Bunge lashauri ukaguzi wa Chakula kufanywa na TMDA na sio TBS

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeishauri serikali kufanya tathmini kuhusu usimamizi wa Usalama wa Chakula kurejeshwa Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba (TMDA), ili kurahisisha utendaji

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Aloyce Kamamba, amesema Wizara ya Afya na Wizara ya Viwanda na Biashara zikutane na kutafuta muafaka wa huduma za Chakula na Dawa kuwa sehemu moja kwasababu ni masuala yanayofanana kuliko kuendelea kubakia TBS.

==========================

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeishauri serikali kufanya tathmini ya kina ya usimamizi wa masuala ya chakula kurejeshwa chini ya Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba (TMDA), ili kurahisisha utendaji kazi na kusimamia usalama wa chakula nchini.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Aloyce Kamamba, mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika Ofisi za TMDA, Kanda ya Ziwa, Mwanza.

“Ni vyema Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara, izikutanishe kamati hizi mbili na kutoa ushauri ambao unakidhi mahitaji ya sasa huduma hizi kuwa sehemu moja,” amesema Kamamba na kuongezea kuwa masuala ya dawa na chakula ni maeneo yanayofanana, ukichukua kwa upande wa chakula usimamizi uko TBS (Shirika la Viwango Tanzania) na dawa ziko TMDA.

Kwa upande wake Tumainieli Macha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango, akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, amesema hadi mwaka 2018, masuala ya usimamizi wa chakula yalikuwa chini ya TFDA (TMDA kwa sasa), kabla ya kuhamishiwa kwenda TBS.

Macha amesema serikali imeanza kufanya mapitio upya ya usimamizi wa masuala ya chakula, ili kuboresha upatikanaji wa huduma na kuongeza usimamizi wa masuala ya chakula na dawa nchini.

“Kulingana na tathmini itakayofanyika na kuwashirikisha wadau wote, tutapata majibu na kuweza kuboresha huduma hizi kwa wananchi pasipo kupata madhara yeyote kwenye usimamizi wa chakula, dawa, vifaatiba au vipodozi,” amesema Macha.

HABARI LEO
 
Wapo sahihi TBS pana urasimu sana hao chakula na dawa hawana mambo mengi TBS wana vipengele utadhani tuna viwanda ukileta bidhaa na pia ni gharama zimeongezeka tofauti na hao wengine sijui maamuzi yao mwanzoni hawakufikiri hili...
 
Hilo nalo ni la kujadili?, chakula na dawa ni vitu vilivyopaswa kuwekwa pamoja, TFDA ilikuwa na mantiki zaidi
 
Theoretically ni sahihi lakini kiutendaji, suala hili tunafahamu sababu yake ni mapato. TMDA inaonekana kufulia na wanafahamu sana kwamba sehemu kubwa ya pesa iko kwenye vyakula. Kampeni hii tunaifahamu imeanza siku nyingi sana! Sababu ni upigaji, upigaji. Kamatu ya Bunge pia tunafahamu imedaka mshiko wake toka Afya!! Nchi ya wapigaji tu!
 
Ulichosema nakubaliana na we we kwa 100%.

UPIGAJI.

Hapa kinachofanyika in Lobbying.

Tangu Chakula na Vipodozi vihamishiwe TBS, TMDA wamebaki na njaa kinoma mpaka wanataka kukagua wavuta sigara.

Kama kweli nia yao ni kurahisisha UKAGUZI kwanini wasipigie CHAPUO Maafisa Afya was Halmashauri wapewe nguvu na kwezeshwa badala yake wamebaki kupinga kitu kile kile walichopitisha miaka 2 nyumba.
 
Maamuzi ya kutenganisha Chakula na Dawa hayakuwa sahihi, Duniani kote hivi vitu vinasimamiwa na Mamlaka moja.
 
Maamuzi ya kutenganisha Chakula na Dawa hayakuwa sahihi, Duniani kote hivi vitu vinasimamiwa na Mamlaka moja.
Unachosema ilikuwa vibaya kuunda TMDA tangu mwanzo. Nashuri TBS na TMDA viunganishwe. Wote wawe ndani ya TBS. SIMPLE!
Hatutaki kelele za upigaji tu!
 
Theoretically ni sahihi lakini kiutendaji, suala hili tunafahamu sababu yake ni mapato. TMDA inaonekana kufulia na wanafahamu sana kwamba sehemu kubwa ya pesa iko kwenye vyakula. Kampeni hii tunaifahamu imeanza siku nyingi sana! Sababu ni upigaji, upigaji. Kamatu ya Bunge pia tunafahamu imedaka mshiko wake toka Afya!! Nchi ya wapigaji tu!
PAMOJA NA HOJA YAKO YA MSINGI, LAKINI PIA TBS HAITENDEI HAKI WATANZANIA KATIKA KUDHIBITI USALAMA WA CHAKULA. Hivi inaingia akilini mkuu wa idara ya uandaaji wa viwango vya vyakula na kilimo kuwa mechanical engineer?anatakuwaje na uwezo wa kuhamasisha uaandaaji wa food safety standards bora????? TBS ipo shida kubwa?
 
Back
Top Bottom