Bunge la bajeti litahudhuriwa na wabunge wasiozidi 150, sijajua sheria inaruhusu au huu uamuzi ni sahihi? Na bunge kuanza saa nane mchana

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mabadiliko katika bunge la bajeti linaloanza Machi 31, Dodoma:

Hakuna maswali kwa waziri mkuu

Bunge litaanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni

Maswali na majibu yatatumwa kwenye 'tablets' za wabunge

Kura za kupitisha bajeti zitapigwa kwa mafungu

Waandishi wachache wataruhusiwa
IMG_20200330_203038.jpg
IMG_20200330_203043.jpg
 
Tetesi mwanzoni lilikuwa lisiwepo kabisa..then zikaja habari kwamba watakuwa Wabunge 50 tu per meeting..naona sasa ndio wamekuja na hiyo figure ya Wabunge 150 kwa kikao..

Anyway hata kama wangekuwa wote 300+, pale hakuna Bunge, ni takataka rubber stamp ya kupitisha mambo ya serikali.
 
Kwa hali ilipofikia, hakuna haja ya vikao vya Bunge, Bunge liahirishwe ili hiyo posho ya vikao ielekezwe kwenye mapambano dhidi ya Corona.

Ibaki posho ya wiki moja tu kabla ya Bunge kuvunjwa, hapo ugonjwa huu huenda ukawa umeshapungua makali.

Bajeti zote za wizara na bajeti kuu zipitishwe wiki moja kabla ya Bunge kuvunjwa.

Ninashauri hivyo kwa sababu sijawahi kuona Bunge likikataa kupitisha bajeti yoyote, hivyo haina haja ya kujiweka katika hatari ya kuambukizana Corona.
 
Ukisikia uchawi ndo huu sasawenzio ndo kikao cha mwisho hiko sidhani kama itakubaliwa asee.

All in all hoja nzuri sana ila si rahisi kukubaliwa na members wenyewe!!

Sent from my iphone using jamiiforums
 
Tukirudi kwene Sheria, Kanuni na taratibu kutakuwa na Bunge hapo?
Kuna mijadala inahitaji kutimia Akidi ya Wabunge itakuwa je?
Futilia mbali Bunge hili halina ulazima kwa kipindi hiki....mbona Mwenge imewezekana?
 
UKISIKIA UCHAWI NDO HUU SASAWENZIO NDO KIKAO CHA MWISHO HIKO SIDHANI KAMA ITAKUBALIWA ASEE

ALL IN ALL HOJA NZURI SANA ILA SI RAHISI KUKUBALIWA NA MEMBERS WENYEWE!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapo ndipo tutaona uzalendo wao wanaohubiri kila siku.
 
Back
Top Bottom