Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,548
Baada ya Baba kusafiri nyumba inaongozwa na Mama akisaidiana na Kaka yetu mkubwa kwa kweli sisi ni watoto wa Baba mmoja lakini Mama na Kaka yetu wanatubagua sana. Dada Leticia aliangalia picha za mbaya juzi akaja akamwambia Mama na kaka mkubwa kwamba sisi watoto wa hapa nyumbani twende kusomea namna ya kutongozana. Kaka Mwigulu alikuwa akibishana jambo na Kaka John Mnyika Mama akaingilia kati kwa kumpendelea Kaka Mwigulu ambaye alimwambia kwa kejeli kuwa wanapoongea wakubwa mtoto wa kiume anatakiwa anyamaze. Naye kaka Peter Serukamba alitoka huko kama kalewa hivi kwa kweli alipofika mlangoni tu, alianza kupiga kelele alipobishwa alitamka matusi hayo kasema "kamoni faki yu" niliwahi kumsikia Tyson akimtukana hivyo hivyo Evander siku walipopigana akamng'ata sikio. Ubishi ulikuwa mkubwa sana Kaka Juma Nkamia wakati akiendelea kusuluhisha ulitokea ubishi katikati ya mazungumzo yake alipobishwa kidogo tu basi aling'aka akasema haongei na mbwa bali anaongea na mwenye mbwa, yaani sisi ni mbwa.
Mama na Kaka mkubwa wamekuwa wakitoa maamuzi ya upendeleo sana utadhani sisi siyo watoto wa baba mmoja kaka alitufukuza tusikae pale nyumbani na mama aliporudi toka safari ameungana na kaka mkubwa kuwa tusikae pale nyumbani. Tunatamani hata kuhama hapa nyumbani lakini basi tu tukihama tutaenda wapi? Tunaishi maisha ya utukutu sana hapa nyumbani si mama, si kaka mkubwa, yaani wote ni tumegeuka watukutu. Akirudi Baba nakuja kusema yooooote!!!!