Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.
Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.
Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.
Wakati wa kutangazwa mshindi, inapaswa kila mgombea awepo.
JK hatokuwepo kwa sababu ...........................................