Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,304
- 2,080
Date::12/17/2009Waziri wa Sheria adai Bunge la sasa halina ubavu kwa serikaliNa Leon Bahati
WAZIRI wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe amezidi kutoa kauli tata baada ya kuligeukia Bunge la Jamhuri ya Muungano, akisema halina nguvu ya kuilazimisha serikali kufanya mambo na kwamba kazi yake ni kuishauri.
Hiyo ni kauli ya pili ya waziri huyo katika kipindi kisichopungua wiki moja baada ya kukaririwa Jumatatu akisema kuwa Rais Jakaya Kikwete hana uwezo wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi kwa kuwa mfumo wa utawala wa sheria hauruhusu vitendo kama hivyo.
Kauli hizo mbili zinazohusu mamlaka ya kisheria zimetolewa katika kipindi ambacho mjadala mkubwa wa hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa katika kashfa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) ukiwa umemgeukia rais.
Pia Chikawe ametoa kauli hiyo wakati Bunge likiishinikiza serikali kutoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio yake 23 dhidi ya wahusika kwenye kashfa hiyo kubwa iliyotikisa nchi baada ya Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu kutokana na ushauri uliotolewa na kamati teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo.
Serikali ilipiga chenga kuwasilisha taarifa hiyo kwenye Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri, hali ambayo inawafanya watunga sheria kusubiri kwa hamu maelezo kuhusu kashfa hiyo wakati wa mkutano ujao.
Lakini wakati hayo yakitokea, Chikawe ameibuka na maelezo mengine ambayo hakuna shaka kwamba yataibua mjadala mwingine mkali na hasa mamlaka ya mihimili mitatu ya nchi katika kipindi ambacho Bunge linaonekana kuanza kupata nguvu ya kuhoji na kuchunguza mambo ya serikali ambayo awali yalionekana kuwa nyeti.
Chikawe alisema kuwa hakuna namna ambayo Bunge hilo linaweza kuweka mguu chini na kusema lazima serikali itekeleze jambo fulani kutokana na nguvu ya chombo hicho kumezwa kisiasa.
"Katika mazingira haya ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, Bunge halina madaraka ya kulazimisha serikali itekeleze jambo," alisema Chikawe kwenye mahojiano na gazeti hili juzi.
"Hata pale yatakapotokea mazingira magumu kwa serikali, nguvu ya siasa itachukua mkondo wake na kuokoa jahazi."
Waziri huyo mwenye taaluma ya sheria alisema katika mfumo wa vyama vingi, wabunge wanawajibika kwa vyama vilivyowaptisha na kwa wananchi tofauti na mfumo wa chama kimoja ambao huwajibika moja kwa moja kwa wananchi.
"Hata serikali iliyo madarakani inawekwa na chama na inatekeleza sera za chama hicho kilichopewa ridhaa na wananchi," alisema Chikawe.
Alikiri kwamba wabunge wanaweza wakapandwa na munkari kama ilivyotokea katika suala la kashfa ya Richmond na kuibana serikali, lakini akasema mwisho wa siku watajikuta katika mazingira ya kuwajibika na kuwa kwenye msimamo wa kichama.
Chikawe hakuweka bayana kwamba CCM inaweza kumaliza vipi suala la Richmond, lakini CCM imekuwa ikitumia nguvu yake ya idadi kubwa ya wabunge kutuliza masuala ambayo yanaonekana kuwa magumu kwa serikali. Pia CCM iliwahi kutumia nguvu yake ya kisera kuzima mjadala wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ulioibuliwa na wabunge 55 mwanzoni mwa miaka ya tisini.
Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaita wabunge wote wa CCM katika mkutano wa pembeni na kuwaeleza kuwa sera ya chama hicho si kurejea kwenye serikali tatu, bali kuundwa kwa serikali moja na hivyo kuwataka kufuata sera za chama hicho wanapokuwa kwenye chombo hicho cha kutunga sheria kwa kuwa CCM ndiyo iliyowapa fursa ya kuchaguliwa kuingia bungeni.
Katika Bunge la sasa lenye watu 318, CCM ina wabunge wapatao 278 na hivyo kuwa na nguvu kubwa katika kufanya maamuzi yanayoibeba serikali.
Tangu kufikiwa kwa maazimio 23 ya Bunge dhidi ya kashfa ya Richmond mapema mwaka jana, serikali imekuwa ikisita kutoa taarifa ya utekelezaji wake zaidi ya kueleza kuwa Lowassa na mawaziri wengine wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha walijiuzulu na kwamba watendaji wengine waliandikiwa barua za kujieleza na walishafanya hivyo.
Hata hivyo, bado serikali haijaeleza kama imeshawawajibisha watendaji hao, akiwemo mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hoseah ambaye mamlaka yake ya kumwajibisha ni rais, huku watendaji wengine wakistaafu kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema serikali inatarajia kutoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio hayo katika mkutano ujao wa Bunge, lakini akasema binafsi anaona kitendo cha Lowasa kujiuzulu pamoja na mawaziri wawili kilichosababisha serikali kuvunjwa, ni hatua tosha kwa tatizo hilo.
Tatizo kubwa katika kashfa hiyo, alisema Chikawe, ni uzembe uliofanywa na watendaji wa serikali wa kutofanya uchunguzi wa kutosha ili kujua uhalali na uwezo wa kampuni ya Richmond.
Lakini akasema anaona suala hilo linakuzwa sana kutokana na kutumika kama silaha ya kukomoana kisiasa kwa kigezo cha mapambano dhidi ya ufisadi.
"Siasa nyingi zimeingia; watu wanatumia (Richmond) kumalizana kisiasa na ndio maana yamekuwepo malumbano yasiyoisha... sasa neno ufisadi linatumika kumalizana kisiasa," alisema Chikawe.
Kuhusu uwezo wa Bunge kuwa na mamlaka ya kuweza kumuondoa rais madarakani pale inapotokea kutokuwa na imani naye kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 46(A) ambayo inaelezewa pia na ibara ya 121 ya kanuni za kudumu za Bunge, Chikawe alisema:
"Katika mfumo wa vyama vingi nenda kokote duniani hata Uingereza, chama kilichounda serikali hakiwezi kikaachia na hadi kuona serikali yake inaondolewa na wabunge wake. Wataitana watawekana sawa (ili kuokoa jahazi)."
Alisema katika mazingira hayo ya vyama vingi, chama tawala kinaweza kuwachukulia hatua hata za kumfukuza uanachama mbunge au wabunge wanaoendesha shinikizo la kuiondoa serikali madarakani.
Alieleza kwamba hayo ni mazingira ambayo hayawezi kuepukika kwenye mazingira ya uendeshaji wa Bunge la vyama vingi, hasa ikizingatiwa kwamba mara nyingi wabunge hujikuta wakilazimika kukutana kivyama ili kuwa na msimamo katika jambo zito.
Alielezea mazingira hayo kuwa ndiyo yanakipa nguvu chama kilichounda serikali kuwa na nguvu bungeni na hasa pale kinapokuwa na wabunge wengi. Hata hivyo, Chikawe alisema chama kilicho madarakani kina wajibu wa kuhakikisha kwamba mambo yanaenda vizuri kwa manufaa ya wananchi wote, hivyo kila jambo la ukosoaji linapimwa na kuchukuliwa hatua kulingana na uzito wake lakini siyo kwa kushinikizwa.
Jamani naomba anayemjua kwa undani huyu waziri atupe background yake kwanza