KATIKA HILI ZITTO KABWE YUKO SAHIHI KABISA NA KWAMBA BAADA YA OFISI YA SPIKA KUWAGAWIA WABUNGE NAKALA YA MUSWADA WA MOI SASA KILA MBUNGE ARUDI JIMBONI TUKASHAURIANE KWANZA TENA BILA KUKOSA!!!!
Katika hili mchangon wa Mheshimiwa Zitto IKO SAHIHI KABISA.
Kiukweli nawaasa Wapiganaji, tusiwe wanafiki kwamba kama hatukubaliani na Zitto juu ya mambo kaadha, sawa na mimi nisivyokubaliana naye juu ya mambo mengi, basi hata pale anapotetea msingi unaokubaliana na matakwa yetu kama Umma wa Tanzania (na wala si kutetea msingi wa mafisadi) basi sisi ni kukimbilia tu KUMWAGA MAJI NJE PAMOJA NA MTOTO NDANI YA BESENI.
Kimsingi kabisa, ni kwamba mara baada ya ofisi ya bunge kuwagawia kila mbunge nakala ya mswada wa CCM basi sasa ni muda muafaka kwa KILA MBUNGE KURUDI JIMBONI KWAKE KWENDA KUSHAURIANA NA MABOSI WA (Sisi Wapiga Kura) juu ya aina ya muswada uliowashilishwa bungeni, maana na mantiki yake, kwa kiasi gani inavyowakilisha maoni yetu.
Tena ni kwamba hadi hapo sasa SISI KAMA WAPIGA KURA TUNAMPA MHESHIMIWA MBUNGE WETU UJUMBE GANI WA KWENDA KUCHANGIA KULE bungeni pindi mjadala utakapoanza; yaani ni kwamba tutakuwa tunamwelekeza mbunge wetu juu ya kitu gani akiunge mkono, kipi kirekebishwe vipi na mambo yapi akayakatae moja kwa moja.
Hakika alichokisema Mhe Zitto endapo haitozingatiwa na Wabunge kudiriki kushiriki mjadala wa HUU MUSWADA BATILI WA CCM bila kwanza kuomba maelekezo ya wapiga kura basi mjue ya kwamba WABUNGE WENGI SANA WATAKAOPINGANA NA UMMA basi ni dhahiri kwamba kibarua chao kitaota mbawa.
Huu mswada, kwa watu makini na wadadisi wa mambo watagundua kwa AG Werema kaudesa kutoka kwa MUSWADA WA MOI WA KENYA enzi hizo alipojitia kicha ngumu kukubali wananchi wake kujiundia katiba mpya. Leo hii Moi hayupo madarakani huko lakini wananchi wapo wamejaa tele na KATIBA MPYA kabisa kutokana na wananchi moja kwa moja sasa hivi inafanya kazi.
Jamani huu mswada wa Moi ambayo hivi sasa Kikwete Kaudesa nukta kwa nukta isipokua kafanya tu kazi ya kuingiza 'Unite Republic of Tanzania' kila mahali kwenye ile nafasi iliyoandikwa Republi of Kenya, hata kule kwa Kibaki alikoidesea Kikwete nako pia iliwahi kukataliwa na kutupiliwa mbali na kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya sheria na katiba na AG kulazimishwa kushauriana kwanza na wadau wote na kuingiza mapendekezo yao moja kwa moja ndani ya muswada ndio mambo yaendelee kwenye sakafu la bunge.
Na hiyo ndio siri kwa nini huo mswada muhimu sana kwa kila raia haukuandikwa kwa lugha yetu ya Kiswahili. Maswali zaidi muulizeni Msekwa aliyeenda huko majuzi kuchukua zaidi ya MOI'S UNPOPULAR FILE ON CONSTITUTION ili waje kuvijaribishia kwetu kama tutakubali.
Tumsikilize Zitto katika hili na hatua ya kufuatia ya maandamano nchi nzima kupinga huu mswada dhalimu ni kwamba maelekezo tutapeana kwa wakati na mtindo stahiki endapo kweli serikali haitoingiza maoni ya Wadau wa katiba kwenye huo muswada.
Aluta Continua!! Vijana kote nchini tukae tayari mkao wa kulikomboa taifa letu, ONCE AND FOR ALL, kutoka mikononi mwa MAFISADI endapo maslahi yao ndio itakayoonekana wa muhimu zaidi hapa!!!!!!!!!!!!
Naona safari ya kamba kukatikia pabovu, baada ya kuibiwa sana kura zetu, kudhalilishwa sana kimaisha na MAFISADI, baada ya kulaghaiwa sana na na vingozi wa CCM, ndio huu!!!!!!