Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

anasema pesa ya tz imeshuka thamani kwa 8.5% ukilinganisha na dola ya marekani mwaka 2010 sababu ni kuimarika kwa dola ya marekani na mahitaji makubwa ya dola hapa nchini.
 
Eshacky
Nini maana ya swali la longeza ina maana muuliza swali hajaridhika na majibu ya waziri anataka ufafanuzi na swali la nyongeza always linakuwa jipya
Kwani si waziri angejibu tuu kuwa mchakato unaendelea kushughulikia hilo kama walivyozoea badala ya kusema swali ni jipya

bora amejibu hivo kwani angesema mchakato unaendelea lingekuwa jibu la kisanii zaidi, ila kwa hivo alivojibu tusubiri siku akija kujibu atatudanganya nini?
 
Sasa kama waziri anaulizwa anajibu hajui mnashangaa nini, wakati wengine wanaulizwa kwa nini WATANZANIA MASKINI anajibu hajui!
 
Mr Mak maswali mengi majibu yake ni kuwa mchakato unaendelea au mikakati ipo ndo maana majibu yao yanakuwa ya kisiasa zaidi na sio ya kiutendaji
 
Tanzania mortage refianance company kwa ajili ya mikopo midogo ningeomba msaada kwenye hii kitu maana .mkulo anasema imeanzishwa kuwezesha watu wenyewe kipato cha chini na wastani kuweza kukopa na kuweza kujenga nyumba......
 
Maganga
Kuna sheria mpya nafikiri ilipitishwa mwaka jana ya
Mortgage Finance ambayo dhamira yake kuu ni kusaidia na kuwezesha taasisi za fedha kutoa mikopo ambayo itawawezesha kujenga nyumba. Sijaisoma vizuri ila ngoja nikaipitie then will revert back to you hata PM nikuambie inaoperate kivipi
 
Itakapofika saa 9 kamili, mh. mkulo, Waziri wa Fedha ataingia na kabrasha lenye mambo yote kuhusu bajeti. Muda huo ndio ataanza kusoma, kesho na ijumaa itakuwa ni kupitia vifungu vya budget bt Discussion yenyewe itaanza j3.
 
Nnajua Watanzania tulio wengi wetu masikini tunatarajia sn bajeti hii ya Serikali itupe unafuu sbb ya hali ngumu tuliyonayo kwa sasa na tulipotoka na huko tunakoelekea.Nilimsikiliza vizuri sana Mwenyekiti wa Chama cha CUF mheshimiwa Ibrahimu Lipumba alipohojiwa na radio Maguc ya jijini Dar es Salaam.Alisema hii neema tunayoitazamia kutoka kwa viongozi wetu hakuna kitakachobadilika sana hali ngumu itazidi.
Alisema pia bajeti itakayosomwa kwa watanzania inatofautiana sn na bajeti waliyopewa wafadhili wetu.Akimaanisha tunayosomewa sisi ni ya maumivu lkn waliyopewa nchi wafadhili itawadanganya sbb ya unafuu unaotofautiana na hii ya wananchi.Ndugu yangu anafanya biashara ya magari juzi alikuja nyumbani akilalamika namna TRA walivyopandisha mapato ya kuingiza magari nchini.Wameshapandisha kabla hata ya bajeti kusomwa.Sasa je hii kodi waliyoipandisha kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha wa Serikali pesa hizo wanazipeleka wapi?Tuendelee kuyatarajia maumivu(hali ngumu ya maisha)tumepoteza matumaini na huko tunapoelkea mambo yatakuwa mabaya sana.Tupo hapa jamvini tutakuja kukumbishana siku za usoni.
 
Maganga bila wafadhili hakuna kitu mkuu na ndio hapo ninapokuambia wakigoma hakuna kitu katika bajeti ya Mkullo ni bla bla tuu
 
Mhe. Mdee, mtindo kandamizi wa makadirio mzgo wa magar badala kuangalia thaman halis ya mzigo. Je serikal inaongelea vip swala hili..
Spika anamwambia wazir km anaweza ajibu km hawez atajibu siku nyengine, wazir kakataa kulijibu, anasema ni jipya. Lilikuwa ni swala nyongeza.

kwa hiyo hajui kwa nini hayo makadirio ya nyongeza yapo pale bandarini?
 
Bajeti ijayo haiitambui mikoa mipya Send to a friend Sunday, 05 June 2011 21:34 0digg

mustafamkulo.jpg
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo

Boniface Meena
BAJETI inayotarajiwa kusomwa bungeni Juni 8, mwaka huu inaonyesha kuwa mikoa mipya iliyoanzishwa haijatengewa fedha za kuiendesha kwa mwaka wa fedha ujao.

Mikoa hiyo mipya ni Njombe, Simiyu na Geita ambayo kusudio la kuanzishwa kwake lilitangazwa bungeni mjini Dodoma mwaka jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akihitimisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti kwa ofisi yake.

Kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowasilishwa katika Kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala, mikoa iliyotajwa katika Bajeti ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mikoa iliyotengewa mafungu ni 21 tu.

Kati ya mikoa hiyo, Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na bajeti kubwa ya Sh 213.8 bilioni huku Lindi ukishika mkia kwa kuwa na bajeti ndogo ya Sh 56.0 bilioni.Mbali ya Dar es Salaam mingine iliyotengewa fedha nyingi ni Mwanza (Sh175.6 bilioni), Mbeya (Sh163.4 bilioni), Shinyanga (Sh141.3 bilioni) na Kilimanjaro wenye Sh138.0 bilioni.

Mikoa inayoungana na Lindi kwa kutengewa bajeti ndogo ni Rukwa Sh63.9 bilioni, Singida Sh63.8 bilioni, Mtwara Sh78.2 bilioni na Kigoma Sh72.3 bilioni.

Bajeti kwa mikoa yote hiyo 21 ya Tanzania Bara ni kiasi cha Sh2.3 trilioni.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alipoulizwa kuhusu suala la mikoa hiyo mipya kutotengewa bajeti alisema kuwa waziri anayeweza kuzungumzia suala hilo ni George Mkuchika wa (Tamisemi): "Mwulize Mkuchinka ndiye waziri ambaye ataweza kukueleza kuhusu hilo."

hata hivyo, jitihada za kumpata Mkuchika kutoa ufafanuzi zilikwama.Kamati ya Bunge ilipitisha mapendekezo ya bajeti hiyo ya Tamisemi na kuitaka kutoa kipaumbele katika miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zote nchini.

Mkuchika aliiambia kamati hiyo kuwa kati ya fedha hizo, Sh2.3 trilioni zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na zilizobaki zitatumika kulipa mishahara watumishi wake.Alisema kutokana na hali hiyo halmashauri nchini zitasimamia miradi yake na kuongeza mapato ambayo yatatumika kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

MIKOA MIPYA ILIYOANZISHWA

(i) Mkoa wa Njombe. Huu umezaliwa baada ya kumegwa na kuunganishwa kwa Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete kutoka Mkoa wa Iringa. Mkoa huu utakuwa na wilaya mpya ya Wangingombe ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Njombe.

(ii) Mkoa wa Geita. Huu unatokana na kumega na kuunganisha Wilaya za Geita kutoka Mkoa wa Mwanza, Bukombe kutoka Mkoa wa Shinyanga na Chato kutoka Mkoa wa Kagera. Mkoa huu utakuwa na Wilaya mpya ya Nyanghwale ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Geita.

(iii) Mkoa wa Simiyu. Unatokana na kumega na kuunganisha Wilaya za Bariadi kutoka Mkoa wa Shinyanga, Maswa kutoka Mkoa wa Shinyanga, Meatu kutoka Mkoa wa Shinyanga na Wilaya mpya ya Busega kutoka Mkoa wa Mwanza. Mkoa huu utakuwa na Wilaya nyingine mpya ya Itilima ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Bariadi.

MADHUMUNI YA KUANZISHWA MIKOA MIPYA

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais anaweza kuigawa nchi katika mikoa au Wwlaya. Hivyo, madhumuni ya kuanzishwa kwa mikoa hiyo ni kuboresha utendaji wa serikali kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya mikoa mama ili wananchi wapate huduma za kiutawala ngazi ya mikoa kwa karibu.
Mkoa wa Katavi ?
 
maganga
kuna sheria mpya nafikiri ilipitishwa mwaka jana ya
mortgage finance ambayo dhamira yake kuu ni kusaidia na kuwezesha taasisi za fedha kutoa mikopo ambayo itawawezesha kujenga nyumba. Sijaisoma vizuri ila ngoja nikaipitie then will revert back to you hata pm nikuambie inaoperate kivipi

asante mkuu tuko pamoja
 
TBC 1 LIVE Mustafa Mkulo anashusha mistari yenye vina kuhusiana na bajeti 2011 -2012 pata uhondo!
Mustafa-Mkulo.jpg
 
Back
Top Bottom