Bunge letu tukufu limekosea wapi?

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
880
844
Leo nimeona tujadiri wapi bunge letu limekosea/linakosea.
Awali tunajua kuwa mbunge wa Jimbo anapochaguliwa anawakilisha wana-Jimbo wote.

Sasa mbona wanawake wanataka mwakilishi wao, mbona walemavu wanataka mwakilishi wao, mbona vijana wanataka mwakilishi wao. Na baadae wazee watataka mwakilishi wao, watoto watataka mwakilishi wao, wafanyakazi watataka mwakili, wakulima watataka mwakilishi.

Katika Hali kama hiyo nauliza wabunge wetu wa majimbo wanamwakilisha nani? au wamefeli wapi? Ukiona Kila kundi linataka kujiwakilisha, maana yule aliyepo amefeli.

Kama siyo kufeli, basi bunge linatumiwa kama kijiwe Cha ajira (mahali pa kujitafutià ajira). Kila mtu anatafuta dirisha la kupitia kuingia bungeni. Wasomi (professor/daktari), vijana waliomaliza vyuo, wafanyakazi waliopo kwenye ajira za serikali, wanaacha kazi zao ili waingie bungeni.

Sitaki kusema bunge letu ni waroho. Wanajipangia mishahara na marupurupu yanayofanya Kila mtu anavutika kuingia bungeni ili akapate mshahara mzuri, allowance za siku zinazozidi mshahara wa kima Cha ChinI, kiinua mgongo Cha miaka 5 kinachozidi mfanyakazi wa miaka 30.

Kilichofanyika bungeni, kwa nini kisifanyike kwenye kilimo. Ili kada zote nilizozitaja hapo juu, zivutike kukimbilia kwenye kilimo?
 
Back
Top Bottom