo mengi, basi hata pale anapotetea msingi unaokubaliana na matakwa yetu kama Umma wa Tanzania (na wala si kutetea msingi wa mafisadi) basi sisi ni kukimbilia tu KUMWAGA MAJI NJE PAMOJA NA MTOTO NDANI YA BESENI.

Kimsingi kabisa, ni kwamba mara baada ya ofisi ya bunge kuwagawia kila mbunge nakala ya mswada wa CCM basi sasa ni muda muafaka kwa KILA MBUNGE KURUDI JIMBONI KWAKE KWENDA KUSHAURIANA NA MABOSI WA (Sisi Wapiga Kura) juu ya aina ya muswada uliowashilishwa bungeni, maana na mantiki yake, kwa kiasi gani inavyowakilisha maoni yetu.

Tena ni kwamba hadi hapo sasa SISI KAMA WAPIGA KURA TUNAMPA MHESHIMIWA MBUNGE WETU UJUMBE GANI WA KWENDA KUCHANGIA KULE bungeni pindi mjadala utakapoanza; yaani ni kwamba tutakuwa tunamwelekeza mbunge wetu juu ya kitu gani akiunge mkono, kipi kirekebishwe vipi na mambo yapi akayakatae moja kwa moja.

Hakika alichokisema Mhe Zitto endapo haitozingatiwa na Wabunge kudiriki kushiriki mjadala wa HUU MUSWADA BATILI WA CCM bila kwanza kuomba maelekezo ya wapiga kura basi mjue ya kwamba WABUNGE WENGI SANA WATAKAOPINGANA NA UMMA basi ni dhahiri kwamba kibarua chao kitaota mbawa.

Huu mswada, kwa watu makini na wadadisi wa mambo watagundua kwa AG Werema kaudesa kutoka kwa MUSWADA WA MOI WA KENYA enzi hizo alipojitia kicha ngumu kukubali wananchi wake kujiundia katiba mpya. Leo hii Moi hayupo madarakani huko lakini wananchi wapo wamejaa tele na KATIBA MPYA kabisa kutokana na wananchi moja kwa moja sasa hivi inafanya kazi.

Jamani huu mswada wa Moi ambayo hivi sasa Kikwete Kaudesa nukta kwa nukta isipokua kafanya tu kazi ya kuingiza 'Unite Republic of Tanzania' kila mahali kwenye ile nafasi iliyoandikwa Republi of Kenya, hata kule kwa Kibaki alikoidesea Kikwete nako pia iliwahi kukataliwa na kutupiliwa mbali na kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya sheria na katiba na AG kulazimishwa kushauriana kwanza na wadau wote na kuingiza mapendekezo yao moja kwa moja ndani ya muswada ndio mambo yaendelee kwenye sakafu la bunge.

Na hiyo ndio siri kwa nini huo mswada muhimu sana kwa kila raia haukuandikwa kwa lugha yetu ya Kiswahili. Maswali zaidi muulizeni Msekwa aliyeenda huko majuzi kuchukua zaidi ya MOI'S UNPOPULAR FILE ON CONSTITUTION ili waje kuvijaribishia kwetu kama tutakubali.

Tumsikilize Zitto katika hili na hatua ya kufuatia ya maandamano nchi nzima kupinga huu mswada dhalimu ni kwamba maelekezo tutapeana kwa wakati na mtindo stahiki endapo kweli serikali haitoingiza maoni ya Wadau wa katiba kwenye huo muswada.

Aluta Continua!! Vijana kote nchini tukae tayari mkao wa kulikomboa taifa letu, ONCE AND FOR ALL, kutoka mikononi mwa MAFISADI endapo maslahi yao ndio itakayoonekana wa muhimu zaidi hapa!!!!!!!!!!!!

Naona safari ya kamba kukatikia pabovu, baada ya kuibiwa sana kura zetu, kudhalilishwa sana kimaisha na MAFISADI, baada ya kulaghaiwa sana na na vingozi wa CCM, ndio huu!!!!!!

TUJE TUJADILIANE NINI??KWA MFANO??

MSWAADA TAKATAKA,WANACNHI TUNAJADILI TAKATAKA ILI TUTOE MAWAZO TAKATAKA AU??
acha utani na huyo ZITTO NI KIATU TUU WALA USIMSIKILIZE NI MNAFKI,MZANDIKI NA MSALITI
 
baada ya mzee kifimbo kuachia ngazi mwaka 1985.................warithi wake wakabuni namna ya kujitukuza....................mithali ya Mwenyezi Mungu............................kwanza walipitisha sheria ya kuwa wao ni waheshimiwa..................na asiyewaita hivyo kuchukulia hatua stahiki za kisheria.........................................na baada ya hii kutotosha wakaanza kimyakimya kuliita Bunge ni tukufu...................kwa sababu linakidhi mahitaji ya matumbo yao ambayo ndiyo wanayaabudu......................

Kule Kenya wakati wa enzi za Bw. Moi vyombo vya habari vilikuwa vinamwita mtukufu Rais Daniel Arap moi............................lakini sikuwahi kusikia Bunge lao wanalitukuza kama Muumba.......................................

sasa bunge letu limekuwa likijenga ubwana na utwana kwa kutumia nguvu za sheria ambao waumini wake akiwamo Waziri wa Bomoabomoa..........wamekuwa wakizihubiri kama vile ni msahafu Mtakatifu.................................

baadhi ya sheria ambazo Bunge linalojiona ni tukufu ambazo wameziunda kukuza matabaka ndani ya jamii ni pamoja na.......................

1) Pensheni za viongozi wa kitaifa na wengineo kwa upande mwingine...................madai hapa ni kuwa wakubwa matumbo yao pia ni makubwa haswa wakistaafu............................lakini hao wengineo watajijua......................they are on their own...........

2) Mfumo wa kodi kandamizi ambao unawabagua wale wanaolipwa ujira dhidi ya wale ambao wanajiajiri....................yawaje mwenye mshahara awe anazuiwa kulipa kodi kama pato lake ni kcc....................lakini mjasiria mali awe anashinikizwa kulipa kodi bila ya kujali kipato chake kuwa chini ya kcc.....................kwa nchi ambayo katiba yake inakataza ubaguzi wa aina zote.......................hii sasa ni aibu.................

3) Huku tunahimiza wawekezaji wa kutoka nje waabudiwe.......................lakini hapohapo tunabuni mbinu za kuhakikisha hawachangii katika pato la taifa.............................ila la sisiemu kwa kuingiza mipesa kwenye akaunti yao kule NewYork na London..........................nchi hii inayoendeshwa kwa misingi ya dhuluma kweli itafuta kero za ajira hapa nchini au kumkwamua mkulima kweli aachane na jembe la mkono kama siyo geresha tupu......................

4) wakati wageni hawalipi kodi serikali kuu na ile ya mitaa wanaunganisha nguvu ya kubuni mikakati ya kuvirudia vyanzo vilevile vya kodi kwa kubadilisha majina ya kodi tu......................kuanzia vat, excise duty, import and export, property taxes, n.k...........kwa kumkamua ng'ombe hadi akatoa damu badala ya maziwa huku wageni wanaendelea na likizo isiyo na kikomo ya kutolipa kodi...................nchi hii kweli ina mwelekeo wa kumpa raia wa kawaida matumaini?

5) sehemu kubwa ya wabunge uhalali wao unatokana na au kuiba kura, kuwanunua TISS na NEC...............na hii inaelezea ni kwa nini hawamjali mpigakura kwa sababu wamejijengea ukuta wa kioo wa kuwahakikishia ya kuwa wapige kura au hata wasimpigie bado ataendelea kutesa........

6) Ukitaka kujua demokrasia yetu ni geresha tupu.............................jiulize kwa nini Bunge linapitisha sheria ya kupiga marufuku mgombea binafsi..............................ni nini wanakiogopa?

7) Pamoja nasi kuwakandia mataifa ya kibeberu kwa kashfa za mdomoni......................lakini kimyakimya viongozi wetu hutembeza bakuli kwenye miji mikuu ya nchi hizo huku wakirudi hawaoni haya kudai bila ya misaada hakuna maendeleo kwetu........................bila ya kuzingatia ya kuwa katiba yetu inatubana tujitegemee wenyewe..............................

8) Viongozi wetu wanapoumwa hudai na kulazimisha kwenda matibabu nje...............hawataki hospitali zetu....ambazo ni wao wamezidunisha.....wakati mzee kifimbo kazidiwa mwaka 1999 na aligoma kwenda matibabu nje......................Mkapa alimwambia eti watanzania hawatamwelewa kama hatampeleka kutibiwa nje...............pamoja na mihangaiko hiyo Nyerere alirudishwa kwenye jeneza..........................kwa maana ya kuwa hizo jitihada za kiubaguzi wala hazikusaidia lolote........................swali ambalo niwaachia ni kuwa hivi Bunge lenye kumkashifu Mwenyezi Mungu kwa kujiita nalo eti ni tukufu laweza kweli kutunga sheria zinazomjali myonge wakati linajijengea mazingira ya kuwa na tofauti na wale ambao linawatawala?

sababu kubwa ya kudai uhuru ilikuwa ni kuwa tujitawale wenyewe kwa kuwa ndiyo tunajua shida zetu.........................lakini sasa imegeuka kwani viongozi wetu wamejitenga nasi kwa kujijengea mazingira bora kwa wao tu.................................nasi tumeachwa solemba........
 
Back
Top Bottom