Watanzania mnapenda Bunge lijalo 2025 - 2030 liwe na sura gani?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,391
1,259
Watanzania,
SALAAM!
Hivi sasa kwa tathmini ya haraka ufuatiliaji wa mijadala ya Bunge kwa wananchi wa kawaida umepungua kwa takriban asilimia 30.

Kwamba kwa kila watu wazima 10 ni watu 7 tu wanaoweza kufahamu mambo ya kibunge na bunge. Tofauti na mwaka 2005 - 2010 ambapo kwa kila watanzania 10 wote waliweza kufahamu mambo mbalimbali ya Bunge na wabunge hususan maendeleo ya mijadala.

Sasa, ili kurudi katika zama hizo mnashauri Serikali na mamlaka za vyama vya siasa zitumie mbinu ipi ili watu wengi wafuatilie shughuli za bunge na wabunge? Je, upo ushauri kwa CCM, CDM, ACT, Umoja, CUF nk?

Msakila Kabende
(Mchumi Mbobezi / Mwanasiasa)
 
Acha upotoshaji wala sio 30% iliyoacha kufuatilia bunge, 80% hawafuatilii bunge, na ukweli ni kuwa ccm sio chama Cha kizazi hiki, na Iko madarakani kwa shuruti. Hakuna uwezekano watu kuendelea kufuatilia vikao vya ccm ndani ya jengo la bunge maana ccm ni chama Cha wazee, au vijana mazombie na wasaka fursa. Na hivi mwenyekiti wa ccm anavyolazimisha kuwa mteule wa tume ya uchaguzi, sioni wapiga kura wa maana hiyo 2025.

Inshort watanzania wengi wamepuuza zoezi Zima la uchaguzi. Na sababu hasa ni ccm kuipotezea siasa mvuto kwa yule kiongozi muovu kulazimisha ionekane ccm inakubalika wakati si kweli. Bila tume huru na katiba mpya, siasa zitaendelea kupoteza mvuto, kwani ccm inashuritisha kutawala kizazi kilichoichoka na kuikinai.
 
..bunge lenye meno.

..uwiano uwe 55 to 45 kati ya serikali na wapinzani.

..uwiano huo utapelekea sheria kupitishwa baada ya kuungwa na mkono na angalau 11% ya wapinzani.
 
Back
Top Bottom