Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Eshacky nimekupata.
Kwa uelewa wangu maswali ya msingi huwa wanakuwa nayo kabla ila ya nyongeza yanatolewa hapo hapo. Sasa inategemea na nadhani kwa maelezo yako swali la Mdee may be lilikuwa nje ya swali la msingi.
Asante mkuu nimekupata
 
Eshacky nimekupata.
Kwa uelewa wangu maswali ya msingi huwa wanakuwa nayo kabla ila ya nyongeza yanatolewa hapo hapo. Sasa inategemea na nadhani kwa maelezo yako swali la Mdee may be lilikuwa nje ya swali la msingi.
Asante mkuu nimekupata

swadakta, ila kwa wazir anayejielewa km magufuli hawez akasema sijajianda.
 
Ila kwa waziri yoyote ambaye anaijua wizara yake at least ana majibu au angekuwa na majibu ya swali kama hilo au hata tuu kumjulisha muuliza swali wizara yake itashughulikia na kutoa majibu hata kwa maandishi kwa muuliza swali na sio kutoka na jibu kuwa hakujiandaa.
Sio kwamba waziri ni mwarobaini kwa kila kinachofanyika wizarani mwake ila at least yuko aware na mambo yanayofanyika ndani ya wizara na watendaji wake na at least ana uelewa na swali la Mdee
Mhhh hapo mkuu unaonaje
 
Mheshiwa spika kaandikiwa ki memo"mhe. Una kengeza hutuoni" anasema ye anaona vizur ila waombaj wengi. Anataja wageni, mi sionagi umuhimu wa hawa wagen kula muda wa bunge.
 
Elshacky unajua kwa wengine ni ujiko kutembelewa na wageni wana ule kama utoto kuwa umepata wageni wewe ni mashuhuri
 
Vipaumbele vya bajeti ijayo ni 1.nishati na umeme 2.usalama wa chakula 3.miundombinu 4.ukosefu wa ajira 5.mfumo wa bei
 
mkulo anasema jana rais alimsadia kuongea mengi ila kasema atayarudia sasa sijui jk alikuwa akifungua bajeti au?
 
Maganga Mweli we kwa kweli unaona hapo kuna kitu au ni bla bla maana bajeti yao karibu robo tatu ni posho na mishahara sasa hiyo robo kweli inatosha hayo yote kuhakikisha hata tunaondokana na janga la mgao wa umeme
 
Ansema hali ya uchumi duniani 2010 iliimalika na kasi ya uchumi ilikua mpaka 5% .pato la taifa kwa nchi zinazoendelea lilikua mpk 3%
 
mkuu swali la nyongeza, huulizwa baada ya swali la msingi, na swal la nyongeza linapaswa liwe na mada moja ya lile swal la msingi, na kumbuka mawazir huwa wanajiandaa na haya maswal, sasa km mbunge akauliza swal ambalo si mada moja ya swal la msing, hvyo inakuwa ngumu kwa wazir husika kutoa majibu sahih kwa kuwa hajajianda. Ni hivyo kwa uelewa wangu.

sasa kama anapewa maswali akayaandalie majibu, kwa hiyo anajipanga...kimsingi wangemalizana wenyewe huko huko...nia ya kuyaleta ktk National TV ni nini?
 
Mheshiwa spika kaandikiwa ki memo"mhe. Una kengeza hutuoni" anasema ye anaona vizur ila waombaj wengi. Anataja wageni, mi sionagi umuhimu wa hawa wagen kula muda wa bunge.

Thanks, Eshacky kwa uzalendo wako wa kutujuza kinachoendelea bungeni, Nashukuru sana mkuu
 
maganga mweli we kwa kweli unaona hapo kuna kitu au ni bla bla maana bajeti yao karibu robo tatu ni posho na mishahara sasa hiyo robo kweli inatosha hayo yote kuhakikisha hata tunaondokana na janga la mgao wa umeme

acha tu ndugu yangu sijui watatekeleza hawa ndugu zetu kweli hivi vipaumbele au ndo danganya toto.
 
Uhalisia ni kuwa kama nusu ya bajeti unategemea wafadhili ambao kwa sasa nao wamechoka au hawataki kuchangia bajeti yako inayowategemea wao hapo ndugu yangu elewa kuwa hizo ni porojo na bla bla kuwadanganya wananchi kuwa bajeti hii itakuwa nafuu kwao.
Hadi sasa hakuna mkakati maalumu wa kumaliza tatizo la umeme
Kilino ndo wala usiseme ni mikakati kwa mikakati isiyo na tija
Elimu huko ni balaa jingine na bomu linalosubiri kulipuka
Miundo mbinu duh wala usiseme
 
Bajeti ijayo haiitambui mikoa mipya

Sunday, 05 June 2011

mustafamkulo.jpg

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo

Boniface Meena

BAJETI inayotarajiwa kusomwa bungeni Juni 8, mwaka huu inaonyesha kuwa mikoa mipya iliyoanzishwa haijatengewa fedha za kuiendesha kwa mwaka wa fedha ujao.

Mikoa hiyo mipya ni Njombe, Simiyu na Geita ambayo kusudio la kuanzishwa kwake lilitangazwa bungeni mjini Dodoma mwaka jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akihitimisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti kwa ofisi yake.


Kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowasilishwa katika Kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala, mikoa iliyotajwa katika Bajeti ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mikoa iliyotengewa mafungu ni 21 tu.


Kati ya mikoa hiyo, Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na bajeti kubwa ya Sh 213.8 bilioni huku Lindi ukishika mkia kwa kuwa na bajeti ndogo ya Sh 56.0 bilioni.Mbali ya Dar es Salaam mingine iliyotengewa fedha nyingi ni Mwanza (Sh175.6 bilioni), Mbeya (Sh163.4 bilioni), Shinyanga (Sh141.3 bilioni) na Kilimanjaro wenye Sh138.0 bilioni.


Mikoa inayoungana na Lindi kwa kutengewa bajeti ndogo ni Rukwa Sh63.9 bilioni, Singida Sh63.8 bilioni, Mtwara Sh78.2 bilioni na Kigoma Sh72.3 bilioni.


Bajeti kwa mikoa yote hiyo 21 ya Tanzania Bara ni kiasi cha Sh2.3 trilioni.


Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alipoulizwa kuhusu suala la mikoa hiyo mipya kutotengewa bajeti alisema kuwa waziri anayeweza kuzungumzia suala hilo ni George Mkuchika wa (Tamisemi): "Mwulize Mkuchinka ndiye waziri ambaye ataweza kukueleza kuhusu hilo."


hata hivyo, jitihada za kumpata Mkuchika kutoa ufafanuzi zilikwama.Kamati ya Bunge ilipitisha mapendekezo ya bajeti hiyo ya Tamisemi na kuitaka kutoa kipaumbele katika miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zote nchini.


Mkuchika aliiambia kamati hiyo kuwa kati ya fedha hizo, Sh2.3 trilioni zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na zilizobaki zitatumika kulipa mishahara watumishi wake.Alisema kutokana na hali hiyo halmashauri nchini zitasimamia miradi yake na kuongeza mapato ambayo yatatumika kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.


MIKOA MIPYA ILIYOANZISHWA


(i) Mkoa wa Njombe. Huu umezaliwa baada ya kumegwa na kuunganishwa kwa Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete kutoka Mkoa wa Iringa. Mkoa huu utakuwa na wilaya mpya ya Wanging'ombe ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Njombe.


(ii) Mkoa wa Geita. Huu unatokana na kumega na kuunganisha Wilaya za Geita kutoka Mkoa wa Mwanza, Bukombe kutoka Mkoa wa Shinyanga na Chato kutoka Mkoa wa Kagera. Mkoa huu utakuwa na Wilaya mpya ya Nyang'hwale ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Geita.


(iii) Mkoa wa Simiyu. Unatokana na kumega na kuunganisha Wilaya za Bariadi kutoka Mkoa wa Shinyanga, Maswa kutoka Mkoa wa Shinyanga, Meatu kutoka Mkoa wa Shinyanga na Wilaya mpya ya Busega kutoka Mkoa wa Mwanza. Mkoa huu utakuwa na Wilaya nyingine mpya ya Itilima ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Bariadi.


MADHUMUNI YA KUANZISHWA MIKOA MIPYA


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais anaweza kuigawa nchi katika mikoa au Wwlaya. Hivyo, madhumuni ya kuanzishwa kwa mikoa hiyo ni kuboresha utendaji wa serikali kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya mikoa mama ili wananchi wapate huduma za kiutawala ngazi ya mikoa kwa karibu.
 
Najaribu kutafutahii key economic indicator 2010 ili wasio na radio na tv waisome kama kuna mdau anwaeza kuipata anaweza kutusaidia
 
Back
Top Bottom