Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Bunge la Marekani, Chris Smith, amekemea vikali vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na mateso dhidi ya waumini wa dini mbalimbali duniani. Katika hotuba yake, Smith ameorodhesha nchi zinazokandamiza uhuru wa kidini kuwa ni China, Urusi, Nikaragua, Korea Kaskazini, Belarus, Cuba, Afghanistan, Iran, Pakistan, Nigeria, Syria, Sudan na Tanzania.
Amesema waumini wa dini mbalimbali wanakabiliwa na ukatili, ikiwemo kukamatwa na polisi, kufungiwa nyumba za ibada, na katika baadhi ya nchi wanafikia hata kuuawa.
Sehemu ya hotuba yake kuhusu Tanzania, Smith amesema: “Nchini Tanzania uhuru wa kuabudu umeporomoka kwa kiwango cha kutisha. Waumini wanazuiwa kuabudu huku viongozi wa kidini wakipitia mateso. Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Padre Charles Kitima, alishambuliwa baada ya kukosoa serikali mara kwa mara. Hata baada ya jaribio la kumuua kushindikana, bado ameendelea kutishwa na kupewa kashfa na makundi ya vijana bila serikali kuchukua hatua.
Kwa upande mwingine, zaidi ya matawi 2,000 ya makanisa yanayohusiana na Askofu Josephat Gwajima yalifungwa baada ya Askofu huyo kukemea vitendo vya utekaji na mauaji ya raia kiholela. Waumini hao walipojaribu kukusanyika kwa ajili ya ibada walipigwa, kurushiwa mabomu ya machozi na kukamatwa na Jeshi la Polisi.
Haya yote yanatokea wakati ambapo Kiongozi wa upinzani nchini humo, Tundu Lissu, bado yuko gerezani, na Balozi wa zamani Humphrey Polepole akiwa hajulikani alipo baada ya kutekwa, huku damu ikionekana katika eneo alilokuwa akiishi ushahidi kuwa alijeruhiwa kabla ya kukamatwa. Si hivyo tu, pia mamia kama si maelfu ya Watanzania wametoweka baada ya kudaiwa kutekwa kutokana na ukosoaji wao kwa serikali.
Mauaji ya Oktoba 29 yanabaki kuwa doa kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo. Umoja wa Mataifa umethibitisha zaidi ya watu 700 waliuawa wakiwemo watoto wadogo na mama wajawazito. Ikiwa Jumuiya ya Kimataifa ingeingilia mapema, mauaji hayo yangeweza kuepukika. Bunge la Congress linatoa rai kwa serikali ya Marekani na Jumuiya ya Kimataifa kutazama zaidi hali ya Tanzania"
Kwa hotuba kamili ya Smith ingia hapa Press Releases | Republican Foreign Affairs Committee