Bunge Jipya: CHADEMA yapaa, CCM yaporomoka!

Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.

Wakati wa kutangazwa mshindi, inapaswa kila mgombea awepo.

JK hatokuwepo kwa sababu ...........................................
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Tunachotaka kupima hapa ni asilimia ya ongezoko la viti vya CHADEMA toka 4 hadi 20, Kama alikuwa wanamiliki viti 4=100% navimeongezeka hadi 20=%? cross multiplication utapata jibu
 
Hivi vyama vilivyosimamisha wagombea Urais ni viwili tu? Mbona hatuongelei na akina Prof. Lipumba?
 
Kiukweli chadema imepaa vibaya mno, lazima dr slaa apongezwe kwa dhati na wanamageuzi wote big up sana. maana hata kama ccm imepata majimbo mengi lakini more than half ya wabunge wao ni mabingwa wa kuuchapa usingizi mjengoni na hata wale ambao hawalali they dont have positive contribution katika mambo yenye maslahi kwa taifa. lakini angalia umakini wa wabunge ambao chadema wamewapata-mdee,lissu,zitto,mbowe,shibuda,vicent nyerere,ndesamburo, wenje etc- QUALITY PEOPLE NA WAZALENDO haswa!!!!
 
Kweli Somo la hesabu ni utata mtupu!! huyu bwana makosini naona anaweza kuwa alichelewa kulia wakat anazalia i mean low score!
 
Weraweraaaaaa!!!!! Majiji yote yamechukuliwa na CHADEMA!!!!! CCM sasa wanakula MAPANKI ya siasa wakati CHADEMA wanakula vinono!!!
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Hawa vilaza wa chama tawala hawa wana matatizo sana!! Si bora ukae kimya badala ya kujiabisha hapa?? Au ndiyo nyie wa elimu ya chini ya mwembe na umepiga kura yako kwa ajili ya kofia na T-shirt!!

May be hizi ndizo design za wasomi wetu aliokuwa anawatetea Pasco kuwa wamekosea badala ya 70 million wameandika 700 million kwa ajili ya matundu manne ya choo jimboni kwa Kikwete!!
 
Nkosiyamakosini wewe hujaelewa kanuni nzuri aliyoitimia kuwapa asilimia. nafikiri amempongeza kwanza Dr kwa Ushindi alioupata na kukabilika na kupendwa na wananchi hata jizo kura za asilimia 60 % aliyopewa ni asilimia ya Dr slaa wamebadilisha tu, pia kazi ya kuwapata wabunge kwenye gome ya CCM na sehemu ambapo si rahisi ccm kuachia ila kutokana na sera makini ya dr slaa na imewafungua watanzania wengi macho na kukubali kumpa wabunge na madiwani ,hivyo yuko sawa kwani kutoak 4-mpaka 30 maana juzi walipata wabunge sehemu tofauti nafikiri huyu aliangalia ile chart ya tbc lakini wako zaidi, kwa kweli anastahili kupewa shahada ya heshima na mtu shupavu.
Mhh, hesabu gani hizo za asilimia 500, wakati ni ongezeko 4-20 + against 239-(4 +), be careful. thanks
 
[QUOTEd=The Dreamer;1225919]Sina shaka una mswaki (F) wa hesabu ndiyo maana mnashindwa kuchakachua bila kujulikana. UKiwa na maembe manne, ukaongezewa manne ni sawa na ongezeko la asilimia ngapi? Kama siyo 100%? Kama asilimia ni shida basi tumia folds na utaona ni ongezeko la 5 folds (au mara tano zaidi)!

CHADEMA has enjoyed an increase of 20/4 * 100 = 500%[/QUOTE]

safi sana kwa kumuelewesha huyu maana anaidhalilisha taaluma ya hesabu hafaham hata maana ya ongezeko la asilimia sasa kama mpaka hesabu ndogo kama hiz zinamshinda me namshaur akaanze kusoma hesabu upya
 
Sina shaka una mswaki (F) wa hesabu ndiyo maana mnashindwa kuchakachua bila kujulikana. UKiwa na maembe manne, ukaongezewa manne ni sawa na ongezeko la asilimia ngapi? Kama siyo 100%? Kama asilimia ni shida basi tumia folds na utaona ni ongezeko la 5 folds (au mara tano zaidi)!

CHADEMA has enjoyed an increase of 20/4 * 100 = 500%
duuh! Nyie Manambalistics ni noma kumbe enh! Ebanae kuishi Ungwinini nako ni upofu! Dah! Shukraa!
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Kama hujui hesabu siuache? Kwani lazima kila mtu aonekane anajua hesabu? Mwenzako kaongelea ongezeko la wabunge ndani ya chama na si ndani ya bunge. Kama ulikuwa unavitu kumi ukaongeza vitano utakuwa umeongeza kwa asilimia ngapi? Na kama ulikuwa navyo kumi ukaongeza vingine kumi utakuwa umeongeza asilimia ngapi katika vile ulivyokuwa navyo? Unajidhalilisha tu. Ukubali au ukatae, ukweli ndiyo huo CHADEMA wameongeza viti vya ubunge kwa asilimia 500
 
kimsingi mwaka huu watatukoma kutokana na hali ilivyo.watu wetu ni makini na damu bado inachemka tofauti na maajuza wao.
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Hivi ni lazima kuchangia hata vitu usivyovijua? - mara zote ukimya huficha umbumbumbu
 
Hivi vyama vilivyosimamisha wagombea Urais ni viwili tu? Mbona hatuongelei na akina Prof. Lipumba?

Lipumba ataongelewa kwenye vibanda vya kahawa sio hapa kwenye jukwa la watu wenye akili timamu! hata yeye anajua kuwa kesha-expire!
 
Pasco tena ushindi huo wa 500% zingatia umekamata majimbo yenye hadhi kama - Ubungo, Kawe, Ilemela, Nyamagana, Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Moshi Mjini - hii inaonyesha kuwa CCM hawakubaliki katika sehemu za mijini ambapo watu wana elimu ya uraia.

JK ataapishwa lakini akumbuke kuwa wananchi zaidi ya 60% toka Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Moshi na Iringa HAWAMTAKI yeye pamoja na chama chake.

Hii ni challenge kubwa sana kwa CCM hii miaka 5 ijayo. Pongezi zetu za dhati kwa DR. Slaa kwa kazi kubwa sana aliyoifanya akishirikiana na chama chake kwa Ujumla.

CHADEMA tunatakiwa tumfanyie sherehe ya kitaifa na kumpa taji kwa kazi kubwa aliyoifanya tena kwa muda mfupi sana. He is truly my hero!
 
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.

NI Kweli ila majònzi yangu ni kwa watanzania maskini ambao wameichagua ccm ukiangalia majimbo yote waliyoshinda ccm ni majimbo ya watz wenye shida na maskini kuliko wote ni majimbo yanayohitaji mabadiliko kuliko sehemu nyingi walizoshinda chadema
 
Hawa vilaza wa chama tawala hawa wana matatizo sana!! Si bora ukae kimya badala ya kujiabisha hapa?? Au ndiyo nyie wa elimu ya chini ya mwembe na umepiga kura yako kwa ajili ya kofia na T-shirt!!

huyu jamaa asikupe shida,
tatizo lake ni moja nalo ni kwamba alichelewa kulia wakati anazaliwa
 
Wana JF tusiwe diverted na viti 20 vya ubunge vya CHADEMA wakati kura za urais na majimbo mengine yameshachakachuliwa. Ni lazima tupate haki yetu na mengine yatafuata! Tunataka haki yetu yoote kwanza!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom