Bunge la bajeti litahudhuriwa na wabunge wasiozidi 150, sijajua sheria inaruhusu au huu uamuzi ni sahihi? Na bunge kuanza saa nane mchana

Tetesi mwanzoni lilikuwa lisiwepo kabisa..then zikaja habari kwamba watakuwa Wabunge 50 tu per meeting..naona sasa ndio wamekuja na hiyo figure ya Wabunge 150 kwa kikao..

Anyway hata kama wangekuwa wote 300+, pale hakuna Bunge, ni takataka rubber stamp ya kupitisha mambo ya serikali.
Nakubaliana na wewe bora budget ipitishwe bila vikao vya bunge maana miaka yote huwa inapitishwa jinsi ilivyoletwa
 
Spika Ndugai amesema wamepunguza muda wa kukaa bungeni kwa siku na idadi ya wabunge wanaopaswa kuhudhuria kwa wakati mmoja.

Bunge litaanza vikao saa 8 mchana hadi 12 jioni badala ya kuanza asubuhi na wabunge watakaohudhuria kwa mara moja ni 150 badala ya 300+

Swali; Je marekebisho hayo yamehusisha kupunguza Sitting allowances pia za wabunge na watendaji wa bunge?

Nawasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni vyema posho za hilo bunge zikaingia kwenye mfuko wa dharula ili pale hali ya Corona itakapokuwa mbaya zitumike, Bunge lisiwepo kabisa mpaka hali ya Corona itakavyotulia kabisa..

Uwepo wa Bunge na shughuli zake,Wabunge pale Dodoma ni hatari sana kwa ule mji kipindi hiki. Uwepo wa Bunge huongeza idadi ya watu na kuleta msongomano ambao ni hatari kwa sasa.
 
Tutambue pia kwa sasa Corona inaweza kutumika kama silaha kuangusha uchumi wa baadhi ya nchi na kurudisha maendeleo nyuma kwa manufaa ya watu fulani, tutambue uwepo wa Corona unaweza kuwaacha baadhi hoi na kuwapa wengine utajiri wengine wenye kutumia akili na hesabu.

Kuliacha Bunge liendelee ni kuongeza mkusanyiko usio na maana pale dodoma kuanzia mabarabarani, maofisini, mahotelini nk. Hali italeta urahisi wa Corona kuenea na kushika kasi kuanzia Dom, Moro, Singida na Dar.. Speed ya Corona ikiwa kubwa basi hata wale maadui wa kiuchumi wanaweza kujipenyeza na kutumaliza..
 
Mabadiliko katika bunge la bajeti linaloanza Machi 31, Dodoma:

Hakuna maswali kwa waziri mkuu

Bunge litaanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni

Maswali na majibu yatatumwa kwenye 'tablets' za wabunge

Kura za kupitisha bajeti zitapigwa kwa mafungu

Waandishi wachache wataruhusiwa
View attachment 1404248View attachment 1404249
Mkuu kuna sheria kwenye nchi hii ??, siku hizi kila mtu anafanya lake anavyoona inampendeza, na sijui watakao baki nje ni akina nani, naamini watakuwa wale wa upinzani tu, maana hakuna jinsi, tusubiri tuone
 
Hapo wanw tafuta Posho tu ,nna ungana na wote walio sahauri kuwa Pesa yote iliyokuwa itumike ktk Kikao hichi cha Bunge itumike kupambana na Ugonjwa wa Corona.

Sababu hakuna tofauti ya Bunge kujadili na kupitisha Bajeti na kuipitisha bila ya kuijadili.Wanacho amua CCM na Bunge lao ndio huwa kinakuwa.Tumeona hivyo ktk Vikao mbalimbali walivyo kwisha kukaa na kupitisha waliyo yahitaji yawe.
 
Kama tunaweza kundesha vikao vya binge tena muhimu vya kupitisha bajeti ya nchi, kwa kutumia wabunge 150, kuna umuhimu gani wa kuendelea na utaratibu wa kuwa na idadi ya wabunge 300+?
 
Ndugu zangu wabunge, pamoja na taarifa za corona hapo Bungeni bado tu mnataka kuingia ndani ya ukumbi kujadili bajeti?

Tujali uhai kwanza

Miswada ya bajeti yote ikabidhiwe kwa wabunge, waisome kwa muda wa mwezi au wiki mbili,warudi na ndani ya siku moja waipitishe,kanuni zitenguliwe.

Ikibidi basi michango iwe kwa maandishi, na kuipitisha kura ipigwe kwa maandishi huko mliko,cha muhimu mchukuliwe kwamba kwa muda huo mnapoipitia bajeti mtatambulika mpo bungeni na posho mlipwe

Lindeni maisha,tunawahitaji sana
 
Wabunge Wako tayari.kufia ndani ya vikao kwa corona kuliko.kukosa posho ya vikao si unajua wanalipwa kila kikao

Wazo lako mleta mada zuri sana tu lakini hapo hakuna cha mbunge Wa CCM wala upinzani Huwa wanapishana na kubishana kwenye maeneo mengine yote ila ikifika eneo la posho na marupurupu ya mbunge huwa kitu kimoja utafikiri watoto Wa mama mmoja,baba mmoja na chama kimoja.Hapo huzika tofauti zao zote
 
Mabadiliko katika bunge la bajeti linaloanza Machi 31, Dodoma:

Hakuna maswali kwa waziri mkuu

Bunge litaanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni

Maswali na majibu yatatumwa kwenye 'tablets' za wabunge

Kura za kupitisha bajeti zitapigwa kwa mafungu

Waandishi wachache wataruhusiwa
View attachment 1404248View attachment 1404249
Wabunge wengine watakuwa wanahudhuria virtually. Na watakuwa wanachangia na kuuliza maswali. Sidhani kama ni tatizo kutengua kanuni za uendeshaji bunge kipindi kama hiki ambapo social distancing inahitajika kwa ajili ya kujikinga na maabukizi.
 
Back
Top Bottom