Geee
JF-Expert Member
- Nov 11, 2012
- 465
- 93
m
BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.
BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.
Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.
Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za ms
Dr kilaza mwingine !!!mwenye CV yake aweke hapa aiseee