Bunge Halina Ubavu wa Kuilazimisha Serikali - Chikawe

Sehemu ya utangulizi wa Katiba yetu unasema hivi:

KWA KUWA​
SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na
amani:

NA KWA KUWA​
misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika
jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na
Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha

wananchi (msisitizo wa italiki wangu)
 
Kweli mawaziri wa JK wengi ni watu wa ajabu sana. Kila kunapokucha Chikawe unakuwa hovyo kuliko ya jana, kuzeeka gani huko mkuu? Hovyo kabisa
 
Badala ya kutukana, soma KATIBA:-
Waziri Chikawe hajakosea. Amerudia yale yaliyowekwa wazi na KATIBA pamoja na Kanuni za Bunge. Maamuzi ya Bunge yanatokana na vikao vya kimaamuzi vya Bunge na ikibidi kura hupigwa na wengi wape. Waziri Chikawe alikumbusha kuwa tayari Serikali imeshapokea ushauri wa Bunge kuhusu RICHMOND.

IBARA YA 63
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

Katiba imebainisha namna Bunge inavyoweza kutumia madaraka yake-
63- (3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza–
(a) kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

Badala ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija kwa watanzania Bunge litunge Sheria Maalum kuhusu jambo husika.
 
Hivi hilo neno kusimamia halina Maana?
Na Je Bunge linapo piga kura ya kutokua na Imani naSerikali au raisi huwa wanamaanisha Nini? Kushauri???
 
Code:
Chikawe hawezi kupinga ufisadi kwani yeye mwenyewe ni fisadi; alikatiwa pochi ya EPA akaanzisha Petrol Station ya BP iliyopo kwenye junction ya Mwenge kuelekea Lugalo na Ubungo!! Anaindesha rafikiye ambaye ndio boya lake!! Kwa wale wanaokumbuka, chikawe alifukuzwa Ikulu alikokuwa anafanyakazi kwa tuhuma za utovu wa maadili leo hii bila kucheck background yake anapewa uwaziri tena wa wizara nyeti ya sheria kwa qualification ya uanamtandao!! What a disgrace.
Code:

Kama haya ni yakweli basi muungwana katuwekea maboya mengi chamani na kabinetini......wengine wana PHD za barabarani, wengine wametimuliwa Ikulu, wengine waropokaji utadhani fuse ya brain imeungua, wengine wapowapo tu. Taabu tupu! Its no wonder kuona ufanisi wa serikali hii ukiwa hivi ulivyo. Rais anakuwa na kazi ya kuzurura na kujibu mapigo, kwishney!
 
naamini chikawe kasema ukweli mchungu.
kwani amesema bunge halina ubavu na ameelezea kwa nini
amesema hivyo.

hata hivyo kauli yake ingekuwa na utata kama angesema "bunge halina mamlaka" ya kilazimisha serikali.... naamini hapo ungehitajika
msaada wa waliobobea katika masuala ya katiba na masuala
ya sheria zinazoelezea mamlaka ya bunge.

Mzee umesema yote hapo! Mbona hakuna mbunge hata mmoja asiejigamba kwa kumtetea JK? Upambanaji na kukumbatia ufisadi ni mbinu mbili tofauti zinazotumiwa na Wana CCM kubaki kwenye ubunge.
 
Chikawe hawezi kupinga ufisadi kwani yeye mwenyewe ni fisadi; alikatiwa pochi ya EPA akaanzisha Petrol Station ya BP iliyopo kwenye junction ya Mwenge kuelekea Lugalo na Ubungo!! Anaindesha rafikiye ambaye ndio boya lake!! Kwa wale wanaokumbuka, chikawe alifukuzwa Ikulu alikokuwa anafanyakazi kwa tuhuma za utovu wa maadili leo hii bila kucheck background yake anapewa uwaziri tena wa wizara nyeti ya sheria kwa qualification ya uanamtandao!! What a disgrace.

Mkuu wangu Bulesi, senksi nimeshagonga pia kule
Niliamua kutozungumizia historia ya Chikawe nikifikiri umri wake sasa unamsaidia kuacha 'utovu wa nmaadili'. Ila naona anastahli kabisa kukumbushwa aliyofanya (sina uhakika kama ameacha) akiwa mtumishi wa Ikulu hasa uzinzi wa kupindukia. Kwani ni wazi utovu wake sasa ni wa kisigina katiba ambao ni mbaya zaidi. Na inaelekea anafikiri watu hawajui 'uchafu' wake. Time will tell, aendelee kuchokonoa wananchi, watamchokonoa vile vile.
Kwa kuwa yuko hapa jamvini ni bora nimpe salamu zangu, Mkuu Chikawe ur damn... malizia mwenyewe aaaaaaaaaagggggggggghhhhhhhhhh!!!!!!!!
 
Sidhani kama inahusiano na matamshi yake

Tabia yake binafsi atajuana na Mungu wake

Lakini asituibie pesa na uchumi wa wananchi

Note: sisapoti alichosema lakini kufuatilia maisha ya mtu sirini si sawa..angalia majukumu yake anatimiza..na hazini na under age or hatumii ngono kugawa nafasi (rushwa) that is what matters for public
 
Hivi hilo neno kusimamia halina Maana?
Na Je Bunge linapo piga kura ya kutokua na Imani naSerikali au raisi huwa wanamaanisha Nini? Kushauri???

Mkuu siyo tu kusimamia,bali kipengele "e" kimeendelea kuainisha kuwa bunge hilo linatakiwa...

(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa
Cha kujiuliza sasa ni nani kasema mikataba inayohusu jamhuri ya muungano haihitajiki kuridhiwa na bunge?Kwasababu inavyoonekana ni kwamba masharti ya mikataba hiyo mojawapo ni kutokuridhia mkataba huo ujadiliwe na bunge,na hilo si kwa bahati mbaya,ila bado inawezekana wameivunja katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuimplicate kwamba rasilmali za Taifa hazihusiani na jamhuri ya muungano...Ama mikataba inayozihusisha rasilimali za taifa haihusiani na jamhuri ya muungano?
 
Mkuu siyo tu kusimamia,bali kipengele "e" kimeendelea kuainisha kuwa bunge hilo linatakiwa...

Cha kujiuliza sasa ni nani kasema mikataba inayohusu jamhuri ya muungano haihitajiki kuridhiwa na bunge?Kwasababu inavyoonekana ni kwamba masharti ya mikataba hiyo mojawapo ni kutokuridhia mkataba huo ujadiliwe na bunge,na hilo si kwa bahati mbaya,ila bado inawezekana wameivunja katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuimplicate kwamba rasilmali za Taifa hazihusiani na jamhuri ya muungano...Ama mikataba inayozihusisha rasilimali za taifa haihusiani na jamhuri ya muungano?
kama ni hivyo kufuatana na hicho kifungu (e) nk basi mikataba mingi tulioingia ni batili, na tunaweza kuifuta au kusimamisha utekelezi wake mpaka bunge liridhie, ni mategemeo yangu Tindu Lisu na Wengineo watatuelezea hili kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom